MBINU AMBAZO SHETANI HUZITUMIA KUHARIBU

Na RP Adriano, Ufufuo na uzima Kilimanjaro,Moshi.

Jana tuliangalia kwamba ili mtu apate kitu fulani anahitaji nguvu za kumwezesha na nguvu za rohoni. Kumbukumbu 8:18

Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Pia tuliona 3Yohana1:1,2  anasema ufanikiwe kama roho yako ifanikiwavyo. Mafanikio makubwa na madogo yanaanzia rohoni.

Efeso 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake KristoHapa tunaona kitu chochote kiwe chema au kibaya kinaanzia kwenye ulimwengu war oho, na kuna viumbe wakaao kwenye ulimwengu war oho wanaouongoza ulimwengu wa roho na wanaleta madhara katika ulimwengu wa mwili. Na ukitaka kushinda lazima ushinde, utawale, au upate nguvu za kutawala kwenye ulimwengu war oho kwanza ndipo utashinda kwenye ulimwengu wa mwili.
Tulishapewa nguvu na kristo katika ulimwengu wa roho, Efeso 2:6 “Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu


Ni ajabu kama mtu ataamua kupigana na mtu asiyemjua aina za silaha zake, anakaa kwenye maeneo gani n.k. vivyo vita yetu ni kupigana na viumbe vya kiroho na hivyo tunahitaji nguvu ya rohoni ili tupate kushinda, Baraka zetu zinaanzia rohoni kwanza ndipo mwilini, na hapo haijalishi nani kazifunga au nani anazuia bali katika jina la Yesu tunazichukua, na hata kama wa wakituona wa kawaida bado sisi si wa kawaida, tuna nguvu za kiroho, maadaui zetu wanatujua, na hatuachi adui atuonee hata tumgeuzie upande wa pili. Mwenye nguvu hakubali kuonewa, na mtu hamwonei mtu mwenye nguvu kwa kuwa anamzidi nguvu na VIVYO KWA shetani hatukubali kuonewa na shetani kwani tunazo nguvu za kushinda, tutawapigapiga wachawi, waganga na wote wanaoleta matatizo kwenye maisha yetu.

Shetani huja na kuwaonea watu kwa akili lakini kwao wenye nguvu za Mungu za rohoni hushinda hila hizo, mfano ni Farao asiyemjua Yusuphu alipanga kwa hila kuwaua watoto wa waebrania, lakini wazalisha hawa walikuwa na nguvu za rohoni wakamshinda Farao, na baadae akaja na mpango wa pili bado mama yake Musa akamhifadhi hai mwanawe kwa ujanja. “Kutoka 1:8-22”
RP Adriano akihubiri
Nawe uwe na nguvu kuliko wanawake wa kimisri, uwashinde wanaotaka kuua Baraka zako, wanaopigana na familia yako na umshinde adui yako katika jina la Yesu. Mipango yote ya farao kuwaua watoto wa waebrania ilikuwa ni kuharibu ukombozi wa Israel lakini watu hawa wakiwa na nguvu za rohoni wakashinda haya yote na makusudi ya Mungu yakatimia kwao kama alivyowakusudia, NA IWE KWAKO PIA maadui zako uwashinde kwa nguvu za rohoni ufanikiwe rohoni na mwilini waone na kujua Mungu wako ndiye atawalaye.

 Ezekiel 28:1-10.
RP Adriano akihubiri

Wakati Yesu alipozaliwa utaona walikuja mamajusi wa mashariki kumshuhudia kwa nini? Walimwona ni kweli ana sura na umbo la mtoto lakini rohoni ni mfalme wa wafalme, nah erode alikuwa akitaka kumuua mtoto Yesu, kwa kuwa aliona ukuu wake rohoni na alipokufa Malaika akamtokea Yusuph kumwambia rdi Yerusalemu kwa kuwa aliyetaka kumuua mtoto amekufa. Katika jina la yesu kristo tunatangaza kufa kwa wote waliotaka kuua maisha yako, waliotaka kuua roho yako, waliotaka kuua ndoa au mchumba wako kwa damu ya yesu, kila alitaka kukuharibia mafanikio yako afe yeye kama Herode ili wewe uendelee na malaika wa Bwana akutokee usiku wa leo. Maana amekufa aliyekutafuta akuue, amekufa aliyetafuta kuua biashara yako, amekufa kila mwenye kuzuia makusudi ya Mungu kwako pokea ushindi wako kwa jina la Yesu maana amekufa aliyekutesa. AMENI

AP Hosea akimkaribisha RP Adriano mapema leo na umati wa watu ukishangilia

Comments