NIFANYE NINI NIPATE KUURITHI UZIMA WA MILELE?

YESU aliulizwa swali hili na bwana mmoja aliye kuwa na hamu yakuurithi uzima huo,YESU akamjibu kwa swali wazijua amri, Jamaa akasema amezishika tangu utoto:YESU akamkazia macho akampenda akamwambia kauze vyote ulivyo navyo ugawie maskini kisha unifuate,jamaa akahuzunika hamu ya uzima wa milele ikamwisha akaondoka(Mark10:17-22).

Ndugu yangu pengine hata wewe una utamani UZIMA WA MILELE, lakini njia ni kuzishika amri na kuzitembelea katika matendo, jamaa alizijua amri lakini hakuziishi katika maisha yake ndio maana alipenda mali kuliko MUNGU kwani mali ilimfanya akatae kumfuata,angeshika amri angeacha vyote akaandamana na KRISTO,amri inahimiza UPENDO yeye hakuwa nao kwani hakuwajali maskini.



Mpendwa katika KRISTO ili uwe mrithi wa UZIMA wa MILELE,shika amri katika kweli Imani yako iambatane na Matendo:


Ni heri ukose vyote katika dunia hii bali umpate YESU yeye anasema ukimpata umepata vyote mara mia(Mark10:28-30) katika  Ulimwengu ujao yaani UZIMA WA MILELE.

YESU ANAKUPENDA AMBATANA NAYE LEO.

MUNGU akubariki sana.

Comments