WATIINI WENYE KUWAONGOZA KIROHO.


Soma paka mwisho upate maarifa
USHUHUDA:KISA CHA MCHUNGAJI NA WASHIRIKA!!
Mchungaji wangu aliniambia ushuhuda Huu ambao nimeona vema kukushirikisha ili upate kujifunza mpendwa

Siku moja mchung
aji aliamua kuteua vijana ambao watakuwa na huduma ya kukemea mapepo na kuombea huduma ya madhabahuni(ibada iwe na uwepo Wa Mungu)

Vijana wale walipoanza huduma hiyo walifanikiwa kwa asilimia mia maana,mapepo yalikuwa yanatoka/uwepo Wa Mungu unashuka/wagojwa wanapona n.k
CHA KUSHANGAZA
Baada ya vijana wale kuona huduma ile wanayoifanya ndyo inayoleta matunda pale kanisani wakaanza kumpatia mlango shetani!

VIJANA WAKAANZA KUJIKWEZA
wakaanza kusemezana!!MCHUNGAJI WETU KAPOA yani sisi ndyo tunasababisha uwepo Wa Mungu ushuke kwenye ibada!
-sisi ndyo tunatoa mapepo
-sisi ndyo tunawahudumia hili kanisa

Yani mchungaji huyuu kazi yake kuhubiri tu!tena hata mahubiri yake yamepoa kabisa!!!!
Yani bila sisi hapa kanisani!!kanisa ili lingekufaaaa kabisa!!kama ameanguka si aondoke tu atuachie kanisa tufanye kazi ya Mungu!!-(vijana hawa walikuwa wakijadili)
INASIKITISHA SANA
Zili pita siku kadhaaaaa yale maneno yalidhidi kuenea ndani ya kanisa!!washirika wanamsema vibaya mchungaji wao!!!

Siku moja mchungaji alibahatika kusikia maneno yale!!
Yalimuumiza sana
Alilia sana mbele za Mungu wake!!!

Lakini hakuamua jambo lolote!!aliamua kunyamaza tu!!(wachungaji wamepewa moyo Wa kuvumilia sana)
NDIPO ASIRA ZA BWANA ZIKAWAKA NDANI YA KANISA!!
Mungu akaamua kumtuma mtumishi wake toka kenya kuja kwenye kanisa hilo kuwaambia maneno aliyotumwa na Mungu!!

Mtumishi huyu wa Mungu kutoka kenya aliwasili jumapili asubuhi na mapema!!
Kilipofika kipindi cha kuwatambulisha wageni!!
Ndugu yule alisimama na kuanza kujitambulisha(kwa bahati mbaya au nzuri!yule aliyekuwa anakaribisha wageni ndyo alikuwa kiongozi wa kumsema vibaya mchungaji)

Kenya alipo simama alisema "mimi nimetumwa na Mungu nije hapa kuwaambia kwamba MUNGU AMEKASIRIKA!!!KUNA VIJANA WENGI HUMU KANISANI WAMEMSEMA MCHUNGAJI VIBAYA!!MUNGU AMEKASIRIKA SANAAA!!!
MUNGU ANAWATAKA MUJE HAPA MBELE MCHUNGAJI AWAOMBEE MSAMAHA njooni hapa mbele(mkenya yule alisema huku akiwa analia)

Nusu ya vijana wapatao14 walipita mbele akiwemo yule aliyekuwa anaongoza ibada!!!
Mkenya yule akasema"Mungu anasema bado kuna watu hawataki kuja Mungu anawaita!!njoooni maana mtakufa(alisema kwa hunzuni sana)
Vijana wakadhania kama utani!hawakutoka mbele!!
Mchungaji alipowaona wale waliotoka na walikuwa kama watoto wake!!alilia sanaaaaaaaa!!!akawaombea kwa Mungu rehema!!!
Baaada ya siku chache wale vijana waliokataaa kutoka mbele kutubu wote walikufa!!
JE UNAONA JINSI MUNGU ANAVYOCHUKIA KUWASEMA VIBAYA WATUMISHI WAKE???
JE NA WEWE UPO KWENYE KUNDI HILO?
Biblia inasema hivi
Watiini wenye kuwaongoza,na kuwanyenyekea;maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu,kama watu watakaotoa hesabu,ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua:maana usingewafaa ninyi(waebrania13:17)

