MASANJA MKANDAMIZAJI ANAKARIBIA KUFUNGA NDOA.


Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili na amabaye pia Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi , Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji’ amesema yupo kwenye mipango na maandalizi ya kufunga ndoa kabla mwaka huu haujamalizika.

Akizungumza na kituo cha redio cha Praise Power, wiki iliyopita , Masanja amesema kuna maandalizi ambayo anayafanya ili kukamilisha mchakato huo.

“Namwamini Mungu huu mwaka hauzami,” alisema. “Pale kitandani tutakuwa tunalala wawili na katika kitu nimekimisi nafikiri ni ile kamba ya kuanikia nguo nyumbani, itakuwa hata inanilaumu, haina hata nguo mchanganyiko. Inapendeza unapita pale nyumbani kwetu unaona pale tumeanika kasuruali, kanga, sketi. Natamani ile kamba yangu ya nguo ifanye vitu mchanganyiko, lakini ninamwamini Mungu, mwaka huu mwishoni mwishoni ukipita nyumbani utakuta kamba ina mchanganyiko wa nguo,” aliongeza.
 
 
MUNGU akuwezeshe mchungaji mtarajiwa.
 

Comments