KWA NINI WANAWAKE WENGI/ WATU WENGI WANAVAMIWA NA Mapepo?

Na Mtume na Nabii Josephat Mwingira, Efatha Ministry.


Joshua 7: 10 “BWANA akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?” MUNGU Alisema, mji wa Yeriko utakuwa sadaka kwangu, na Aliwaambia Msichukue chochote toka ndani yake bali Fedha yote, Dhahabu, Vyombo vya Shaba na Chuma vitaletwa katika Hazina ya BWANA, Joshua 6: 1 – 24. Lakini Akani mwana Karmi, alishikwa na tamaa, akachukua baadhi ya vitu wakati BWANA alisema Mtu yeyote Asichukue kitu (Hakutii Agizo la BWANA).

Wanawake wengi wanavamiwa na mapepo kwa sababu ya TAMAA YA VITU Vinavyowapitia, mfano kama Hereni, Mapambo mbalimbali, Wigi (Manywele ya watu waliokufa, manywele bandia) na n.k.

SIYO VITU VYOTE Unavyoviona Wewe Vinakufaa, Acha vitu vingine Mwana wa MUNGU, siyo Vyote vinavyokufaa, na hii ndiyo Sababu KUBWA inayowafanya Wanawake wengi wapate MATESO.

Akani alipoleta vile vitu alivyovichukua, alisababisha Hatari kwa Wana wa Israeli, Wana Israeli walipokuwa wakienda vitani walikuwa wanapigwa katika Vita, Maadui zao waliwakimbiza. Ndipo Yoshua Akamwendea BWANA, Akamalilia BWANA na kumuuliza Yanatokeaje haya? Mbona tunapigwa?, mbona Maadui zetu wanatukimbiza? Ndipo BWANA akamwambia Yoshua, kuna mtu Ameleta NAJISI kati yenu. Ndipo Yoshua alipowaita Wana wa Israel wote na Akani akapatikana na akapigwa mpaka kufa pamoja na familia yake na vitu vyote alivyokuwa navyo kuchomwa moto (Soma Yoshua 7: 7 – 26 ili uelewe zaidi).

Inawezekana kuna kitu ambacho si kisafi kati yako, kitu najisi kati yako, kinaweza kikawa kimeletwa na Wewe Mwenyewe, au Mke wako, au Mume wako, au Watoto wako, au Wazazi wako, au Marafiki zako, au Wafanyakazi wako na n.k. Ni vema ukafuatilia na kujua ni nini hiko.




Mwanamke  aliyekuwa anasumbuliwa na mapepo akiombewa Efatha Mwenge.
 

Comments