KUPATA KWA KUCHELEWA


RP Adriano Makazi. ufufuo na uzima Morogoro
Utangulizi:  Somo letu linaitwa Kupata kwa Kuchelewa”. Bwana anataka upate vile unavyomuomba.  Mungu ni Mungu  wa kutimiza ahadi zake kwetu.  Hata hivyo, ingawa tunataka tupate kwa wakati wa maombi yetu, kitu ulichokiomba kinachelewa kupatikana. WAGALITA 4:4…[Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,]… Mungu hufanya kazi kwa wakati wa utimilifu. Upo uwezekano wa kuahidiwa jambo na Mungu na ukalipata kwa kuchelewa au usilipate kabisa, kutokana na kuwepo kwa watu waovu ambao wanalizuia. Leo ni siku ya  kupita katikati ya watu hao kwa Jina la Yesu. Leo tutapita katikati ya madeni, katikati ya magonjwa na katikati ya umaskini kwa kuwa tumejengwa juu  ya mwamba ambaye ni Yesu Kristo, na malango  ya kuzimu haitatushinda kwa Jina la Yesu.
JOSHUA 15:5-15 ….[Vile vile kama Bwana alivyomwamuru Musa, hao wana wa Israeli walifanya vivyo, nao wakaigawanya hiyo nchi. 6 Wakati huo wana wa Yuda walimkaribia Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno Bwana alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadeshbarnea. 7 Mimi nilikuwa mtu wa miaka arobaini umri wangu, hapo Musa mtumishi wa Bwana aliponituma niende kutoka Kadeshbarnea ili kuipeleleza hiyo nchi; nami nilimletea habari tena, kama ilivyokuwa ndani ya moyo wangu. 8 Lakini wale ndugu zangu waliokwea kwenda pamoja nami waliiyeyusha mioyo ya watu; ila mimi nilimfuata Bwana, Mungu wangu, kwa utimilifu. 9 Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata Bwana, Mungu wako, kwa utimilifu. 10 Sasa basi, angalia, yeye Bwana ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arobaini na mitano, tangu wakati huo Bwana alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli waliokuwa wakienenda barani; na sasa tazama, hivi leo nimepata miaka themanini na mitano umri wangu. 11 Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani. 12 Basi sasa unipe mlima huu, ambao Bwana alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye Bwana atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama Bwana alivyonena. 13 Yoshua akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake. 14 Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi, hata leo; kwa sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa utimilifu. 15 Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriatharba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.]…. Kalebu na Joshua ndio pekee waliosimamia imani yao kusema Bwana anaweza kuwavusha salama Israeli yote kwenda nchi ya ahadi. Ingawa wale wapelelezi wengine 10 walikatisha tamaa waisraeli, lakini katika Mungu, demokrasia haisemi wengi wape, bali wale wenye imani kwa Yesu hashinda kwa Jina la Yesu. Mungu amekaa ndani ya Joshua ili kuwavunsha watu kwa Jina la Yesu.  Kataika wale walioianza safari kuelekea Kanani (zaidi ya milioni sita), ni watu wawili tu ndio waliofanikiwa kuingi Kanani (Joshua na Kalebu). Wengine wote walioingia Kanani ni wale waliozaliwa njiani.
Mji wa Hebroni (ambao kabla uliitwa Kiriatharaba), vita ilikoma pale tu Kalebu alipopewa huo mji. Ahadi ya Mungu kwa Kalebu ilitimia baada ya miaka 45.  Ahadi ya Bwanani kamilifu. Wapo watu wanaomsubiria Bwana  kwa kipindi kifupi tu na papo hapo wakakata tamaa. Mungu si mwanadamu hata aseme uwongo. Anapoahidi jambo atalitimiza.
MWANZO 15:13-14 ….[Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. 14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.]…..Kuna wakati ukifika, mateso  yako yatakoma. Mungu ni Mungu wa majira na nyakati. Mungu ameweka kipimo cha mateso na kuonewa. Mwaka huu wa 2015, kwa kila anayemtumaini Mungu ni ‘mwaka wa kutoka’ kwa Jina la Yesu. Wakati huu Mungu akiongea na Abramu, ni kipindi hicho hicho ambacho Abramu na Sarai walikuwa hawana mtoto. Je,ahadi hii kwa wana wa Israeli ilitimia kwa wakati wake au haikutimia?
