KIJANA USIKUBALI KUHARIBU UJANA WAKO.

BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze.
Neno '' KUPENDA''limekuwa msamiati mgumu sana kwa vijana wa leo, shetani amefanikiwa kwa asilimia 90 kuwanasa vijana wengi na kuwaangusha katika dhambi, akitumia msamiati huu NAKUPENDA.

 2 Timotheo 2:22 ''  Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. ''
-Kwa Wasichana Kusumbuliwa Na Vijana Wasio Na Hofu Ya MUNGU Limekuwa Ni Jambo La Kawaida. Kwao Ni Kama Vile Usivyoweza Kuwazuia Ndege Wasiruke Juu Ya Kichwa Chako. Lakini Licha Ya Hayo Mimi Naamini Kila Msichana Anaweza Kuwazuia Ndege Hao Wasijenge Viota Kwenye Nywele Zake. Dada Najua Umeshindwa Kuwazuia Ndege Kuruka Juu Ya Kichwa Chako Lakini Naamini Unaweza Kuwazuia Ndege Hao Kujenga Kiota Kwenye Kichwa Chako, Shika Utakatifu Na Utunze Wokovu Wa BWANA YESU Kama Pesa.
-Mabinti jizuieni na uasherati, jizuieni maana nyie ndio mara nyingi mnafuatwa. upendo hauko katika ngono.

1 Kor 5:10  Biblia inasema ''Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.''
-Wazinzi na wenye kutamani tunao katika mazingira yetu iwe ni nyumbani au ni kazini lakini ni jukumu lako binti kukataa kutumiwa kama chombo cha kujifurahishia wadhalimu. Kataa dhambi ya uzinzi, ogopa dhambi ya uzinzi, ikimbie dhambi ya uzinzi na usifanye dhambi ya uzinzi.

 BWANA YESU Anakupenda Sana Na Hataki Ukose Uzima Wa Milele Kwa Sababu Ya Hao Ndege Wanaoruka Juu Ya Kichwa.

Ufunuo 21:8 '' Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.''
-Kumbe katika watakaopelekwa jehanamu na wazinzi wamo.
-shetani analeta kila mitindo ya mavazi na mapambo ili tu kuwanasa vijana katika dhambi ya uasherati.
-Uzinzi ni moja ya dhambi zinazowakosesha wengi.
-Nduguyangu, uzinzi wa muda mfupi unaweza kukupeleka kabisa jehanamu kama hukupata nafasi ya kutubu, na sio wote wanaopata nafasi ya kutubu na kugeuka.
-Uzinzi na uasherati ni dhambi ving'ang'anizi na ndio maana shetani huitumia sana ili kuwaangamiza maelfu ya vijana, uzinzi unamfanya shetani anapata nafasi ya kukutawala. 
ndugu kupitia ujumbe huu nakuomba badilika. Na kama umeona imekuwa ngumu mweleze mchungaji wako akusaidie na kukuombea maana wengi hadi wana majini mahaba. 
Mithali 6:32-33 '' Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. '' 
 -Mvulana Leo Akimwambia Msichana "NAKUPENDA" Maana Yake Hasa Ni " NATAMANI KITU, SIO WEWE MWENYEWE BALI KITU KUTOKA KWAKO, SIWEZI KUNGOJA, NATAKA KUWA NACHO SASA HIVI, BILA KUCHELEWA. SI KITU NINI ITAKAYOTUKIA BAADAE. NINAANGALIA WAKATI HUU, NINAYO HAJA KWAKO ILI KUZITULIZA TAMAA ZANGU, WEWE NI CHOMBO TU CHA KUNIFIKISHA KWENYE SHABAHA YANGU, NATAKA KUWA NA WEWE MUDA HUU" 

Hiyo Ndio Maana Ya Neno "Nakupenda" Kwa Maisha Ya Leo Kwa Vijana Wengi. Maana Halisi Ya Kijana Kama Huyo Ni Hii "NINAJIPENDA MIMI MWENYEWE PEKE YANGU TU, KWA SHABAHA HIYO NAMTUMIA MSICHANA KUKAMILISHA KUJIPENDA KWANGU". 
 Wasichana Wengi Nao Hujikuta Wakiingia Kwenye Upendo Huu Feki Na Kuingia Dhambini. 

Ndugu Zangu Tambueni Neno Hili Kwamba MUNGU Atawahukumu Adhabu Ya Jehanamu Wazinzi Na Waasherati, Waebrania 13:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu. '',  

 BWANA MUNGU Anawaonya Wanadamu Kila Leo Ili Waache Uovu Huu. Dhambi Hii Ndio Ilisababisha Sodoma Na Gomora Kugeuka Matanuru Ya Moto Na Kuwateketeza Wanadamu Wote Isipokuwa Lutu Na Familia Yake
1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.   ''

 Upendo Wa Kweli Haukamiliki Isipokuwa Katika Ndoa Takatifu Mlioingia Bila Dhambi. Kwa Hiyo Mvulana Asitaje Lile Neno Kubwa La Kusema "NAKUPENDA" Kwa Msichana Asipokuwa Na Nia Ya Kufunga Nae Ndoa Tena Asiseme Neno Hilo Huku Akiwa Na Mpango Wa Kufunga Ndoa Miaka 10 Ijayo Bali Miezi Kadhaa Ijayo.
 Yakobo 4:4 ''Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU.''Wazinzi ni adui wa MUNGU, Ukianguka kwenye dhambi ya uasherati au uzinzi kwa sababu tu ulidanganyika na neno ''nakupenda'' basi wewe unakuwa adui wa MUNGU hadi utakapotubu.

Kijana na kiume au wa kike tambua kwamba  wewe ni wa thamani sana mbele za MUNGU, Tunza uthamani wako na mwili wako bila kufanya uasherati. 

Maombi yangu MUNGU akupe kinga kwa kila hatari iliyo mbele yako, akupe baraka kwa kila jambo jema unaloliwaza na kulipanga kwa ajili ya maisha yako ya baadae yakiwemo maisha ya ndoa, BWANA akupe jibu katika ombi lako la kumpata mwenzi wa maisha mwenye hofu ya MUNGU, BWANA YESU akupe tabasamu kwa kila chozi unalolia ukimuomba akupe mme/mke mwema, akujalie afya njema, furaha,amani na upendo.  Nguvu ya MUNGU likasimame na wewe katika magumu unayopitia hadi ushindi wako  na maadui zako kuanzia walio ndani hadi walio nje  kwa jina la YESU KRISTO washindwe. 
BWANA YESU akuondoe kwenye maagano ya ukoo na mizimu yanayokuzuia kuoa au kuolewa. MUNGU  akawafunge waliokufunga,wawe mateka waliokufanya mateka,wateseke wao waliokutesa,waliokufungia uchumi wafungwe wao.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Vijana wa kiume wanatakiwa kuwa makini sana, na wawe na hofu ya MUNGU ili kupinga dhambi ya uasherati kablya ya ndoa..

Mabinti ni kundi linalotakiwa kuwa makini zaidi dhidi ya mapenzi ya kabla ya ndoa.

Comments