TAMBUA NGUVU YA MUNGU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO.



BWANA YESU asifiwe Wana wa MUNGU.
Napenda kuleta kwenu somo hili:

                        Je Unakiri nini?

 “Nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU, (Matendo 1: 8).
Je, tunatumia hii nguvu ya MUNGU?
Na je tunaitumia  mamlaka ya KRISTO tuliyopewa kama inavyotakiwa?
Haijalishi mwana wa MUNGU unapita katika magumu kiasi gani, Unachotakiwa ni kubadilisha kukiri kwako, na kadri unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana,elewa kuna jambo katika ulimwengu wa Roho linafanyika, hata kama huna shilingi mia mfukoni wewe sema pesa zipo,  hata kama wewe ni mgonjwa umelala kitandani Sema mimi ni mzima, maana Neno la MUNGU  linasema aliye dhaifu na aseme ana nguvu.
 Ezekieli alipoonyeshwa lile bonde la mifupa mikavu, kwa macho  ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi.
Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa unabii na kuitabiria ile mifupa, akaiambia  ’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi.’’  Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni jinsi gani Ezekiel ialivyoweza kutumia nguvu na uweza ulioko ndani ya kinywa chake na kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana wa MUNGU nini ni kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako?
-Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena,
-au ni uchumi wako,
- afya yako,
-watoto wako,
-hudumayako,
MUNGU anakuambia leo simama na uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.


Unakiri nini kushindwa au kushinda?
Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote yanayoonekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO mwenye nguvu zote. AMEEEN.
MUNGU awabariki sana.  
Emma E. Lyimo.
Cell: 0756 496 496

Comments