MAMBO AMBAYO MCHUNGAJI ANAWEZA KUKUONGOZA KWA KUUGUA:
1:TABIA ZA ULIMWENGU
Tabia hii imewaathiri washirika wengi sana makanisani!
Unakuta mshirika yupo kanisani lakini anatabia chafu:
-mtukanaji
-mnzinzi
-muongo
-msengejaji
Sasa tabia hizi anapokuwa nazo mshirika kwanza zinachafua sifa ya kanisa pia sifa ya mchungaji!!!!
Kwa maana hiyo unamtesa mchungaji wako kukuchunga!!
NDUGU YANGU MWENYE TABIA HII GEUKA MAPEMA maana unapomtesa mchungaji wako ni sawa unamtesa Mungu!!

2:UTORO
Baadhi ya washirika huwa wanatabia hii!!!unakuta mshirika kwenda kanisani kwenda mwenzi paka mwenzi!
JE NI NANI ATAJUA MAENDELEO YAKO YA KIROHO??

JE MCHUNGAJI ATAKUWEKA KWENYE KUNDI LIPI KONDOO au MBUZI???
Maandiko yanasema
Lakini ndugu tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu,na kuwasimamia ninyi katika bwana,na kuwaonyeni
13 mkawastahi sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao.iweni na amani ninyi kwa nyinyi.

Leo mchungaji anayekesha kwa ajili yako we unamdharau?
Leo Mchungaji anayekuhudumia kiroho unamsema??
Ngoja nikupe kaushuhuda kidogo!
Mchungaji mmoja alionyeshwa maono na Mungu kuhusu mshirika wake kuwa roho ya ajari inamfuata!!
Mchungaji aliamua kufunga na kuomba kukemea roho ile ya ajali!!!
Mchungaji aliamua kumuita yule ndugu kumuambia yakupa uombe kufunga roho ya ajali inayokufuata.lakini ndugu yule kila akiitwa anasema yuko busy!NI AJABU SANA

Mchungaji akaendelea kumuita lakini hakusikia alijidai busy kuliko kutii sauti ya mchungaji!!
Siku moja yule ndugu anampigia simu mchungaji na kumwambia amepata ajari na kuvunjika miguu yoteee!!!
Mchungaji alisikitika sana akasema "laiti angenitii yasingemkuta haya"
CHA KUSHANGAZA NA KUSIKITISHWA!
-Wapendwa Wa Leo kumuona mchungaji wao paka wapatwe na shida lakini kwenye rahaa ndio hao wakwanza kumsema vibaya mchungaji!!!!

Ndugu yangu huko ni sawa na kujidanganya mwenyewe!!!
Unawezaje kupokea baraka kwa mchungaji wakati moyo wako haupo pamoja naye???
HUKU NI KUJIDANGANYA MWENYEWE!!!

TUKIANGALIA KISA KUTOKA KWENYE BIBLIA
Hesabu16:1 na 16:45
Unapata tukio nzima!!tukiangalia kwa ufupi!!!

Hesabu16:1
Basi kora mwana Wa ishari!mwana Wa kohathi,mwana Wa lawi,akatwaa watu pamoja na Dathani na Abiramu,wana Wa eliabue na oni mwana wa pelethi,waliokuwa wana Wa Reuben,
2 nao,pamoja na watu kadhaa Wa wana Wa israel na watu mia na mbili na msini wakuu wa makutano waliokuwa wateule Wa mkutano watu wenye sifaa WAKAINUKA MBELE ZA MUSA!!

Ukisoma kwa makini Kora anajaribu kujiinua awe kama Musa!
3 nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni na kuwaambia,NINYI INAWATOSHA,kwakuwa mkutano wote ni mtakatifu,kila mmoja miongoni mwao.BWANA naye yu kati yao:n nini basi kujitukuza juu ya mkutano Wa BWANA?
Ukisoma kisa hiki vinziri utaelewa vinzuri!
Kora alipotakuwa kuwa kama Musa ndipo Musa alipoanza kumlilia Mungu akamwambia Mungu watu hawa wasife kifo cha kawaida!wafe kifo ambacho watu wataamini ni nani uliyemchagua!
Ukisoma Hesabu16:30-45
Musa akawaambia wanaomkubari kora waende upande huo na wanikubali Mimi waje upande wangu!ndipo asira ya Bwana ikawaka juu ya kora na watu wake!!ardhi ikapasuka ikawameza!!haaaahaaaaaaaaa INATISHAAA

JE WEWE AUGOPI???
kwanini unawasema vibaya watu Wa Mungu??
Kwanini unataka kijiinua kama mchungaji wako??
Kwanini unawasumbua watu Wa Mungu/auwatii??
Je unajua Mtu wa
Mungu akikwazika juu
yako Mungu ataachia mapigo juu yako??

Huu ni wakati wako wakubadilika ndugu
S E M A M A N E N O
H A Y A K W A
K U M A A N I S H A

Ninaomba Neema Yako Ee, Mungu Uliye Hai,
Baba Yetu Wa Mbinguni, Uishiye Milele Na Milele,
Na Kwa Kupitia Mamlaka Ya Jina Lako, Ee Yesu
Kristo Wa Nazareti, Mwana Wa Mungu Uliye Hai,
Ninakuomba Utakaso Mbele Zako Ee Mungu Uliye
Hai Milele Na Milele, Na Mbele Zako Ee Bwana
Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Uliye Hai Milele Na
Milele, Na Mbele Zako Ee Roho Mtakatifu, Uliye
Hai Milele Na Milele, Nami Ninaupokea Utakaso
Huu Sasa, Ulioniandalia Kabla Ya Kuwekwa
Misingi Ya Ulimwengu, Na Kwa Kifo Chako Ee
Bwana Yesu Pale Msalabani, Ninajitakasa Sasa
Na Hata Milele Kwa Utakaso Huu Kwa Damu Ya
Yesu Kristo Mwana Wa Mungu, Uliye Hai Milele
Na Milele,naomba unisamehe dhambi zangu
-nimewasema vibaya watumishi wako ulioniwekea wanichunge!!
Nisamehee kwakutowatii Bwana Yesu
Na Kwa Utakaso Huu Kwa Neno La
Mungu Uliye Hai Milele Na Milele, Na Kwa
Utakaso Huu Kwa Upako Wa Roho Mtakatifu Wa
Mungu Uliye Hai Milele Na Milele; Na Kwa
Utakaso Huu Kwa Jina La Yesu Kristo Wa
Nazareti, Mwana Wa Mungu Uliye Hai, Uishiye
Milele Na Milele! Na Kwa Utakaso Huu Ninazifisha
Nguvu Zote Za Kila Aina Ya Dhambi, Na Kila Aina
Ya Uchungu Wa Dhambi, Na Kila Aina Ya
Magonjwa, Na Kila Aina Ya Udhaifu, Na Mauti. Na
Kwa Utakaso Huu Ninang’oa Kila Aina Ya Pando
Lisilopandwa Na Baba, Mungu Uliye Hai, Katika
Jina La Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Uliye Hai
Milele Na Milele, Amina!

HITIMISHO
Ningependa kusikia kitu kwako!!je somo hili limekusaidiaje kiroho??

Umebarikiwaje na somo hil??
NA MUNGU AKUBARIKI
nitumie ujumbe wako kwa mawasiliano zaidi
Sheikhedenhazard@gmail.com
GLORY TO GOD

Comments