PETER MABULA AMVISHA MTU PETE YA UCHUMBA.

Tukio lenyewe ndio hili. Asante YESU kwa wema wako kwa kuwa wewe BWANA unaweza kubariki.
BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.
Namshukuru sana BWANA aliye MUNGU kwa uzima na kwa tukio la leo ambalo bila yeye lisingefanyika . Kwangu yote ni MUNGU tena ametenda kwa utukufu wake (Zaburi 83:18).
Leo tarehe 17 August 2014 mimi Peter Mabula nimemvisha Pete ya uchumba Scholar Mungusa na uchumba kutangazawa rasmi.
Nikiwa na msimamizi wangu Pius
Namshukuru sana BWANA YESU kwa hili. Hatua ya uchumba imemalizika, Hatua ya Ndoa inafuata na hatua ya maisha ya ndoa itafuata.
Tukio hili lilifanyika katika kanisa letu la Kawe Pentecostal Church(KPC) na liliendeshwa na Mchungaji Kiongozi Elly Boto.
Hizi hapa picha katika tukio hilo.EMENITENDEA, AMENITENDEA. EMANUELI AMENITENDEA.



Tunamtazama bibi harusi mtarajiwa akija mbele.

Scholar baada ya kuitwa mbele na Mchungaji.

Namshukuru sana MUNGU kwa tukio hili.


Mchungaji Elly Boto akinyanyua juu pete ya uchumba ili watu wote waione.

Wachungaji wakitukabidhi kwa MUNGU kwa maombi.


Wakati wa maombi lakini leo nilishtuka kidogo baada ya kupewa na Scholar  zawadi ya ua.

Tukiwa pamoja na wateule wa MUNGU .


Tukiwa na marafiki.

Asante BWANA YESU kwa wema wako.

Tukiwa na wasimamizi wetu.

Kumtumikia MUNGU ni raha sana.


Scholar na marafiki zake.

Scholar na wadogo zake.


Scholar na msimamizi wake Tobietha.




Scholar katika pozi.

Mimi furaha yangu ni kuwa na YESU KRISTO maishani mwangu.

Peter Mabula na Scholar Mungusa.





Comments