Mzee Malinga (katikati), mkewe (kushoto) na Baba (SNP Dr. Godson), wakati familia hii ikishuhudia matendo makuu ya Mungu kwa mtoto wao Naomi. |
Familia hii wana mtoto anayeitwa Naomi, ambaye alifaulu vizuri form 4, na
tarehe 27 March 2014 ilikuwa birthday yake. Hata hivyo, Jioni ya hiyo siku ya tarehe 27 March mwanae alianza kuona watu ambao walikuwa wanamfuata sebuleni ingawa baba yake alikuwa hawaoni.
tarehe 27 March 2014 ilikuwa birthday yake. Hata hivyo, Jioni ya hiyo siku ya tarehe 27 March mwanae alianza kuona watu ambao walikuwa wanamfuata sebuleni ingawa baba yake alikuwa hawaoni.
Katika
wale watu aliokuwa anawaona miongoni mwao ni majirani za familia hii,
na ambao miongoni mwao watoto wao hawakuwa wamefaulu kama Naomi.
Usiku
ule Naomi (mwanae) alikuwa anakimbia kimbia ovyo, na kumgongea mlango
baba yake akisumbuliwa na wale wachawi. Maajabu Naomi alikuwa na macho
ya kuona watu ambao wasioonekana kwa baba yake waliokuwa wanamvizia.
Ndiposa Baba yake aliwaza pengine ni malaria imepanda kichwani kwa
mwanane.
Kuna wakati baadae
baba alitaka kumsaidia mwanae, lakini looh, Naomi akamwambia baba yake
kuwa amechelewa na huyo mtu aliyekuwa anamfuata akimvizia kutaka kumchinja na kisu na keshaondoka zake.
Mama mzazi wa Naomi alikuwa ameenda Moshi kipindi hiki cha kuanza kwa hili tatizo.
Baba yake Naomi alimpeleka kwa Mchungaji ambapo anaabudu, na
akafanyiwa maombi na kuazimia kumuacha kwenye hii nyumba ya mchungaji.
Hata hivyo mwanane kuanzia siku ile alikuwa halali kabisa usingizi
wowote.
Siku
moja Naomi alitoroka na alipopatikana alipelekwa hospitalini, ingawa
alikutwa hana tatizo kubwa la malaria, kwani hakuwa na vimelea vya
malaria vyenye kuhitaji matibabu.
Siku
iliyofuata alipatiwa tiba nyingine ya 'quinine' na kila mara akawa
anaongezewa dozi. Madakatari walikiri aina hii ya malaria haijawahi
kufahamika au kuwepo kwenye taaluma zao. Madaktari walipendekeza
pengine aanzishiwe dozi ya wenye vichaa.
Dozi
ilianza lakini pia wazazi na madkatari wakapendekeza kuwaona watumishi
wa Mungu. Muhimbili ikawa sehemu ya mwisho, na ambapo madaktari
walishauri kama wazazi wanataka kwenda kwa waganga wa kienyeji sawa, au
makanisani kuombewa sawa, wafanye hivyo.
Wazazi
walimpeleka Majumba Sita Dar es Salaam akaombewa na baada ya maombi, Naomi akawa ametulia na kulala. Walimuacha mwanae
mahali pale akiombewa, na huku ile hali inamrudia kila baada ya siku.
Muda wa
mwanae kwenda shuleni ukawadia, na wazazi wakaenda kumchukua kutoka
huko Dar es Salaam. Hata hivyo fujo ziliendelea kuwa kubwa zaidi, na
Naomi alikuwa akitaja majina ya watu wakubwa serikalini, na hata wasanii
kama akina Kanumba n.k. alipotajiwa kwenda shule, ndipo kabisa aligoma
katakata na kusema hana mpango wa kwenda shuleni tena.
Wapo
ndugu waliomshauri ampeleke Moshi kwa sababu kuna sehemu ya maombi
mazito. Mzee Malinga kwa kujali alifunga safari kwenda Moshi na Naomi.
Ilibidi amfunge miguu mwanae ili asimtoroke. Njiani alipata shida sana
kumepleka, kwani alikuwa anakataa kufuatana na baba yake na hata
kunyanyuka kwenye kiti cha basi na kuanza kucheza nyimbo za TV ya lile
basi mbele ya abiria wote.
Mbaya
zaidi, Naomi akiwa njiani alikuwa anasema baba yake anataka
kumtoa kafara, jambo ambalo lilifanya abiria waingilie kati na kujua
kulikoni? Walipofika Moshi, mzee huyu alikodi Guest House yenye double
beds ili kuhakkikisha kuwa mwanae hatatoroka, lakini mwanane akagoma
kulala akipiga makelele kwamba baba yake amefanya hivyo ili apate nafasi
ya kumbaka. Baba huyu alijisikia vibaya sana na aibu ikawa inampata.
Palepale Baba yake alipewa wazo la kutafuta hosteli ya masista pale
Moshi na
ambapo mwanane alikubali kulala pale hosteli.
ambapo mwanane alikubali kulala pale hosteli.
Kesho
yake alimpeleka mwanae kwa 'Yule Mtu wa Maombi'. Mzee Malinga anakiri
kuwa toka amekulia wokovu hakuwahi kukutana na aina hii ya maombi. Kwa
nini? Anasema ni aina ya maombi ambayo mwanae aliambiwa aizunguke
madhabahu, na kisha kunyweshwaa maji ambayo hakufahamu yana kitu gani. Hata hivyo maombi yale hayakumsaidia mwanae.
Alirudi Morogoro,
ikabidi wampeleke upya Naomi Hospitalini, na ambapo madkatari
walishauriana kumuanzishia huyu mtoto dozi ya kutuliza watu wenye
kichaa. Pale hospitalini hata hivyo, alikuwepo Dr. Loice wa Hospitali
ya Saba saba (Majeshi Majeshi) ambaye aliwashauri wazazi hawa wampeleke
Naomi Kanisani Ufufuo na Uzima Morogoro, kwani alibaini kuwa tatizo
kama hili tiba yake siyo ya Hospitalini tena. Hata hivyo,
wazazi walikuwa na taarifa hasi dhidi ya Kanisa hili. Walijishauri
sana juu ya wazo hilo, wakisema endapo makanisa yote waliyokwenda
shida ya Naomi haikutatuliwa, je, Kanisa la Ufufuo na Uzima watawezaje?
Hata hivyo walitii na kesho yake wakafika kanisani ambapo walipokelewa
vizuri na maombi kwa Naomi yakaanza rasmi. Kuanzia siku ile, Naomi
alianza kufunguliwa na kuanza kurudiwa na ufahamu wake. haikuchukua muda
mrefu, wazazi wakiwa wanamleta Naomi kwenye Mkesha na Ibada za katikati
ya wiki, Naomi akawa mzima kabisa.
Baba na Mamawa Naomi Malinga wakitoa sadaka ya Shukrani na Dictionary ya Biblia kumshukuru Mungu aliyemponya Naomi kutoka kwenye Maradhi / Ukichaa wa kutengenezwa 07/09/2014. |
Comments