KILA MTU ANA USHUHUDA.

Mungu akikupa nafasi ya kuiona siku mpya, na kuwa hai katika siku hiyo, huo ni ushahidi tosha kuwa;

 1. Mungu ana kazi na maisha yako bado na kama ana kazi na wewe, uwe na uhakika Mungu atayagharamia maisha yako katika maeneo yote… Lakini itatokea pale tu utakapojua kitu gani au jambo gani Mungu anataka ufanye kwa niaba yake na kuanza kulitenda

 2. Mungu amekupa nafasi ya kuyagusa maisha ya weng
ine na kuyapa thamani 
3. Mungu amekupa nafasi ya kuweka rekodi na alama ya maisha yako hapa duniani… Rekodi au alama hiyo inaweza kuwa ya mema au mabaya, uchaguzi ni wako, hata Mungu hawezi kuingilia 
4.Mungu ameiondoa jana, amekupa leo, Mungu anataka ujue kuwa haiangalii jana yako kukutengenezea kesho yako njema. Hivyo jizoeze kuyasahau mabaya yaliyopita, unaweza kuwa bora leo na kuandika historia mpya, unamkumbuka Rahabu yule kahaba? Unamkumbuka Ruthu mkwe wa Naomi? Unamkumbuka Yabezi? Wote hawa walikuwa na JANA/ HISTORIA MBAYA lakini walipoelewa thamani ya LEO YAO kila kitu kikabadilika 
5. Mungu anapokupa fursa ya kuwa hai anataka ujue kuwa amekupa MTAJI WA KUPATATA YOTE UYATAKAYO hapa duniani. Anataka ujue kuwa bila MAISHA/ UHAI yote uyatakayo hautayapata… Anataka ujue kuwa ni BORA MARA MIA kuwa MBWA ALIYE HAI kuliko kuwa SIMBA ALIYEKUFA! 
6. Mungu anapokupa fursa ya kuwa hai, anataka uutumie muda huo kujiandaa kwa ajili ya MAISHA YA MILELE, MAISHA BAADA YA KIFO… Ndio maana Mungu anakupa nafasi kunisikia nikizisema habari za Yesu, Msamaha wa dhambi, Uzima wa milele, Hukumu, Mbinguni na Jehanamu nk. 
Lakini UAMUZI NI WAKO… Ila uamuzi huo utakupa furaha au kilio milele.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.


                     MUNGU akubariki sana .

Comments