HISTORIA YA KANISA LA EFATHA.

Photo: APOSTLE N PROPHET MWINGIRA
Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira.
Huduma ya EFATHA yenye msingi wa Kitume na Kinabii, ilianzishwa mwaka 1996 na kuandikishwa kisheria hapa Tanzania mwaka 1997

Huduma hii imeinuliwa kwa majukumu makuu matatu;


1.   Kuponya watu kutokana na mateso ya magonjwa na madhaifu mbalimbali. 
2.   Kuwafungua watu kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya mwili, nafsi na roho. 
 3.  Kuliandaa kanisa la mwisho tayari kwa ajili ya unyakuo. 

Kanisa la Efatha wamedhamilia  kuwafikia wote waliokusudiwa na Mungu kwa njia mbalimbali kama vile
TV, Radio, Mitandao ya Kijamii kama Facebook, Twitter, Blog na Youtube. Pia kupitia Ibada, makongamano na warsha mbalimbali. Huduma ya Efatha chini ya mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira, ambaye ndiye Mkurugenzi wa huduma hii, ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa Tanzania na nje ya Tanzania ikiwa na makanisa zaidi ya 200 na makanisa zaidi ya 15 nje ya nchi.

Ni hakika kuwa Huduma hii imekuwa makimbilio ya wengi hasa wanyonge waliodharauliwa MUNGU amewainua na kuwathibitisha. 

Makao makuu ya Huduma ya Efatha yapo Kibaha Precious Centre, na kanisa kubwa lilipo Mwenge katika jiji la Dar es salaam, Tanzania. 

Mnakaribishwa watu wote katika ibada za kanisa la Efatha  zinazofanyika katika vituo mbambali vya Efatha ndani na nje ya Tanzania. 
Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira
Huduma ya Efatha imeanzia Tanzania na kuenea sehemu mbalimbali Afrika na nje ya Afrika. Hadi sasa Efatha ina vituo vya ibada Kenya, Zambia, Malawi, Rwanda, Afrika ya Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Marekani, Ulaya.
YESU ameniponya.
MUNGU akubariki sana.

BWANA YESU akiwa kazini Efatha baada ya kumponya mama.

Kibaha Precious Centre

Comments