VIJANA WA ASKOFU KAKOBE WAHUBIRI INJILI KALI SANA MITAANI, SHUHUDIA INJILI HII.

Askofu Zacharia Kakobe ambaye ni mbeba maono wa huduma yaFull Gospel Bible Fellowship(  FGBF), Kulia na kushoto ni maaskofu wa kanisa hilo kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania. Hongereni sana FGBF kwa kazi nzuri ya BWANA na hakika mmemzalia BWANA YESU matunda mengi.
Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship; Maumini  waliotoka mikoani waliungana na wenzao wa Dar es salaam na kusambaa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam  kwenda kubiri Injili iliyopokelewa kwa furaha na wengi.

Hizi hapa ni baadhi ya picha katika matukio ya kuhubiri mtaani yaliyofanya na watumishi wa MUNGU kutoka FGBF wakati wakiwa katika kuadhimisha miaka 25 Tangu huduma hiyo kuanzishwa.

Injili ikihubiriwa na wana FGBF Kariakoo.Dhambi Ni Mbaya, Uongo Ni Mbaya, Uzinzi Ni Mbaya Sana, Uasherati Haufai, Rushwa Haistahili, Masengenyo Ni Machukizo. Tusiishi Kwa Sababu Uongo Na Utapeli Umekaa Ndani Yetu Bali Tuishi Kwa Sababu YESU KRISTO Mwana Wa MUNGU Aliye Hai Anaishi Ndani Yetu.
 Ndugu Njoo Kwa YESU Ujisalimishe Maana Dunia Imeharibika Tena ina Wayawaya. Kwa Miaka Mingi Sana Umeyawaza Ya Dunia Lakini Bado Hujayapata, Nakuomba Waza Uzima Kuanzia Leo, Waza Kukombolewa Na Damu Ya YESU, Waza Mbinguni
YESU KRISTO anaokoa, ukiamini leo unaokoka. Mpokee leo awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yako. duniani hapa sisi sio wakaaji bali wapitaji,  na kwa sababu ni wapitaji basi tutengeneze uwezo wa kwenda uzimani na sio motoni, njia pekee ya kutupeleka uzimani ni kumpokea BWANA YESU ili atuokoe maana hakuna uzima kwingine( Yohana 14:6, Matendo 4:12)
Maana nimewekewa shart! Ole wangu nisipoihubiri injili. Ewe mwanadamu tambua ya kwamba YESU anakuita ili uokoke, YESU hajawahi kuchoka kukuita na leo ukiisikia sauti yake usiufanye moyo wako kuwa mgumu, Wokovu ni sasa na hakuna nafasi nyingine ya kutubu baada ya kufa bali kutubu ni sasa ukiwa hai na BWANA YESU yuko anakusubiri tu wewe umpe maisha yako, Fanya hima ndugu yangu maana dunia itapita, njoo kwa YESU leo.
kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
Yohana 3:16-21 inasema  ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.
Ndugu yangu  Siku Ukifa Hakuna Awezaye Kukuamsha, Ndugu Na Jamaa Zako Watalia Sana Lakini Hata Hivyo Hutawasikia. Swali kwako ni hili,  Ndugu Yangu Ukifa Utapenda Uwe Mgeni Wa Nani? Je Ungependa Uwe Mgeni Wa MUNGU Au Mgeni Wa shetani? Najua Kila Mtu Anataka Akifa Awe Mgeni Wa BWANA, Lakini Je Umeukubali Kabla Hujafa Huo Mwaliko Wa MUNGU, Je Umempokea YESU Ili Akupe Tiketi Ya Kwenda Mbinguni? Je Umempa BWANA YESU Maisha Yako Ili Siku Ya Kufa Kwako Amtume Malaika Wake Aje Akuchukue Na Kukupeleka Mbinguni?

Comments