KUTOKA 12:40-41…[Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. 41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri.]…. Je, miaka  430 ni sawa na 400 aliyoahidi Mungu kwa Ibrahimu? Ahadi ya Mungu kwao ni kuwa ilitimia lakini kwa kuchelewa. Mungu anaposema amesema, lakini mtekelezaji ni wewe ili Mungu afanye sehemu yake. Mungu hufanya kazi pale alipokubaliwa.  Maandalio ya moyo ni  ya mwanadamu,  lakini jawabu la ulimi  ni la wandamu. Waisraeli walipaswa kutunza muda walioahidiwa na Mungu, kwa kuwa muda huu uliptimiaMungu alikuwa  kazini kuwasubiria wana wa Israeli watekeleze ahadi yake kwao ya kuwatoa nchi ya utumwa huko Misri. Matokeo yake, Mungu alisababisha kitu kitokee, kwa kumuinua mfalme mpya huko Misri asiyemjua Yusufu. KUTOKA 1:8…[Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.]…. Israeli  walijisahau, wakakaa Gosheni wakifikiri ile ni nchi yao. Mfalme asiyemjua Yusufu hufanya akili za watu zianze kufanya kazi.
2 KORINTHO 12:7-9…[Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. 8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. 9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.]… Paulo katika udhaifu aliowekewa mwilini mwake, alimsihi Mungu mara 3 lakini majibu ya Mungu kwake yakawa ‘neema yangu yakutosha’….Mungu anaweza kusababisha uwepo wa miiba ili kumfanya mtu ajirudi, na tabia za maisha ya mtu huyu zibadilike.
Wana wa Israeli walipoanza kuomba na kumlilia  Bwana,ndipo ambapo Mungu alimuinua Musa ili awatoe Israeli kutoka Misri,nchi ya utumwa (KUTOKA 3:7-8….[Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; - 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.])… wakati mwingine mtu anaweza kuwa kwenye tatizo lakini likachukua muda kuisha kwa sababu huyo mtu hajachukua hatua ya kumuomba Mungu. Wana wa Israeli walichelewa kutoka Misri kwa sababu ilipotimia ile miaka 400, walijisahau bila kumuuliza Mungu awatoe kama ahadi yake kwao  ilivyokuwa. Siyo mpango wa Mungu kuchelewesha kutoa vile alivyoahidi bali huo ni  mpango wa mashetani.
Danieli alifunga na kuomba, lakini  akachelewa kupata majibu ya Mungu.
DANIELI 11:12-14 ….. [Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. 13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi. 14 Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.]….Unapoona unapata majibu kwa kuchelewa,ujue kuna kitu kinachokuzuia,  na kitu hicho si Mungu.
MUNGU (JEHOVAH) HAWEZI KUSEMA UONGO: Ushahidi wa Kimaandiko (Kibiblia)
(a)   HESABU 23:19….[Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute;Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?]….
(b)   MALAKI 3:6…[Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.]…. Mungu wetu (Jehovha) hana kigeu geu.
(c)    TITO 1:2…[katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;]… 
(d)   YAKOBO 1:17…[Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.]….
WATU WALIOCHELEWA KUPATA AHADI ZAO KUTOKA KWA MUNGU KATIKA BIBLIA
(a)   Wanawa Israeli walichelewa kutoka Misri, badala ya kutoka huko baada ya miaka 400, kwa kutojua majira ya kujiliwa kwao walitoka kule baada ya mmiaka 430.
(b)   Danieli vivyo hivyo, alicheleweshewa majibu ya maombi yake na aliyefanya hivyo ni Mfalme wa Uajemi.
(c)    Sara alichelewa kupata mtotoo wake (Isaka), na akampata akiwa na umri wa miaka 90.
(d)   Raheli naye alikaa katika hali ya utasa kwa muda mrefu, na baadae akampata Yusufu - MWANZO 30:22-24…[Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. 23 Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu]…
(e)   Mke wa Manoa alimpata Samsoni lakini kwa kuchelewa (WAAMUZI 13:1-2;…24 …[Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto. 3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai;   lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume….. Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana akambarikia.]…
(f)     Hana alimpata Samweli lakini kwa kuchelewa (1 SAMWELI 1:2 …. 19-20)….[naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto….. 19 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka. 20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.].
