INJILI YA YESU KRISTO INAMHITAJI KILA MWANADAMU.

BWANA YESU asifiwe ndugu.
Karibu tujifunze habari njema za ufalme wa MUNGU.
Injili maana yake ni habari njema za ufalme wa MUNGU.
Kama kuna kitu cha muhimu cha kuhubiri kwa wahubiri basi injili ni jambo la kwanza.
Injili ndiyo inayohubiri wokovu.
Injili ndiyo inayohubiriwa na watu wanapata ondoleo la dhambi kama wakimpokea BWANA YESU.
Injili ya BWANA YESU inamuhitaji kila mwanadamu, wanaoipokea injili na kutubu na kuanza kuishi maisha sahihi ya wokovu hao wataurithi uzima wa milele.BWANA YESU anatutaka wanadamu wote tutubu na kuiamni injili, Neno la MUNGU ni injili na shabaha ya Neno la MUNGU ni ili wanadamu wafike uzima wa milele, YESU anakutaka wewe ndugu uiamini injili, Marko 1:14-15 ''     .........  YESU akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini INJILI. ''
Injili Ni Neno La MUNGU, Sehemu Nyingine Biblia Imesema Kwamba Injili Ni Neno La Msalaba. Wokovu Wetu Unatokana Na Injili, Msingi Wa Wokovu Wetu Umesimama Juu Ya Yale Yaliyotendeka Msalabani, Juu Ya Ukweli Na Juu Ya Kazi Ya MUNGU. 1 Kor 15:3 '' Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; ''
-Kama KRISTO asingelikufa msalabani basi injili isingehubiriwa, lakini sasa BWANA wetu YESU KRISTO yuu hai, ameshinda kifo na mauti na sasa yeye ndio sababu ya watu kuupata uzima wa milele, Hakuna Mwokozi mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO.


Injili Ni Ujumbe Wa MUNGU, Wala Sio Maoni Ya Wakristo Tena Sio Mawazo Ya Wafuasi Wa Kanisa Lolote. Ndugu Hubiri Injili Ya KRISTO Siku Zote Za Maisha Yako.

Katika Biblia Kila Jambo Lazima Lithibitishwe Kwa Mashahidi Wawili Au Watatu. Hata Wokovu Wetu Unathibitishwa Na Mashahidi Wawili NENO LA MUNGU Na ROHO MTAKATIFU. 

           1:    NENO Linasema Hakuna Hukumu Juu Ya Waliookoka(Warumi 8:1,  Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU.
 YESU Ndio Sababu Ya Wokovu Wetu Sisi Tunaomtii(Waebrania 5:9, naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; ),  

         2.    ROHO MTAKATIFU Anashuhudia Kwamba Sisi Tu Watoto Wa MUNGU(Warumi 8:16-17, ROHO mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa MUNGU; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa MUNGU, warithio pamoja na KRISTO; .........
-ROHO MTAKATIFU anashuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi tu watoto wa MUNGU.
-Wasiookoka na watenda dhambi  hata ROHO MTAKATIFU hayumo ndani yao hivyo hawezi kushuhudia kwao.
-Na Ndio Maana Yeye ROHO Anakaa Ndani Yetu(Warumi 8:9, Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake. )
-Kama huna ROHO MTAKATIFU huwezi kuzishinda dhambi.
-Kama una ROHO MTAKATIFU na ukashindwa kumtii pia huwezi kushinda dhambi.
-Kama huna ROHO MTAKTIFU huwezi wewe sio wa KRISTO.
-Lakini pia kuna tofauti kati ya kujazwa ROHO na kufurika ROHO. Kuna kunena kwa lugha na pia wakati mwingine kunena kwa Lugha ni karama kama Biblia inavyosema.
-Kuna wenye kiwango kidogo cha udhihilisho wa ROHO MTAKATIFU na kuna wenye kiwango kikubwa.
-Kuna watu ROHO huongea nao kwa sauti kabisa, kuna watu hata akama anaambiwa jambo lolote iwe ni kwenye simu au kwa njia ya kawaida ROHO anamwambia ''hilo unaloambiwa ni la uongo''
-ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana kwa kila mwenda mbinguni.
-Tamani kufikia kiwango cha juu cha udhihilisho wa ROHO MTAKATIFU.
-ROHO MTAKATIFU ni mtakatifu hivyo hakikisha unaokoka na kuwa mtakatifu.

