ALBAMU YA "SHILOH" NA "ZWADI GANI" YA JOY BAND KWA APOSTLE JOHN KOMANYA KUZINDULIWA 05 KTOBA 2014


Kundi la Joy Band lililo chini ya Apostle John Komanya (JK) siku ya tarehe 5 Oktoba 2014 wanatazimia kuachilia albam ya DVD yenye jina la Shiloh albam yenye nyimbo 8. Sambamba na Uzinduzi wa Albam ya shiloh siku hiyo pia wata zindua DVD ya Wimbo wa "Zawadi Gani".

Uzinduzi wa Albam hiyo Itafanyika katika Ukumbi Wa Kisasa Maeneo ya Sinza barabara ya "Makaburini" karibu kabisa na Ukumbi wa Mwika. Uzinduzi huo utafanyika kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 1 usiku na mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo atakuwa Mhe. William Ngeleja.



Kiingilio Kwa ajili ya Tamasha hilo itakuwa ni shilingi 5,000 viti vya kawaida, Shilingi 10,000 VIP na watoto shilingi 3,000.

Akiongea na Waandishi wa habari kwenye Ofisi za Kiango Media, Msemaji wa Tamasha hilo Ze Blogger Samuel Sasali alieleza kuwa Mke na Mume (Couples) watakaokuwa wamevalia kwa kupendeza watapata Chakula pamoja na Joy Band na Kisha watapata Usiku wa Mapumziko kwenye hotel ya Kisasa yenye hadhi ya nyota 3. Na Singles Wa kike na kiume watakaokuwa wamependeza watapata chakula cha pamoja na Joy Band pasipo offer ya Kulala.

Kazi ya Utengenezaji wa Video hiyo imekwisha kamilika na kwa sasa Band Iko katika Mazoezi katika Mkoa wa Pwani Eneo la Msata.

Apostle JK katika Kazi zaidi..


Director Fred akiwa kikazi zaidi

Apostle JK pamoja na Joy Band wakiwa Location


Wakiwa Kikazi zaidi


Baadhi ya Waimbaji wa Joy Band


Unaweza Pata Picha

Habari Ndo Hiyo...

Apostle akiwa katika Shooting


SOURCE: Samsasali

Comments