ABEL SHIRIWA:KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTOSEHEMU YA 3

Na Abel Suleiman Shiriwa
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA
Inaendeleaaaaaaaaa.....

Baada ya kuinuka nilipokuwa nimeanguka, kucheki nyuma yangu nikawaona waislamu wenzangu ambao miongoni mwao ni wale ambao tulikuwa pamoja nao wakija mbio huku wanazivua kanzu nzao, wakaniambia "kimbia wewe wenzetu wameshakamatwa" Nikawaambia, "Hata mimi nimewaona ndo maana nimekimbia hadi kuanguka" nami nikaivua kanzu yangu nikaitupa, ili hata kama Polisi watakutana nami, nitawaambia me Mkristo nakimbia vurugu za waislamu,, tukaendelea kukimbia mpaka msikiti wa kirumba, Siku hiyo tuliingia na viatu na kina mama nao kwa uoga ule waliingia nao upande wa wanaume, hapo tukiwa na hofu, nilikaa kidogo mle ndani, nikafikiria kule kumeshasanuka, ni lazima Polisi watakuja huku, nikaamua kutoka zangu, wenzangu nikawaacha humo, nikiwa na pensi yangu, pamoja na TISHETI, nikazunguka kupitia uwanja wa CCM KIRUMBA,
Nikatokezea Ghana Kotazi, nikaingia zangu home Ghana mtaa wa kifua wazi, nikakuta milango imefungwa, nikawagongea wakanifungulia, nikawakuta wengine wanatokwa machozi, nikawauliza "Kulikoni?" Wakasema BOMU la machozi, limerushwa nje hapo wakati tumekaa ikabidi tukimbie, Wakaniuliza mzee yuko wapi? Nikawaambia "Tulipoona wenzetu wanakamatwa, mimi nilikimbia kuelekea msikiti wa Kirumba, mzee yeye aliekea upande wa MAKONGORO, kwa hivyo sijui kama amekamatwa au vipi" Wakaniuliza "Kanzu iko wapi?" Nikawaambia "Nyie acheni tu, Wakati nakimbia na Kanzu, nilikula mweleka wa hatari, walipokuja wenzangu, nikawaona kanzu zao wanazitupa, nami nikaona ni kheri niitupe maana nilikuwa naiona nzito" Wakanicheka, nikawaona wananizingua tu, basi nikaenda bafuni, Wakati naoga nikamsikia Mzee anaita, Aboubakariiii Wakamfungulia, nami kwa haraka nikatoka bafuni, maana bafu ni la ndani. nikamkuta ana hema balaa, nikamtazama, akacheka, akasema, "Al-hamdu Lillah, الله اكبر (Mungu mkubwa) Nikamtaza nikamuona shati lake limechanika, Nikamwambia, اخي كيف? (Ndugu yangu vipi)? Akasema, "We acha tu nilipokimbilia kumbe ndiko Polisi wanakotokea, mmoja alishika shati, nikatumia nguvu kumsukuma, ndipo shati langu likachanika kipande amebaki nacho nikatoka mbio, nikavuka barabara pale MISSION, Nikaona geti liko wazi badi nikaingia zangu mle, nikawakuta makafiri wapo nje wanaimba" (Aliingia kwenye eneo la Kanisa la AIC MAKONGORO) Tukacheka, akasema, "Nikakaa kwenye nyasi huku nahema, Wakanifuata, nikawaambia kule FURAHISHA waislamu tunakimbizwa na polisi, kwa sababu waislamu wenzetu, wameng'oa Vyuma vya Wakristo, mimi nilienda kwenye muhadhara, ndo nikakuta vurugu hizo ndo maana nimekimbia, wakanipa pole, Wakaniletea maji nikanawa, nimekaa pale mpaka hali imekuwa shwari, ndo nikaja" tuliongea mengi, chakula kikaiva, tukala, tukalala,
Kesho yake kama kawaida nikaenda zangu school, baadae madrasa, Tukatoka saa 12 Nikaenda msikiti UHURU, kuswali, baada ya swala, tukatangaziwa kuwa Kina Mazinge, Issa Kalenga, na baadhi ya Wahadhiri wamekamtwa, kwa hivyo kesho baada ya swala ya IJUMAA, tukutane pale GHANA GREEN VIEW, Pale Thaqibu, Kitengo ambacho kilikuwa kina simamiwa na marehemu ILUNGA KAPUNGU, tukutane pale.kwa ajili ya kujadili hatima ya ndugu zetu, waliokamatwa, baada ya Tangazo hilo nikaondoka zangu kwenda home, na kesho yake tukaenda kweli THAQIIBU, tukaelezewa kuwa baada ya kukamatwa, walipekwa polisi, na Leo wamepekwa Mahakamani, wamenyimwa, dhamana, Waislamu tulichukia, ila tukaambiwa tutulie kwani Masheikh watafuatilia.
Kipindi hicho kina MaZINGE walikaa Butimba miezi mine, mimi nikaendelea na mambo yangu, na Rafiki zangu wa KIKRISTO nikaendeelea kuwabana kwa maswali, kutokana na zile aya ambazo nilikuwa naziandika kutoka kwa Wahadhiri wa kiislamu, nikaonekana bonge la Mwalimu, baadae Kina Mazinge wakafutiwa kesi, wakatoka, wakaandaa muhadhara, Mkuyuni, nikawa nawafuatilia, baadae waliondoka MWANZA, wakabaki Wahadhiri wa Mwanza, nikaendelea kuhudhiria, Hapakuwa na Mkristo alieonyesha upinzani mkubwa, katika Muhadhara uliofanyika tena FURAHISHA, kuna Mkristo alikuwa anasomea uchungaji, akasilimishwa, furaha yangu ilikuwa kubwa sana siku hiyo, Baadae kukawa kimya hakuna mihadhara, kama miezi mitano, SIKU MOJA Natoka zangu shule, Mida ya saa 10 Jioni nikiwa kwenye gari, nikasikia sauti.ya HON SPEKEAR uwanja wa FURAHISHA, nikasema huo utakuwa ni muhadhara, nikaenda home nikabadili nguo hata sikula, huyo nikaenda UWANJANI, Nikashangaa kukuta sura ngeni, tena wamevaa tai, wanaichambua quran na kuonyesha udhaifu wake, nikauliza "Kina nani hawa?" Nikaambiwa, NI SIMBA ULANGA NA Daniel Mwankemwa Ni wahubiri Wa Kikristo kutoka DAR, nikashangaa nikajiuliza Hawa Makafiri wamejifunzia wapi Quran? Wakaitisha maswali, Wakati nataka kwenda, nikamuona IDDY muhadhiri wa MWANZA ameshakaa kwenye kiti cha maswali, , akapewa maiki, (Kama walivyokuwa wanafanya kina MAZINGE kwa Wakristo) Akauliza swali, Kwa kutoa quran 22:78 Kuwa sisi tumeitwa Waislamu ndani ya quran,, sasa niandiko gani katika BIBLIA, ninyi mmeitwa Wakristo? tukapiga Takbiir tukijua kuwa hawatajibu, Lakini kumbe Ilikuwa ni tofauti na mtamzo wenu, Alisimamishwa Mwankemwa, Akatoa Wagalatia 3:27-29 Ilipomalizika tu kusomwa, Wakristo wakalipuka furaha, Nikanywea, nikamatazama IDDY, Nikamwambia "Inuka me nikae niulize, Akainua mkono na kuniashiria nitulie, Nilivyoona kila hoja yake anabwana, Nikajiuliza nimetoka home bila kula, halafu nije kuambulia aibu hii? Kwa hasira NIKA......... UTAENDELEA.
USIKOSE SEHEMU YA 4 YA USHUHUDA HUU KESHO SAA 3 USIKU.

Comments