DVD YA NINAMPENDA YESU YA KWAYA YA KIJITONYAMA DSM KUZINDULIWA RASMI IKIMBATANA NA TAMASHA LA UIMBAJI


Tukio hilo linatarajiwa kufanyika jumapili hii katika kanisa lao wakisindikizwa na waimbaji wengine akiwemo mwanamama Christina Shusho ambaye amekuwa akifanya mazoezi na kwaya hiyo wiki hii kwa uimbaji wa live, pia waimbaji wengine ni pamoja na malikia wa muziki wa injili nchini Rose Muhando, kwaya za usharika wa Kijitonyama, Ukombozi Msasani pamoja na waimbaji wengine.



Uzinduzi huo pamoja na tamasha halitakuwa na kiingilio. Kwaya hiyo inawaalika wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kufika bila kukosa katika tamasha hilo kwakuwa itakuwa wakati mzuri wa kumsifu Mungu pamoja na waimbaji waalikwa na wenyeji ambao wamejiandaa vyema kwaajili ya tukio hilo muhimu.

Kwaya ya vijana Kijitonyama inatamba na wimbo wake maarufu uitwao 'Naingojea siku ya ahadi' ambao umekuwa ukipendwa na watu wengi kila upigwapo kupitia WAPO Radio FM ya jijini Dar es Salaam, waweza kuusikiliza wimbo huo kwakubonyeza link iliyowekwa hapo juu.

USIKOSE JUMAPILI HII KIJITONYAMA HAKUNA KIINGILIO.



Source: Gospel Kitaa

Comments