MWIMBAJI NYOTA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA AFARIKI.

Marehemu George Njabili enzi za uhai wake , hapa akiwa na mkewe
Tasnia ya muziki wa injili leo imempoteza mwimbaji wake nyota na mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti Mtoni almaarufu kama Lulu choir kutoka kanisa la Kilutheri, George Bonge Njabili aliyefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema, marehemu George alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam wakati akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda mrefu na mwimbaji huyo kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.

George Bonge enzi za uhai wake.

Marehemu George atakumbukwa kwa huduma yake njema ya uimbaji kupitia kwaya ya Lulu ambako aliongoza nyimbo mbalimbali ukiwemo Around the corner Jesus coming, Tazameni Upendo huu, Haleluya na nyingine nyingi huku akiipamba vyema DVD ya kwanza ya kwaya hiyo iliyobebwa na wimbo wa Lulu. Ni takribani miaka mitatu sasa toka aliyekuwa mwalimu mkuu wa kwaya ya Lulu kufariki dunia, kifo ambacho wengi walidhani aliyefariki ni George kiasi kwamba taarifa za kifo chake hii leo kimepokelewa kwa tofauti hasa baadhi ya watu wakidhani alishafariki siku nyingi.
Taarifa ya rais wa shirikisho la waimbaji wa nyimbo za injili ni hii hapa.
 Tanzia Tanzia na huzuni kubwa! Ni kwamba mwimbaji nguli wa kwaya ya Lulu mtoni GEORGE BONGE amefariki dunia mchana huu Muhimbili. Kabla ya Hapo alianguka leo asubuhi nyumbani kwake Tabata alipokua akijiandaa kwenda kazini, hakuchukua hata dakika nyingi akafariki, buriani rafiki yetu, buriani mpendwa wetu George, Nitakupeni taarifa zaidi!
  
Tazama wimbo wa Around the corner alioimbisha George Bonge. na kwenye Wimbo wa Maarufu wa LULU George Njibili anapiga gitaa.
BWANA alitoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe milele.

Comments