(g)   ELizabethi alimpata Yohana Mbatizaji lakini kwa kuchelewa (LUKA 1:7 … 24-25)…..[Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana… . . 24 Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema, 25 Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.].
1 THESALONIKE 2:17-18….[Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu. 18 Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.]…. Mtume Paulo, mtu wa vita ndiye anayeongea maneno haya. Ndiye aliyesema ‘ingawa naenenda katika mwili, lakini sifanyi vita kwa jinsi  ya mwili’. Paulo  anawaambia Wathesalonike kuwa alitamani  kwenda kwao,  lakini hata hivyo shetani akamzuia zaidi ya mara tatu (3). Shetani anaweza kukuchelewesha usipate,  lakini hawezi kukuzuia usipate.
UKIRI
Bwana Mungu,katika Jina la Yesu, nawarudisha nyuma yangu wote walio kikwazo,  leo nawakamata, kwa Damu ya Mwankondoo, warudi nyuma yangu, aliyekaa kwenye  njia ya mafanikio  yangu, nawakamata kwa Jina la Yesu, kila kikwazo cha ushindi wangu, nakiondoa leo kwa Damu ya Yesu. Ninafanya vita na yeyote, awe ni ndugu, au  kiongozi, leo namshughulikia kwa Jina la Yesu, kwa kuwa imeandikwa, ‘shetani akamuingia Yuda ili amsaliti Yesu’,  nami nawashughulikia, mashetani mliowaingia wanadamu ili wanizuie, kwa Jina la Yesu. Amen.
 
Katika Biblia, tofauti kubwa iliyopo kati ya Musa na Joshua ni kuwa, Musa alikuwa anaomba kwanza na baada ya maombi anagawanyisha Bahari ya Shamu. Joshua kwa upande wake, alikuwa anatanguliza Makuhani kwanza katika Mto Jordani wakiwa na Sanduku  la Agano na baada ya hapo maji  yakagawanyika. Hii ilianza baada ya Mungu kumwagiza Musa aweke mikono yake juu ya Joshua na roho wa Mungu aliyekuwa ndani ya Musa akahamia kwa Joshua. Kwa hiyo, upako wa Joshua ni upako uliorekebishwa.
DANIEL 9:1-5….[Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; 2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. 3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.  4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;].. Kuna nyakatiyingine ibabidi usome  nyakati. Baada ya Daniel kujua siri iliyopo  kwenye  vitabu aliomba na kupata majibu yake. 2 NYAKATI 36:21-22 …[ili kulitimiza neno la Bwana kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini. 22 Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,]…na pia katika YEREMIA 25:11…[Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.]… Wapo watu ambao hata sasa wanamtumikia Mfalme wa Babeli, wakijua au bila kujua.
SABABU 10 ZINAZOMFANYA MTU APATEKWA KUCHELEWA

   (i).            Kutokujitambua: Mtu anayefanya vitu  visivyo sawa lakini binafsi anaona ni sawa ujue hajitambui. Ipo nguvu ya kujitambua,ambayo shetani hutumia hila za kupofusha akili za wanadamu ili swasijitambue. Matatizo mengine yapo na wala hayahitaji kufanyiwa maombi. Pindi hayo yakifanyika,mtu anawekwa huru. 
 (ii).            Kutokujua unatakiwa kuwa wapi: Pale ulipo kwa sasa sipo ambapo unapaswa kuwepo. Wana wa Israeli wakiwa Gosheni kule Misri, walidhani kuwa pale ni mahali alipokusudia Mungu  wakae, kumbe lilikuwepo eneo zuri zaidi alilokuwa amewaandalia Mungu. 
