IJUE HUDUMA YAKO NA ANAYETOA HUDUMA KATIKA MWILI WA KRISTO NA INAVYOTENDA KAZI (SEHEMU YA III)

Na Emmanuel Kamalamo
Bwana Yesu asifiwe!
Nawasalimu kwa Jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu.
Natumaini katika Kristo sote tu wazima katika mwili
na roho.
Leo tunaendelea na somo letu, hivyo fuatana nami
namuombe ROHO MTAKATIFU aliye mwalimu awe pamoja
na wewe uposoma mafundisho haya, akufunulie akili upate kuelewa na maandiko juu ya kile kilichomo katika somo hilinasi ili uwelewe anachotaka tuelewe katika jina la
Yesu Kristo Amen.

Msingi wa somo letu ni Waefeso 4:8-12. Hasa
uzungumzia Huduma tano katika mwili wa Kristo.
Pia kuna karama 9 katika mwili wa Kristo, na vyote
hivyo uvitoa ROHO MTAKATIFU.Hatutazungumzia karama za Roho Mtakatifu bali tujifunza juu ya huduma tano.

JINSI HUDUMA TANO ZINAVYOTENDA
KAKI KATIKA MWILI WA KRISTO.
NA SIFA ZAO.

>>HUDUMA YA MTUME.
Ukisoma katika Waefeso 2:20 maandiko yanasema hivi; "Mmejengwa juu ya msingi wa mitume
na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu
pembeni" pia tusome kitabu cha
1 Wakorintho 12:28 " maandiko yanatwambia;.."Na Mungu ameweka wengine
katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii
wa tatu waalimu..." unaweza kujiuliza na Mwinjilisti na Mchungaji mbona hawapo? si kwamba hawapo, wapo, bali alitaka kuzungumzia "UMUHIMU WA HUDUMA HIZI" ndani ya kanisa ingawa zote zina umuhimu. Kanisa bila Mtume kanisa halipo, Utauliza Emmanuel una maanisha nini?...na maanisha hivi; Mtume asipokwenda mahali kufungua kanisa hapawezi kuwepo na kanisa, kama kanisa halipo hujue hapawezi kuwepo Mchungaji.Pia Nabii bila kuwepo ndani ya Kanisa kanisa litakosa kusikia kutoka kwa Mungu na kuona adui anayetaka kuingia ndani ya kundi (Kanisa) Vivyo hivyo kanisa Kama halina Mwalimu Kanisa haliwezi kusimama na kukua kwa chakula kile cha ndani kitokacho katika Huduma ya ualimu kwa mtu mwenye huduma hiyo ndani ya kanisa, Mchungaji atachunga sawa lakini bila mafundisho kondoo watamfia machungani mahali pasipo na majani ya malisho.

Tunaposoma mistari hii tunapata kujua juu ya
Huduma ya MTUME ilivyo ya kwanza na muhimu
katika kanisa (mwili wa kristo) Na kanisa lazima
lijengwe juu ya MSINGI wa mitume na manabi.
Na MITUME na MANABII pia na wao msingi walio
nao uko juu ya JIWE KUU la pembeni ambalo ni
YESU KRISTO......"TAZAMA, NAWEKA JIWE KATIKA
SAYUNI, LIWE MSINGI, JIWE LILILOJARIBIWA, JIWE
LA PEMBENI LENYE THAMANI MSINGI ULIO
IMARA.." Isaya 28:16.

MSINGI NI NINI?
> Ni mafundisho sahihi na imani sahihi katika Kristo
Yesu.
Yesu Kristo ndiye MSINGI WA KWELI (JIWE KUU LA
PEMBENI) ambalo Mitume wamejengwa juu ya
MAFUNDISHO sahihi na IMANI sahihi na kanisa
(mwili wa Kristo) wanajengwa juu ya mafundisho ya
Mitume.
Kwa mantiki hiyo kipindi cha Yesu (kanisa la
kwanza) Huduma ya KITUME NA KINABII ilifanya
kazi sana ili kusimamia IMANI na MAFUNDISHO.

NINI MAANA YA MTUME?
>Mtume kwa lugha ya Kiyunani ni
APOSTOLES.Maana yake "ALIYETUMWA" Tusome kitabu cha Warumi
1:1 maandiko yanasema,,,"Paulo,mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa
mtume.."

KUNA MAKUNDI MANNE YA MITUME
1.MTUME MKUU.
>Yesu Kristo ndiye Mtume mkuu. Waebrania 3:1
"..Mtafakarini Mtume na Kuhani MKUU.."
Yesu ndiye MTUME MKUU na AME EBA Huduma
zote tano.
>MTUME
>NABII
>MWINJILISTI
>MCHUNGAJI
>MWALIMU.
2.MITUME WA MWANA KONDOO
>(Mitume 12) Luka 6:13 "Hata kulipokuwa mchana
aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili
miongini mwao, ambao aliwaita Mitume".
Kati ya wanafunzi wengi wa Yesu alichagua kati yao
wawe Mitume atakao watuma.

SIFA ZAO.
A.Walishuhudia maisha ya Yesu.
B.Waona kifo cha Yesu.
C.Kuzikwa kwa Yesu.
D.Kufufuka kwa Yesu.
3.MITUME WA AGANO JIPYA WANAOTAJWA
KATIKA BIBLIA.
>Waliongezeka wakina Paulo,Mathiya,Barnaba na
wengine wengi walioitwa na Kristo watumwe kama
Mitume.

4.MITUME WA LEO.
>Ni kipindi hiki tulicho nacho Mungu anatoa Mitume
kwa kazi ya Kitume.

SIFA ZA MITUME.
A) Lazima Mtume awe muhubiri wa Injili, na
anakwenda mahari popote atakopotumwa.
1 Timotheo 2:7 "Nami kwa ajili ya huo naliwekwa
niwe muhubiri na mtume, ( nasema kweli, sisemi
uongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli".
2 Timitheo 1:11 "Ambayo kwa ajili ya hiyo
naliwekwa niwe muhubiri na mtume na mwalimu."

B) Awe na Huduma tano.
>Utume .Kwenda polite.
>Unabii. Kupata taarifa kwa Mungu.
>Uinjilsti.Kuvua kondoo.
>Uchungaji. Uwezo wa kulea kondoo.
>Ualimu. Kufundisha.

C) Awe na uwezo wa kuongoza.
D) Awe na kiu name uwezo wa kuujenga na
kuukuza mwili wa Krsto.

E) Uwezo wa kusimamia mafundisho sahihi ya
Kristo.

F) Awe na Huduma ya wazi kwa watu wote.
(iambatane na ishara na miujiza na maneno ya
unabii)

G) Awe mwalimu.
KAZI ZA MITUME KATIKA MWILI
WA KRISTO.

Fuatana nami katika somo lijalo nawe utabarikiwa.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA YA KUFA
NI HUKUMU. (Waebrania 9:27.)

MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments