NCHI YAKO NI URITHI WAKO ULIOPEWA NA MUNGU. MWANZO 13:15.

Na Godfrey Miyonjo.

BWANA YESU asifiwe sana,
Wapendwa wana wa MUNGU ningependa kila mmoja ajue kuwa imeandikwa:
“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake” ZABURI 24:1.
Tukisha kulijua hilo ningependa pia tujue kuwa imeandikwa:
“bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” YOHANA 1:12.
Baada ya kuyajua hayo ndiyo tuje kwenye somo letu
“NCHI YAKO NI URITHI WAKO ULIOPEWA NA MUNGU”

Tunaposoma neno nchi katika biblia lina maana ya ARDHI,
Na uwepo wa ARDHI na watu ndani yake ndiyo hupelekea uwepo wa taifa.
Watu wengi hudhani kuwa uwepo wa mataifa mbalimbali kuwa ni mpango wa shetani kitu ambacho si kweli.
Siyo kweli kwasababu shetani hana Nchi/ardhi na wala dunia siyo mali yake.
Kama ilivyoandikwa kuwa Dunia hii na vyote viijazavyo ni mali ya MUNGU nasi kama wana wa MUNGU tunapaswa kujua kuwa huu ni urithi wetu.
Mungu katika milki yake ametugawia sisi wanawe maeneo ya kuyamiliki.
Mimi kuzaliwa Tanzania bara (Tanganyika), au wewe kuzaliwa Kenya, Uganda, Burudi, Rwanda, Malawi, Sudani N.K na kuwa raia wa hapo ni mpango wa Mungu kuturithisha Ardhi/Nchi hiyo.
Mungu kama Baba yetu anataka kutuona tukisimamia vyema ule irithi aliotupa.
Mungu anataka kuona sisi wana wake tukitambua thamani ya ya urithi wetu na kujivunia urithi wetu.
Mungu Hataki kuona tukitapanya mali (kuutumia vibaya urithi), tukiwaachia wezi watuibie, tukiudharau urithi wetu.
Mungu hataki kuona tukiishi maisha duni kwa kukosa fedha, chakula, mavazi na mahitaji mengine yoyote yale.
Mungu hataki kuona mafisadi wakijinufaisha wao na familia zao rasilimali za nchi na kuwaacha wengine ndani ya nchi hiyohiyo wakiwa ni maskini wa kutupwa.
Mpendwa mwana wa Mungu usijidanganye kuwa eti madini, mafuta na kila rasilimali zilizopo zinawahusu wapagani, wachawi, wapungapepo, wanajimu, wanasiasa, N.K.
Hivi vyote ni mali ya Mungu wetu, na sisi kama watoto wa Mungu tuna hati miliki ya vyote.
Huu ni wakati wa sisi sote Kutiisha na kutawala vyote vilivyopo chini ya jua. MWANZO 1:28.
Ni wakati wa kukataa kutawaliwa na roho umaskini, roho ufukara, roho kutojitambua, N.K.
Ni wakati wa sisi kusimama kama wana wa Mfalme Mkuu, katika ulimwengu wa Roho na katika ulimwengu wa damu na nyama (mwili) pia,

Ni wakati kila mmoja kuiombea nchi yake (taifa lake), ili vile vyote vilivyoshikiliwa na mwovu viachiliwe.
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, SIMAMA LEO ILI UMILIKI NA KUTAWALA.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu
)

Comments