 Injili ya BWANA YESU inaambatana na uponyaji wa roho na mwili.
Ndugu, Usipoteze Uhakika Wa Wokovu Kwa Kukaa Kwenye Mafundisho Ya Kanisa Linakataa Neno La MUNGU Na Nguvu Ya MUNGU Huku Kanisa Hilo KRISTO Kwao Akiwa Ni Ziada Tu. Sali Kanisa Ambapo Utapata Injili Kamili, Injili Ambayo Haijawekewa Chumvi Ya Udhehebu.

Watu Wengi Huishi Kama Wateule Wa MUNGU Lakini Hawajaokoka. Ndugu Anayeishi Hivyo Huyo Amepungukiwa Na Utukufu Wa Ukombozi Utokao Mbinguni. Maisha Ya Bila Kuokoka Ni Ya Kujisukuma Kwa Nguvu Zao Wenyewe. Mteule Ni Yule Aliyepokea Asili Ya MUNGU Kwa Kuzaliwa Mara Ya Pili Kutoka Juu. BABA Yao Wa Kiroho Yuko Mbinguni.
Hakuna anayetakiwa kuigeuza injili ya BWANA YESU, Kama yupo na alaaniwe ndivyo Biblia inavyosema, Wagalatia 1:7-9 '' Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya KRISTO. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. ''
-Mtu akileta injili tofauti na Wokovu kupitia YESU KRISTO, huyo haijui injili sahihi.
-Mtu akileta mafundisho yanayomkataa ROHO MTAKATIFU, huyo ni wakala wa shetani.
-Mtu akileta mafundisho ya kwamba kuna njia nyingine ya uzima wa milele nje na KRISTO, huyo ni baba wa uongo na ni shetani kabisa.
-Mtu akileta mafundisho yeyote yanayokataa kuokoka, huyo hajitambui na hamjui MUNGU aliye hai.
-Mtu akihubiri kuabudu sanamu na kuabudu watu wakiwemo watakatifu, huyo, huyo hayuko upande wa MUNGU.
=Anayeabudiwa ni MUNGU BABA(Ufunuo 19:10, 1 Nyakati 16:29) , 
=MUNGU MWANA(Mathayo 14:33, Mathayo 28:9; Luka 24:52; Yohana 9:38 ) 
=na MUNGU ROHO MTAKATIFU (Ayubu 33:4,Yohana 4:24) , ukimwabudu mariamu, Musa au Eliya wewe uko upande wa sheatni hata kama una jina la Kikristo.

 Ukitaka Kuwa Mkristo Mwenye Afya Njema Hakikisha Kwanza Unakula Chakula Kizuri Ambacho Ni Neno La MUNGU. Pili Hakikisha Unakunywa Maji Mengi Ambayo Ni Ujazo Wa ROHO MTAKATIFU. Tatu Hakikisha Unafanya Mazoezi Ambayo Ni Kumtumikia MUNGU Na Kutenda Kazi Yake. Nne Pata Hewa Safi Ambayo Ni Kwenda Kwenye Ibada Kanisani Kila Iitwapo Leo. Na Mwisho Jiburudishe Kwa Kuwa Na Ushirika Na Wateule Wengine Mkishauriana Na Kuombeana.

 Mafundisho Yeyote Ya Dini Ambayo Yanakuacha Mashakani Juu Ya Wokovu Wa Roho Yako, Hayo Hayaambatani Kabisa Na Injili Ya KRISTO. BWANA YESU Anasema Ukimpokea Yeye Kwa Imani Maana Yake Umepita Kutoka Mautini Na Kuingia Uzimani (Yohana 5:24, Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani) . Wokovu Ni Muhimu Sana Kwa Kila Mwanadamu. YESU KRISTO Anaokoa, Ukiamini Leo Unaokoka.

 Neno La MUNGU Humnyamazisha Mshitaki Wetu ibilisi. Ukitaka Kumnyamazisha shetani Tumia Neno La MUNGU Kwenye Maombi Yako Na Maisha Yako Kwa Ujumla, Kiri Neno La MUNGU Na Hakikisha Unaishi Kama Neno Litakavyo. BWANA YESU Anakupenda Sana.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments