USHUHUDA WA NDOTO.


Nikiwa na Scholar wangu

BWANA YESU asifiwe.
Karibu upate ufahamu kuhusu ndoto na maana zake.
Mwaka 2012 Mwishoni Niliota Ndoto, Siku Hiyo Nilikuwa Nimefunga Siku 4, Na Katika Maombi Hayo Nilikuwa Naombea Mambo Mengi Likiwemo Kupata Mke Mwema, Kuna Dada 1 Ambaye 2006 Kule Nyumbani Mwanza Tuliishi Mtaa 1 Na Wakati Huu Mimi Nilikuwa Dar, Niliulizia Mwenendo Wake Kiroho Nikaambiwa Anaendelea Vizuri Sana, Nilimtuma Rafiki Yangu Ambaye Wanasali Wote Ili Amfatilie Na Kunihakikishia Kama Yule Dada Kasimama Kiroho, Nilipewa Majibu Mazuri Na Kuhakikishiwa Kwamba Yule Dada Yuko Vizuri Kwa MUNGU, Nilisema Huyo Atafaa Kuwa Mke Wangu. Siku Ya 3 Ya Maombi Niliota Ndoto, Nilikua Natembea Kwenye Barabara Nzuri Ya Lami Huku Pembeni Kukiwa Na Malaika, Pia Kwa Mbali Sana Nilimuona Yule Dada Akitembea Barabarani Pia Na Pembeni Mwake Kukiwa Na Malaika, Nilitembea Mwendo Kidogo Nikimfuata Yule Dada, Malaika Aliyekuwa Pembeni Yangu Akaniambia "Huyo Dada Hatakuwa Mkeo, Mkeo Yupo Na Yeye Mmewe Yupo". Nikaamka, Na Ni Kweli Miezi Michache Baadae Yule Dada Alifunga Ndoa Na Mimi Pia Mwaka Huu tarehe 20 Sept 2014 Nimefunga Ndoa. Ndugu yangu lengo la kukushuhudia ndoto hii ni kwamba Usidharau Ndoto unayoota. 
-Mawazo kama haya Yanawaumiza Vijana Wengi wa kiume Wamwonapo Tu Mwanamke Ana mwenendo Mzuri Anafaa Kuolewa Basi Kosa Kwao Atataka Akamwambie Eti asipomwambia Atawai Mtu Mwingine Pasipo Kujali Ndie Ambae Mungu Amempa Au Tama Zamwili Wake.
- Mimi Peter, Binafsi Nilikuwa Sijaomba Juu Ya Huyu dada, Ila Huyo Nilikwenda Kibinadamu Na Kuona Ana Sifa Zote Za Kufunga Nae Ndoa Ila MUNGU Akaonyesha Kwamba Mawazo Yangu Yalikuwa Batili, Nimeandika Ili Tujifunze Maana Sio Kila Kizuri Kinafaa, Na Sio Kila Kinachofaa Ni Sahihi, Pia Tusiangalie Kwa Macho Ya Kibinadamu Maana Hudanganya Sana Bali Tumuombe BABA Wa Mbinguni.
- watu tulio wengi hatuombi katika hilo yaani yupi mke au mume Mwema kutoka kwa MUNGU, tunatumia akili zetu na tamaa za mwili(muonekano wa nje au MVUTO) ndio mana ndoa nyingi zinayumba.Na tutambue wakaka au wadada walio wengi Makanisani hawapo kiroho wapo kimwili wamefata kuoa na kuolewa na sio kumtafuta MUNGU.Tujifuze kwa hili.
- Akili Ya Kibinadamu Inadanganya.
- Mke/Mume  mwema hutoka kwa BWANA, bali mke bora hutoka ATM.
Jambo kubwa ambalo nataka tujifunze ni ndoto. Ningedharau ndoto hiyo ningeng'ang'a kumchumbia yule dada, ningepoteza muda maana nisingemuoa. Wengi wanakuwa wameshajibiwa maombi yao na kuona kabisa kwenye ndoto lakini kwa sababu ya kudharau ndoto hudhani kwamba hawajajibiwa kumbe tayari.


 Kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani.

MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Siku ya ndoa yangu tarehe 20 September 2014


Comments