ANGAMIZA ROHO ZA NYOKA MAISHANI MWAKO.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu ujifunze na kupata ufahamu juu ya nyoka.

shetani huonekana sana kama nyoka kwenye ndoto ili kuwatesa wanadamu.
shetani alitumia nyoka kumdanganya Eva Soma bila kuacha Mwanzo 3:1-24.
Uongo huo wa shetani ndio ulioleta kifo duniani, mateso duniani na kila aina ya matatizo duniani, nyoka ni hatari na anatakiwa apondwe kwa jina la YESU KRISTO hata leo.


Nyoka kwenye ndoto huwakilisha
-roho ya uongo.
-huwakilisha pia shetani mwenyewe.
-Huwakilisha mizimu.
-Huwakilisha uchawi
-Huwakilisha uganga wa kienyeji.
-Huwakilisha unajimu pia na machukizo mengine mengi.


Unaweza ukaota nyoka anakukimbiza kumbe maana yake ni kwamba wachawi wanataka kukuangamiza na maana nyingine ni kwamba uko kwenye eneo ambalo shetani ametawala sana hivyo uwe makini.

Unaweza ukaota nyoka anazunguka sehemu kumbe maana yake kuna uongo mkubwa utanenewa wewe ambao uongo huo unaweza ukaleta madhara makubwa maishani mwako.
Kumezwa na nyoka ndio kabisa kumwezwa au kuzidiwa na nguvu za giza.

Nimesema hapo juu kwamba shetani hutumia sana wanyama kwenye ndoto ili kuhakikisha mwanadamu hafanikiwi au hapati baraka zake na pia huhakikisha mwanadamu haendi uzima wa milele.

shetani au majini yanaweza kuonekana pia kama wanyama wengine mfano mbuzi, mbwa, mamba, fisi na wengine wengi.

Usione raha tu kuwasimulia wenzako kwamba '' nimeota mbwa ananifuatilia'' Kumbe uzinzi unakufuatilia.


Usidharau ndoto ila omba ukiharibu mipango ya shetani maishani mwako. BWANA YESU siku zote yuko tayari kukushindia kama tu ukimpokea na kumuomba MUNGU kwa yeye.

Biblia inamwita shetani kama baba wa uongo wote duniani pia shetani ni joka na wasaidizi wake ni vijoka vidogo vidogo.
Bahari kwenye ulimwengu wa roho huwakilisha ''mahali wakaapo watu'' au ni duniani, ndio maana kuna sehemu za nabii kwenye Biblia zinasema ''Kisha nikaona mnyama akitokea baharini'', bahari hapo humaanisha dunia na mnyama huyo ni roho ya shetani.Lakini ushindi una BWANA MUNGU siku zote 


Biblia inasema kwamba shetani kama nyoka na wasaidizi wake wataangamizwa na MUNGU aliye hai. Isaya 27:1 inasema Biblia '' Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. ''
 
-Kuna nyoka yupo baharini yaani Dunia hata sasa na huyo mwangamize kwa jina la YESU KRISTO.

-Kuna viongozi wana roho kabisa ya nyoka na nyoka hao wanatakiwa waondolewe katika mioyo yao, vongozi hao haijarishi ni wa serikali au vinginevyo lakini kama shetani amewavamia lazima uongo utawale katika eneo hilo.

Ufunuo 20:1-3 Biblia inasema '' Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.''
 
Kupitia maandiko hayo unaweza kujifunza kwamba.


-roho ya uongo ni ya shetani hivyo popote ulipo uongo ujue shetani ndie anapamiliko hapo, ndugu yanko akiwa anaongea uongo ujue kabisa kwamba roho ya shetani imemwingia.
-shetani sasa amefungwa kuzimu kwa sasa hivyo wasaidizi wake tu ndio wanatesa dunia kwa sasa ila ipo siku ataachiwa kwa muda kisha kuangamizwa milele, ataachiwa kipindi ambacho kanisa litakuwa limeondolewa duniani.
-shetani hana nguvu ndio maana kwa agizo la MUNGU, malaika mmoja atamshika na kumfunga minyororo.

mwisho wa joka na mawakala wake wote ni huu hapa ''Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.-Ufunuo 20:10''
Baada ya kuona kazi za nyoka na mwisho wake sasa nataka tuone msaada pekee ambao utakuweka huru mbali na nyoka na majoka, mbali na uchawi na laana , mbali na uonevu wa kuzimu. Kwa upendo mwingi sana MUNGU anatupenda wanadamu na ameweka ushindi wote ndani ya BWANA YESU KRISTO, Biblia inasema '' Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. -Yohana 8:36"
-YESU akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli mbalia na kuonewa na roho za nyoka.
-Uhuru wetu wanadamu uko katika YESU KRISTO pekee.
Tunaupata uhuru huu kwa kumpokea kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu kisha tunaanza kujifunza neno la MUNGU ambalo litatuimalisha, kumbuka shetani anaogopa neno la MUNGU na KRISTO ni Neno juu ya neno la MUNGU. Huu ndio uhuru kamili.

Wengine hukimbilia kwa waganga wa kienyeji, ndugu zangu waganga hawa ni vijoka ndani ya joka, usikimbilie huko bali mkimbilie YESU KRISTO anayeokoa. YESU atakuokoa na jehanamu na pia atakuokoa na mateso ya shetani.
YESU yeye anasema '' Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. -Mathayo 11:28 ''
Ndugu zangu tumkimbile BWANA YESU mwenye uzima wetu.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments