AKILI ZA ROHONI.


“Yafahamu sana hayo niyasemayo, kwa maana BWANA atakupa AKILI katika mambo yote” 2TIMOTHEO 2:7.
BWANA YESU asifiwe sana,

Watu wa Mungu, atukuzwe Mungu wetu kwa kutupa kibari cha kuiona siku ya leo ili tujifuze na tujitajirishe kwake.
Inajulikana kuwa watu wote walio na matatizo ya akili (akili za kimwili) huwa wanafanya mambo mengi katika hali ya ukosefu/kimakosa.

Baadhi yao huwa wanafanya mambo yasiyostahili hata wakawa ni vituko mitaani, Popote wanapopita watu huwashangaa au kuwakimbia.

Hii yote ni kutokana na matatizo ya akili.
Katika mambo ya rohoni pia wale wasio na AKILI ZA ROHONI nao huboronga kila siku hata watu wakawashangaa.
Biblia inasema kuwa Bwana atatupa akili katika mambo yote, lakini cha ajabu siku hizi kuna watu wasio na akili kabisa makanisani,
Na Godfrey Miyonjo
Watu wanaokataa kuongozwa na Roho wa Mungu wakifuata ubatili wa nia zao,
Watu waenendao kama watu wa mataifa (wapagani) tu,

Watu walioelemewa na uovu wa kila namna, watu walevi, watukanaji, wenye mizaha, watembea uchi, wazinzi, waasherati, wenye husuda, n.k,

Nimewahi kukutana na watu wengi tu wajiitao wakristo wakiitetea dhambi,
Mabinti wakitetea uvaaji wa mavazi yasiyompa Mungu utukufu (vijisuruali, vimini, vichupi. N.k) hadharani wakisema kuwa mavazi hayamfikishi mtu mbinguni,
Wengine hutetea ulevi wakisema kunywa pombe kidogo Biblia inaruhusu,

Pia wapo wele waendao kuuliza mambo yao kwa wafumu na wachawi wakidai kuwa Mungu amesema “jisaidie nami nitakusaidia”
Huku ni kukosa AKILI ZA ROHONI.

Ili kila mmoja wetu awe na AKILI ZA ROHONI sharti akubali kuongozwa na Roho wa Mungu,
Kwa maana hakuna kitu kingine kiwezacho kumfanya mtu awe na AKILI ZA ROHONI zaidi ya ROHO MTAKATIFU.

Biblia inasema kuwa Mtu aliye na ROHO MTAKATIFU ana AKILI ZA ROHONI kuliko watu wengine wote.

MWANZO 41:38-39 “Farao akawaambia watumishi wake, Tupate wapi mtu kama huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake?. Farao akamwambia Yusufu, Kwakuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, HAPANA MWENYE AKILI na ufahamu kama wewe”.
Mtu aliye na AKILI ZA ROHONI Haenendi kama mataifa waenendavyo,

EFESO 4:17-18 “Basi nasema neon hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao, ambao AKILI ZAO ZIMETIWA giza, nao wamefarakanishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao”.

Huu ndiyo wakati ufaao kwa kila mmoja wetu kutubu na kuamua kuishi maisha matakatifu kwa msaada wa Roro Mtakatifu.
KILA MMOJA ALIYE NA UHITAJI WA AKILI ZA ROHONI, AMWOMBE ROHO MTAKATIFU SAS NAYE ATAMJAZA SASA.

Comments