(iii).            KutokujuaMadhara ya yale uyafanyayo leo na athari zake baadae: Kila jambo ulifanyalo leo,  sirini au nuruni, lina mshahara wake baadae (furaha au  kilio).  Yona yalimkuta haya, badala ya kwenda Ninawi yeye alichepuka kuelekea Tarshishi. Wakati watu  ndani ya ile merikebu wanamuomba Mungu ili dhoruba itulie, Yona yeye alikuwa chini, amelala usingizi. Ogopa sana mtu ambaye wakati wengine wanaomba, yeye anakuwa amelala. Mtu anawezakujificha ili watu wasimuone, lakini siku ikifika Bwana atamtoa kwenye maficho yake, na siri zote kufichuka.  Ili Bahari iwe shwari, lazima Yona wa maisha yako atupwe baharini kwa Jina la Yesu. GALATIA 6:7…[Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.]…
(iv).            Kukwepa Gharama: Ukikwepa gharama kunaweza kukusababishia upate kwa  kuchelewa. Kila Baraka ina Jaribu lake,  na  kila Jaribu lina Baraka yake.  Usiwe mwepesi kumuomba Mungu alipunguze jaribu lako, kwa sababu akifanya hivyo na Baraka iliyoambatana nalo itapungua. Maandiko yanasema,mtu atakula matunda ya kazi yake. Kataa vyepesi vyepesi, lipa gharama
 (v).            Kutokujua wakati sahihi: WARUMI 13:11..[Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini]…  Mungu akupe akili ya kujua siri za mafanikio yako kwa Jina la Yesu. 1 NYAKATI 12:32….[Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini]…Ni akili pekee ya kujua majira na nyakati itakayofanya mtu kutenda kwa wakati.
(vi).            Mtu wa kulalamika na manung’uniko  kila wakati: Mtu wa aina hii, hawezi kuona jema hata moja analotendewa. Wana wa Israeli waliuawa wote jangwani kutokana na shida hii. Hii ni roho ya kuona makosa tu, nay ale mema hayaonekani.  Usiwe mwepesi kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzako, wakati boriti kwenye jicho lakohujalitoa. Soma katika Biblia katika ZABURI 106:25; 1 KORINTHO 10:10; EBRANIA 3:18.
(vii).            Kubweteka kusubiri kupewa kila kitu, hauko tayari kuonesha uwezo wako binafsi: Ukiwa kazini kwenye nafasi yako,  onesha ubunifu wa kazi ile, ili iwe rahisi kupewa cheo. Wake vivyo hivyo, wanapaswa wawe wabunifu katika ndoa zao, kwenye mapishi yao.
(viii).            Utoto wa Kudumaa na  kutokuwa  tayari kuwa mtu mzima: Mtu anakuwa ni mtu mzima, lakini maamuzi na mambo yake  ni ya utoto bado. GALATIA 4:1-2…[Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; 2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.]…. Kuna vitu vingine umekosa kuvipata kwa Bwana kwa sababu bado u mtoto. EBRANIA 5:12-14….[Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya..]….Ukiwa mtu mzima, unapata unavyostahili kwa wakati wake.
(ix).            Kukosa mtu sahihi wa kukuongoza kwenye  hatima yako: Kuna kipindi cha kutoka kwenye tatizo lako huko Misri (Musa), lakini pia anahitajika mtu sahihi wa kukuingiza kwenye nchi ya ahadi (Joshua). Unahitaji mtu sahihi, wa kukutoa dhambini na kukupeleka kwenye  Baraka zako.
 (x).            Dhambi humgharimu mtu akapata alichoahidiwa kwa kuchelewa: Muujiza na baraka zako zinaweza kucheleweshwa kutokana na dhambi. Ibrahimu aliahidiwa ampate Isaka akiwa na miaka 86, lakini kitendo chake cha kuzaa na mjakazi wake Hajiri, kilimfanya ampate  Isaka akiwa na umri wa miaka 100 (miaka 14 baadae). Dhambi ukiifanya leo, huifanya ahadi ya Mungu kwako  isogee mbele zaidi. HESABU 14:34…[Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu.]…Dhambi inaweza kuimeza ndoto yako. Yusufu alijua siri hii,  akagoma kulala na mke wa Potifa,  ili asiikose ahadi ya Mungu maishani mwake.
 
UKIRI
Bwana Yesu,nimejifunza haya ili nisije kupata vile nilivyoahidiwa wakati nimechelewa, ili nipate kwa wakati uliokusudiwa. Naomba neema yakuzitambua njia zangu, na nijue jinsi ya kuishi kulingana na mapenzi yako, Kwa Jina la Yesu. Amen.

Comments