KUTUBU NI KUMRUHUSU MUNGU AKUSAIDIE, TUBU.



BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze toba.
Isaya 59:2-5 ''  lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya.Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.''

Uovu ni mbaya, uovu unaweza kukupeleka jehanamu.
Uovu ni dhambi na dhambi huzaa mauti.

Madhara ya dhambi kulingana na Isaya 59:2-5.
1.Dhambi zinaweza kumfanya MUNGU asisikie kile uombacho.
2. Dhambi zinamfanya mwanadmu awe adui wa MUNGU.
3. Dhambi humnajisi mtu hata akawa chukizo.
4. dhambi huufanya hata mwili usiwe na thamani tena kwa MUNGU.
5. Dhambi huondoa ukweli na kumukandamiza mtu mkweli.
6. dhambi huzaa mimba ya mabaya.
7. Dhambi hutaga mayai ya nyoka na hutotoa nyoka  na nyoka ni shetani, maana yake dhambi na shetani ni mtu na mtoto wake. dhambi na shetani ni mtu na damu yake. shetani na dhambi ni sawa na dhambi ndio bomu pekee ambalo shetani hutega ili mwanadamu alipuke nalo hilo bomu maana mwanadamu akiitii tu dhambi maana yake amemdharau MUNGU na kumdharau MUNGU ni kujipeleka kuzimu.

Nini kifanyike?

Matendo 3:19 '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;   ''Kwanini MUNGU anataka kutubu?
Ni kwa sababu '' ... twajua ya kuwa hukumu ya MUNGU ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. -Warumi 2:2 '' na ndio maana BWANA YESU anasema ''  Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.-Luka 5:32 ''
Kiuhalisia hakuna mwenye haki hata mmoja hata asimhitaji BWANA YESU ila wale wenye haki feki za kujihesabia hao hawamhitaji YESU, hata ukiwambia watubu watakataa maana hawajitambui. lakini kwa anayetbu na kumpokea BWANA YESU, MUNGU husema kwake kwamba '' Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. -Isaya 43:25''. Hakika huu ni upendo wa ajabu sana lakini wanadamu wengi hawataji toba maana wamejaa viburi hata pale pasipohitaji kiburi. kiburi hakihitajiki kwa MUNGU maana kiburi kilimshusha lucifer na kiburi hicho hicho kitawapeleka kuzimu wanamkataa BWANA YESU kwa sababu ya viburi vyao na kujikinai, BWANA YESU anasema '' Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.-Yohana 3:19-20''

Ndugu, fanya ujanja ujanja wote lakini kwa BWANA YESU hakuhitajiki ujanja wala usela bali kutubu tu.
Tubu na BWANA YESU atakusamehe.  hakika akitubu mmoja tu huwa ni furaha mbinguni, Luka 15:7 ''Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu. ''. 

 Kutubu kuna maana sana kwa MUNGU ndio mlango wa kumruhusu MUNGU akuangalie tena hata kama kwa miaka mingi alikuwa amegeuza uso wake asikuangalie. Kutubu ni kumfanya BWANA aseme ''karibu mwana mpotevu'' usitende dhambi tena. Ktubu kuna maana sana na ndio maana '' Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.-Zaburi 32:1-2''  ndio maana mimi nasema kwako ndugu kwamba ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. -1 Yohana 1:9''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments