YALIYOJIRI SIKU MOSES KATINDASA AKIFUNGA NDO.

Moses Katindasa na mkewe.
MUNGU anajibu maombi na anatenda pale ambapo wanadamu hawawezi .
Rafiki yangu na mtumishi wa MUNGU Moses Katindasa hatimaye amefunga ndoa takataifu Kanisani. Ni furaha kuwa ndani ya YESU ni furaha kumtegemea MUNGU.
Ndoa ilifungwa katika kanisa ni KKKT kinyerezi  na zoezi hilo liliendeshwa na mchungaji kiongozi Kijalo. ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIKITENGANISHE.

“Apataye mke (mume) apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA “-Mithali 18:22

Ningeambia kufungisha ndoa ningefundisha yafuatayo.

1 Wakorintho 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.”


Napenda uelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo.

Waefeso 5:23 “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.”

1Timotheo 2: 9 – 10 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.”

1 Petro 3:7“Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa AKILI; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe”
Waefeso 5:33 “Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.” Upendo ni nguzo ya Pili na pia ni moja ya tunda la Roho katika ndoa. Hapa naomba nieleze hii ndoa inayoongelewa ni ya Kikristo hivyo upendo huu hauwezi kuutenga na upendo wa Kristo kwa ujumla, je upendo unaelezwaje katika Biblia
1 Timotheo 5:8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”

 HIZI HAPA BAADHI TU YA PICHA KATIKA TUKIO HILO AMBALO LILIFANYIKA KANISA LA 




''Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake cahpita kima cha marijani'' Mithali 31:10

Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe”

Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.”
Moses na Mke wake.
Wakati wa kuvalishana pete ya ndoa.
Kwa YESU KRISTO ni raha.
Ndugu na marafiki.

Comments