Peter Michael Mabula Kwenye huduma: Hapa nikiwa na wateule wa BWANA YESU huko Chalinze Mkoa wa Pwani. |
BWANA YESU
asifiwe ndugu.
Karibu
tujifunze ujumbe huu wa tutuimarisha katika safari yetu ya kwenda mbinguni.
Nilipookoka
kulikuwa na changamoto ambazo zilikuwa zinanikabili, kwanza sikujua kuomba
kabisa, nilichokuwa nafanya ni kwamba, wakati wa maombi ya wote nilikuwa
namuiga mchungaji anavyoomba, yaani kila neno analotamka na mimi nalitamka kwa
sauti ya chini. Nilitamani sana kujua kuomba kwa muda mrefu na kwa kweli hata
mwezi haukufika nikawa najua kuomba hata nusu saa bila kukoma.
Ndio
nilikuwa nimezaliwa kiroho kama Biblia inavyosema katika Yohana 1:12-13( Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.
).
Baada ya
kuzaliwa mara ya pili na kuwa mtoto wa MUNGU nilitakiwa kukua kiroho kwa
kuzingatia mafundisho kanisani. Namshukuru MUNGU nilifaulu kwa hilo la
kuhudhuria mafundisho, Siku kadhaa
baadae ROHO MTAKATIFU alisema nami kwa njia ya andiko, nikasikia sauti ikisema ‘’Mtu
hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo kwa MUNGU’’ Nikatambua kwamba
natakiwa kufunga, kweli kesho yake nikaanza kufunga na kuomba.
Zilikua ni
hatua za kuukuliwa Wokovu.
Kama kimwili
kuna kukua kuanzia mtoto mchanga, mtoto, kijana, mtu mzima na mzee, hata kiroho
ni hivyo hivyo ila kwa sasa sijui kama nimefikia umri gani kiroho ila nauhakika
sio mtoto mchanga wala mtoto kiroho.
Nimekueleza
mambo hayo kunihusu mimi huku nikiamini kabisa kwamba hata wewe uliyeokoka kuna
mapito uliyopitia katika kuukulia wokovu. Maombolezo
3:27 ''Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.''
Nira
inayozungumzwa hapa ni kumpokea BWANA YESU na kujifunga nira yake ambayo ni
laini, Ni vema sana kuokoka ukiwa kijana , sio kuwa na mawazo ya kuokoka ukiwa
mzee huku huna uhakika hata asilimia 1 kama utafika uzeeni.
Ndugu ulifanya
vyema sana kumpokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yako. Baada ya kuwa ni
mzima kiroho yaani wewe huwezi kupeperusha na upepo wa kumwacha KRISTO mwenye
uzima wako wa milele, Huwezi kuyumbishwa na mafundisho potofu au mafundisha
manyonge.
Unaenenda
kwa roho wala hauzitazamii tamaa za
mwili.
Kwa
kuzingatia hayo yote juu, unafanya vyema sana lakini hapa kuna mambo 7 ya
kuzingatia na ya muhimu sana kwako ili tu tumpendeze MUNGU wetu na kuenenda
vizuri katika Wokovu wako ambao ni wa thamani sana.
Nazungumzia
SIFA 7 ZA KIJANA ALIYEOKOKA.
Vijana ndilo
kundi ambalo linawindwa sana na shetani na wachawi kwa sababu umri huo ndio
umri wa kuchagua maisha ya kuishi, shetani anajaribu kwa kila mbinu ili tu
kijana achague kumtumikia shetani na sio MUNGU aliye hai. Vijana tunatakiwa
tuwe Macho sana na tusikubali kuamua kuishi maisha yaliyo nje na KRISTO YESU.
Biblia
katika 1 Yohana 2:14 Inasema ‘’ Vijana tuna NGUVU, Neno la MUNGU liko ndani
yetu na TUMEMSHINDA shetani.
Vijana
wakiamua kumshinda shetani , hakika wanamshinda maana wana nguvu, hata wakisema
watembee kilomita 20 kwenda kwenye maombi wanaweza maana wana nguvu.
Vijana
waliookoka wanatakiwa Neno la MUNGU liwe ndani yao ili wasiyumbishe na dhambi
na kila cha shetani.
Tumemshinda
shetani na tukiamua kumshinda tutamshinda siku zote, jambo la kufanya ni
kuhudhuria mafundisho kanisani , kuwa mwana maombi, kukisoma na kulitafakari
neno kila mara, Kumtii MUNGU, na kufanya kazi ya MUNGU.
SIFA 7 ZA KILA KIJANA ALIYEOKOKA.
KILA KIJANA
ALIYEOKOKA LAZIMA AWE NA.
1.
UTII.
Kutii ni
kitendo cha kuyapokea maagizo na kuyatekeleza. 1 Petro 5:5-7 ‘’ Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini
wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa
sababu MUNGU huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa MUNGU ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
‘’
BWANA YESU ni mfano hai kwetu maana alipozaliwa na Mariamu aliendelea kukua kiumri lakini akimpendeza MUNGU na wanadamu pia, na hata sisi katika maisha yetu vijana tunatakiwa tumpendeza MUNGU na wanadamu pia.
1 Samwel
2:26 ‘’ Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.
‘’
2.
KUWA
MTU WA KUTAFAKARI NENO LA MUNGU.
Yohana 8:31 ‘’Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
‘’
-Kukaa kwenye neno ni kujifunza neno na kulitafakari neno .
Mithali 1:7 ''Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.''
-Lazima vijana tuwe karibu na mambo ya MUNGU.
3.LAZIMA UWE
VIELELEZO.
1 1
Timotheo
4:12 ‘’ Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio,
katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
‘’
4.LAZIMA UWE NA HEKIMA.
4.LAZIMA UWE NA HEKIMA.
Mhubiri 4:13 ‘’ Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu.
‘’
5. UKUMBUKE HUKUMU.
5. UKUMBUKE HUKUMU.
Vijana wengi kwa sababu ya uhuru
wa maamuzi hujikuta wakifanya dhambi, kumbe kuna hukumu. Mhubiri 11:9-10 ‘’ Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na
moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo
wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa
ajili ya hayo yote MUNGU atakuleta hukumuni.
Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.
‘’
6.KUMKUMBUKA MUNGU.
Mhubiri 12 :1 ‘’ Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo
mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika
hiyo.
‘’
7.KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUWEKA MALENGO
MAZURI.
Mithali 13:16(Kila aliye na busara hutenda kazi kwa
maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. )
Neno
la mwisho kwa leo kwa vijana ni hili.
1 Thesalonike 4:1-12 (Iliyobaki, ndugu,
tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika BWANA YESU; kama mlivyopokea
kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza MUNGU, kama nanyi mnavyoenenda,
vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa
kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa BWANA YESU. Maana haya ndiyo mapenzi ya MUNGU, kutakaswa kwenu,
mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili
wake katika utakatifu na heshima; si
katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua MUNGU. Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo
hili; kwa sababu BWANA ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama
tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. Maana
MUNGU hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali MUNGU,
anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na MUNGU kupendana.
Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana. Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote. )
Kwa sasa naishia hapo,
MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea
BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu
kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani
aliko KRISTO BWANA.
mabula1986@gmail.com
Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na MUNGU kupendana.
Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana. Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote. )
Comments