BWANA YESU
asifiwe.
Karibu
tujifunze kweli ambayo huwaweka watu huru kutoka kwenye utumwa wa mambo mabaya.
Yohana
8:31-31 ‘’ Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
‘’.
-Huwezi
kuwekwa huru pasipo kweli.
-Neno la
MUNGU ndio kweli.
-Neno la
MUNGU huweka huru.
-Neno la
MUNGU ndio kweli inayodumu milele.
-Alichokisema
MUNGU ndicho neno lake.
-Neno la
MUNGU ni hakika na amina.
Neno la
MUNGU linayajua mawazo ya kila mwanadamu.
-Hakuna jambo
ambalo linaweza kujificha mbele ya Neno la MUNGU.
Siku moja BWANA
YESU na wanafunzi wake walikuwa wanatembea kutoka mji mmoja kwenda mji
mwingine. Njiani YESU akaulaani mti na kuendelea na safari, walipomaliza huduma
huko wakarudi, wanafunzi wake walipofika pale kwenye ule mti wakakuta ule mti
uliolaaniwa umekauka kweli, ikabidi wamuulize BWANA YESU kuhusu jambo hilo.
BWANA akajibu, akawaambia ‘’Mwaminini MUNGU’’ . Neno hilo la BWANA YESU sio
dogo ni kubwa sana, sio watu wote
wanamwamini MUNGU, wengi wanamwamini kwa midomo yao tu lakini ikitokea jaribu
kidogo tu uaminifu wao hutauona. Lakini mtu ambaye kweli imemweka huru , huyo
lazima awe na imani timilifu kwa MUNGU maana kweli ya MUNGU imemweka huru.
Ndugu yangu
tamani sana neno la MUNGU siku zote, tamani neno ambalo halijaghoshiwa wala
kuwekewa matakwa ya binadamu ndani yake.
Watu hutenda
dhambi kwa sababau kweli haimo ndani yao, kweli ni BWANA YESU.
Yohana 3:31’’Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili
yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka
mbinguni yu juu ya yote.
‘’.
-Aliyekuja
kutoka juu ni BWANA YESU.
Biblia pia
kuna sehemu inasema ‘’ Amebarikiwa ajaye kwa jina la BWANA’’. YESU yuko juu ya
yote, ukimpata yeye umepata vyote, yeye ni kweli ya milele, yeye ni Neno la
MUNGU, yeye alifanyika mwili ili atukomboe, atuokoe na atuweke huru. Neno lake
hutuweka huru, jina lake hutuweka huru, Damu yake ni ulinzi kwetu. Ni faida kuu
kuwa na BWANA YESU.
Ndugu yangu
utakuwa huru kama tu neno la MUNGU utalipa nafasi maishani mwako.
Wala
usikubali kuwa msikiaji tu wa neno la MUNGU bali uwe mtendaji wa neno.
Neno la
MUNGU ni kweli ambayo inaweza kumbadilisha mtu kutoka kwenye ukahaba na kuwa
mchungaji, kutoka Ujambazi na kwa Mhubiri, kutoka mchawi na kuwa Askofu, kutoka
mnajimu na kuwa Mwanamaombi, kutoka kuimba nyimbo za shetani na kuimba nyimbo
za injili.
Tuliruhusu
tu neno la MUNGU lifanye kazi yake maishani mwetu. Kubali ndugu kubadilishwa na
Neno la MUNGU.
Yohana 17:17
‘’Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
‘’
-Neno la
MUNGU ndio kweli, sio kukimbilia miujiza tu huku neno hulitaki, bali taka neno
la MUNGU na miujiza kwako itakuja.
-Miujiza
haimfikishi mtu mbinguni bali ukilitii
neno la MUNGU siku zote za maisha yako, utafika mbinguni.
- Ukilikataa
neno la MUNGU unakataa uzima.
-ukilikataa
neno la MUNGU unakaribisha matatizo.
Yohana 1:12 ‘’
‘’
-Ndugu zangu
tumepewa uwezo wa kushinda dhambi.
- Tumepewa
uwezo wa kufanyka watoto wa MUNGU.
Mtoto wa
MUNGU ni Yule aliyempa BWANA YESU maisha yake.
Zaburi 125:1
‘’Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;
‘’.
KWANINI
TUNAJIFUNZA NENO LA MUNGU?
1. Tunajifunza
neno la MUNGU kwa sababu Neno la MUNGU huleta tabia ya uungu ndani yetu.
2. Tunajifunza neno la MUNGU kwa
sababu MUNGU huliangalia neno lake ili alitimize kwetu.
3. Tunajifunza neno la MUNGU kwa
sababu neno la MUNGU ndio mpango wa MUNGU katika maisha yetu.
4.
Tunajifunza neno la MUNGU kwa sababu Neno la MUNGU ndio kweli inayodumu
milele.
5. Tunajifunza neno la MUNGU kwa
sababu, kwa neno hilo tutapata uzima wa milele.
6. Tunajifunza neno la MUNGU kwa
sababu adui yetu ibilisi anaogopa neno la kweli la MUNGU kama sisi wateule
tukilitumia ipasavyo.
7. Tunajifunza neno la MUNGU kwa sababu
neno hilo ni sauti ya MUNGU ya kutuongoza katika maisha yetu yote.
Ni heri
kulitendea kazi neno la MUNGU.
Ni heri
kuliishi neno la MUNGU.
Isaya 55:11 ‘’ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu;
halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa
katika mambo yale niliyolituma.
‘’
Neno la MUNGU lina mamlaka kuu.
Neno la MUNGU ndio katiba ya watakatifu.
Neno la MUNGU ndio chakula cha uzima war oho zetu.
Tunalihitaji
neno la MUNGU siku zote za maisha yetu.
Comments