KILA MTU ATALIPWA SAWASAWA NA MATENDO YAKE.

BWANA YESU atukuzwe ndugu wote.
Karibu tujifunze ujumbe wa kututoa pabaya na kutupeleka pazuri.
''Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.{Yakobo 2:26}'' 
 Imani inayozungumzwa hapa ni imani ya pekee ya uzima ambayo ni imani ya kumpokea YESU KRISTO kama BWANA na MWOKOZI wa maisha ya kila Mwanadamu(Warumi 10:9-13, Matendo 4:12, Yohana 14:6, Warumi 10:17)
-Imani ya kweli huja kwa neno la KRISTO .
-Imani ya kweli ni ya kumpokea BWANA YESU na kuliishi neno la MUNGU.
-Imani ya kweli ni ya kuokoka ukiwa duniani maana hakuna sala ya toba kwa marehemu.
-Imani ya kweli ni ya wanaoongozwa na ROHO MTAKATIFU.
 YESU anasema ''Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;-Mathao 7:24''
Sasa imani huambatana na matendo na imani sahihi katika KRISTO YESU huambatano na matendo ya utakatifu.
Matendo ni kile tukifanyacho kila siku iwe kwa kusema, kutenda na hata kuwaza.
Kuna watu licha ya kuwa kwenye Wokovu lakini matendo yako hayafanani na wateule wa BWANA Ndiposa tunasema SAWA NA MATENDO YAKE KILA MTU ATALIPA.
Ukiamua kumshika YESU lazima ushike na utakatifu wake.
''wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa MUNGU kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa MUNGU kuwa silaha za haki.Warumi 6:13''
Ukiwa kwa MUNGU unakuwa hauko kwa shetani. Ukiwa nje ya MUNGU, moja kwa moja unakuwa uko kwa shetani. Hakuna sehemu ya kati! Matendo yako yatakutambulisha kwamba wewe ni wa MUNGU au wa shetani hata kama unajumuika na wengine kansani. ''Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi. -Warumi 14:23b'' 
Kila tendo lisilotoka katika imani ya KRISTO ni dhambi.
Wengine wamemkataa BWANA YESU lakini na wao watalipwa sawa sawa na matendo yao, wengine wako kwenye dini za shetani na hawamhitaji YESU KRISTO na hata wao watalipwa sawa sawa na uovu wao. Hakuna uzima nje na BWANA YESU.
“Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU.” 2 Wakorintho 4:3
 mungu wa dunia hii[shetani] amepofusha fikra zao ili isiwazukie nuru ya BWANA YESU ambayo ni nuru ya uzima wa milele.

 "Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu". ndugu  zangu naomba  tupambane na matendo ya mwili yaliyo dhambi ili tumpendeze MUNGU.''Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.-Wagalatia 5:19-21''
 Sawa na matendo yake kila mmoja duniania atalipwa siku ya Mwisho uzinzi, uasherati, ufisadi;
kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano;husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalme wa MUNGU. Hawa kama hawatatubu basi watalipwa jehanamu ya moto.


 Sio Lazima Kumpokea YESU Lakini Haiwezekani Kuingia Uzima Wa Milele Bila Yeye. Soma Yohana 14:6, Warumi 10:9-13, Matendo 4:12 Na Yohana 8:36. 

 Kila Mwanadamu Anamhitaji YESU Kwa Ajili Ya Uzima Wa Milele, Kama Humhitaji Leo Basi Utamhitaji Siku Ukielekea Jehanamu Ila Utakua Umechelewa. Neno La MUNGU Halipitagi Aure Bali Linapita Ili Likupe Ufahamu, Ujitambue Na Ili Uamue Kuupokea Uzima. ''Amwaminiye Mwana(YESU) yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU inamkalia.-Yohana 3:36''

 Ana Heri Mtu 1 Anayeokoka Na Kuacha Dhambi Kuliko Watu 99 Ambao Hawana Haja Ya Kutubu.

  Na kwa wale waliokwisha kumpokea BWANA YESU ''mtawatambua kwa matunda yao. Mathayo 12:33''
BWANA YESU anatupenda sana , Yeye  YESU ni MWALIMU tena ni DREVA na analiongoza gari lake{KANISA} lifike salama mbinguni kwa BABA

 ''Yohana  8:12 {Basi YESU akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe bali atakuwa na nuru ya uzima} Ndugu natamani uliweke neno hili ndani kabisa moyoni mwako ili usijemwacha YESU maishani mwako kwani hakuna uzima kwingine.

 IKIWA INJILI YA YESU KRISTO IMESITIRIKA BASI IMESITIRIKA KWA HAO WANAOPOTEA.

Wala hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ila ni jina la YESU pekee {Matendo  4:12}

 YESU KRISTO ni BWANA wa mabwana na MFALME wa wafalme. ndugu ulie kwake uko mahali sahihi kuliko sehemu yeyote ila dumisha tu utakatifu ili siku ile ulipwe uzima wa milele.
Kuna watu watalipwa uzima wa milele na kuna watu watalipwa jehanamu ya moto. Kila unayemuona duniani akifa anakwenda ama Paradiso ama kuzimu, Paradiso ni furaha na kuzimu ni mateso makuu. Kuzimu ni mateso lakini jehanamu  ni mateso zaidi.

 Hata kuwa na dini tu haitoshi kuhesabiwa kupata uzima wa milele.
Dini ni njia ya kumwelekea MUNGU{Ayubu 4:6} YESU KRISTO ni NJIA na UKWELI na UZIMA na mtu haendi mbinguni ila kwa njia ya yeye{yohana 14:6} 
 YESU ndie dini ya kweli na ya uzima wa milele. karibu kwa YESU ndugu na ubarikiwe sana.
YESU anasema 
''kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari kwa kuwa katika saa msiyodhani MWANA WA ADAMU yuaja {Mathayo 24:44}'' 
-Tunajiweka tayari kwa kutenda matendo mema huku tukiwa tumeokoka.
-Tunajiweka tayari kwa kulitii neno la MUNGU.
-Tunajiweka tayari kwa kujifunza neno la MUNGU na maombi.
-Tunajiweka tayari kwa kumtii BWANA YESU.

''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; Bali karama ya MUNGU ni uzima wa millele katika KRISTO YESU BWANA wetu. [Warumi 6:23]''

 ''shetani Ni shetani Tu. Hakuna shetani mtakatifu Wala shetani Mbaya. Ndugu zangu jiepusheni na shetani.

Mwivi(shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; YESU KRISTO alikuja ili tuwe na uzima sasa kisha uzima wa milele {Yohana 10:10}
Ndugu yangu tambua ya kuwa kuna YESU KRISTO na kuna shetani hivyo tunapomtaja YESU KRISTO tambua ya kuwa tunamtaja yeye wa kutupeleka uzima wa milele na anapotajwa shetani basi jua ya kuwa hata wafuasi wake wote wako kwenye njia  nyingine tofauti na YESU KRISTO na huyu shetani ana matawi ndizo hizo dini zote ambazo zinampinga YESU KRISTO.
Sina haja ya kutaja dini fulani maana zote ni za shetani hata kama wanaonekana ni dini safi lakini MUNGU ametaka wote wanaoutaka uzima wa milele basi wampe YESU maisha yao na pia kumbuka YESU KRISTO hakuja kuanzisha dini ila tunaitwa Wateule wa MUNGU  kwa sababu tunamfuata KRISTO lakini hii ni kwa roho maana wengine wakristo majina tu lakini huyo KRISTO hayumo mioyoni mwao.

Pi tambua ya kuwa shetani ana matawi mengi sana lakini wanadamu bila kujua wanadhani sio shetani lakini huyo ni shetani mfano wafuga majini je wanasali kwa MUNGU yupi? ambaye anawaruhusu kutumia majini kuroga wengine? au je kitabu kitakatifu kitumike kwa uganga wa kienyeji je huyo ni MUNGU yupi? hivyo hizo dini maarufu za kishetani unazozifahamu wewe ni matawi madogomadogo tu kwenye utawala wa shetani.
Mimi nakujulisha tu ili siku ya mwisho usiseme kwamba sikujua kama hakuna uzima wa milele nje na BWANA YESU.
Siku ya mwisho kila mtu atasema YESU ni BWANA.
Kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri.''Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. -2 Kor 5:17''

-Ndugu yangu hakikisha unakuwa ndani ya KRISTO.
-Hakikisha matendo yako yamekuwa mapya yaani yamekuwa ya utakatifu. 
Uamuzi wako wa leo wa kumpokea BWANA YESU una manufaa makubwa katika kesho yako. Mchague YESU maana ukimchagua YESU KRISTO umechagua uzima baada ya hapo dumisha utakatifu maana SAWA NA MATENDO YAKE KILA MWANADAMU ATALIPWA SIKU YA MWISHO.

Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments