KILA ATAKAYESIKIA HABARI YA MAISHA YANGU ATACHEKA PAMOJA NAMI-

Na Mchungaji Bryson Lema, Ufufuo na uzima Morogoro.
Utangulizi:  Imeandikwa katika MWANZO 21:6-7….[ Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. 7 Akasema, N'nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.]
Sara akasema kila asikiaye atacheka pamoja naye. Ni kweli kila atakayesikia habari ya maisha yangu atacheka pamoja nami. Sara aliishi na Ibrahim miaka mingi pasipo kupata mtoto, akapewa jina tasa. Sara akakata tum aini la kupata mtoto maana aliisha kuwa mzee. Ikambidi ampe mume wake mjakazi ili amzalie mwana, naye Ibrahimu akapata mtoto aitwae Ishmaili. Lakini Sara alijua mtoto huyo atakuwa furaha yake lakini ikawa kinyume kwani yule mjakazi alimcheka Sara kuwa hana mtoto. Lakini Sara alivumilia mbele za Mungu na akiwa na miaka 90 ndipo aliweza kupata mtoto wakati akiwa hana wazo hilo tena na alikuwa haombi tena kwa ajili ya mtoto.
Tatizo ulilonalo ni dogo sana mbele za Mungu, tunaona Sara akiwa mzee Bwana alimwambia ni saa yako ya kupata mtoto. Inawezekana umedharaulika na kudhihakiwa na hata kukata tamaa na muda umepita wala huoni majibu, lakini hii ni saa yako ya Bwana kukutana na wewe na watu wote watacheka nawe na kufurahi nawe kila watakaposikia habari ya maisha yako. Baada ya muda mchache wanaokudhihaki watakaposikia habari ya maisha yako watacheka nawe. Lazima ujue ng’ambo ya tatizo hilo kuna kicheko. Sara alipopata mtoto dharau yote aliyokuwa anadharauliwa iliisha naye alipata nguvu tena akiwa kikongwe. Hata nawe leo ipo saa yako ya kuinuka tena, maana hata kuja duniani ilikuwepo saa kwa ajili yako ya kuja duniani. Walimzoea Sara ni mtu wakulialia lakini alipokuwa mzee na kupata mtoto alianza kucheka. Musa alipokuwa akiishi kwa Farao Mungu hakusema naye, bali alisema naye akiwa kwenye kichaka. Tunaona kumbe mfalme wako hawezi kusema nawe lakini Yesu anaweza kusema nawe. Yesu  akasema maneno ya mwisho ya kwamba, nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi nami naenda kuwaandalia makao, ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Je! ni binadamu gani ambaye angeweza kukuruhusu ukae kwenye nyumba ya baba yake? Lakini Yesu anasema alipokwenye ushindi nawe uwe na ushindi. Tunaona Yesu alizaliwa kwenye holi la ng’ombe kila eneo Mariamu mamaye alipoenda kuomba kujihifadhi alikataliwa. Hivyo Yesu yeye ni Baba kwa wale waliokataliwa maana hata yeye alikataliwa. Ikifika saa ya Bwana lazima utapita tu hakuna atakaye kuzuia.
Mungu tunaye mwabudu yeye huwa anapita mahali pa wenye shida na ndio maana anasema, njooni kwangu ninyi nyote mnaolemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Kanisani ni mahali pa kutua mizigo na kupumzika. Usiangalie tatizo lako ni kubwa kiasi gani au limekaa muda gani. Je! ni jambo gani lililo gumu mbele za Mungu? HALIPO. Ndio maana Mungu amesema njoo tuhojiane, eleza shida yako, upate haki yako. Mungu anaangalia unaongea nini , unavyoongea Mungu anaweza kubalidilsha taarifa uliyonayo. Taarifa ya Mungu huwa haibadiliki hata siku moja, lakini taarifa ya binadamu inaweza kubadilika maana mwanadamu akikuahadi kitu anaweza asikupe ile ahadi. Lakini Mungu akisema amesema habadiliki. Weka msingi wako kwa Yesu Kristo, maana yeye ni jana,leo na hata milele. Haijalishi nani amesema kuhusu maisha yako, bali ujue alichokianzisha Yesu ndani yako yeye anakikamilisha. Lakini Mungu anasema kila atakaye sikia habari ya maisha yako atacheka, maana Bwana atakuinua tena. Ndio maana taarifa ya Sara ikaandikwa kwenye biblia kwa ajili yako ili ukisoma Mungu akusidie tena. Hivyo kila atakaye sikia habari ya maisha yako atacheka pamoja nawe, maana watasema hakika yupo Mungu amekusaidia na kukuinua. Maana Mungu amesema hakika nitakupigania, kukuinua na kukusimamisha tena.
Kanisa ni kiwanda, hivyo wanavyokuona hivyo wajue upo kiwandani kutengenezwa, kutengenezwa sura, afya n.k. Na mwenye kiwanda mwenyewe ni Mungu naye anawarekebisha watu wawe sawa. Wao wamejipanga ili wakuangamize lakini wasichokijua ni kuwa unaye Mungu mkuu kuliko miungu yote. Wameiweka afya yako msalabani wakakuona kama umekufa, wamekuchimbia shimo. Mungu tunayemtumikia huwa hazuiliwi na mauti na kifo. Lakini Yeye ni zaidi ya kifo, mauti na vita waliyoinua juu yako. Na zaidi atakufundisha kupigana vita. Huyo adui aliyesimama mbele yako hatakuangamiza na wala asikutishe, lakini yeye huyo huyo atacheka pamoja nawe. Wote wanaokucheka, na kukudharau hao hao watasema hakika Mungu amekusaidia. Wao wamejipanga ili wakuzuie, uangamie,upotee na wana subiria saa chache ufe, lakini wasichokijua saa yako bado, kwani Mungu naye amejipanga ili ucheke. Inatakiwa ufurahie adui anapoinuka juu yako, maana Yuda alivyoinuka juu ya Yesu alisababisha Yesu ainuliwe msalabani na kupata ushidi, hivyo adui yako ndiye anayekupeleka kwenye ushindi wako.
Nabii Isaya akasema tumepewa mtoto mwanaume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake. Na tulichopewa kimejitosheleza, ukimwita mfalme anakuwa mfalme, ukimwita askari anakuwa askari na kutoa silaha za vita,hivyo kwa jinsi unavyomwita ndivyo atakavyokuwa kwako. Mkamate Yesu Kristo, kwani unachokitafuta tumeishapewa tayari. Ndio maana Mungu akaona amtume Yesu kuja duniani maana alijua akimtuma wenye shida wataondolewa shida zao.Haijalishi amekaa nani mbele yako lakini ninacho kijua ipo siku ya furaha inakuja. Ni saa yako kuvaa vazi jipya. Wao wamekaa vikao ili ufukuzwe kazi lakini wasichokijua wanampiga chura teke ili asogee na kumwongozea safari, jaribu hilo lipo ili kukuvusha ng’ambo na kukuongezea safari ili uvae vazi jipya na ucheke. Ni saa yako kuingia kwenye ushindi uliousubiria muda mrefu. Bwana aliweka siku za kufurahi, ndio maana Daudi alisema usifurahi ndugu yangu ninapoanguka maana nitainuka tena.
Pamoja na matatizo uliyo nayo utaingia kwenye ushindi, hivyo ni lazima uweke msingi juu ya jiwe ambaye ni Yesu Kristo, kama Sara alicheka nawe utacheka. Adui zako wanao kutukana watakuinamia tena, kama Yusufu, ndugu zake walivyomwinamia.Walimwondoa Yesu kwa siku tatu tu, hawakumwangamiza milele, ila siku ya nne walimwona tena Galilaya. Naye Yesu alisambaa juu ya wanafunzi wake wote nao wakasema kama Yesu baada ya siku ile ya nne. Wanaokuzuia kwenye biashara yako waaambie wakikuzuia ndipo unapoanzisha tena biashara nyingine.Unapofukuzwa kazini ndio saa ya kuanziasha kampuni yako, kero za upangaji wa nyumba zinapokupata ndio zinakufanya ujenge nyumba yako tena.
Lile tatizo ulilo nalo ndilo limekufanya uje kanisani, usichokijua Shetani ni mtumishi wa Mungu mzuri sana, maana bila lile tatizo usingemtafuta Mungu, hivyo shetani anamtumikia Mungu bila yeye kujua na kukufanya uchimbe sana kwenye mwamba. Mjenzi anayechimba  sana ujue anajenga jengo refu sana. Nasi leo tunachimba sana na kusimamisha nguzo pale tunapoukuta mwamba. Na maadui walipouona mnara juu walichimba kuuondoa lakini wasichokijua tumejenga nguzo yetu juu ya mwamba. Na wsichokijua kadri unavyooupiga mwamba ndivyo unavyoongezeka maana kwa jinsi hiyo ndivyo kanisa lilivyozidi kuongezeka na kukua zaidi.Unapopigwa vita usifikiri ndio unaondoka, bali ujue vita inaongeza nguvu ya kushida maana kila kilichozaliwa na Mungu kinaushinda ulimwengu. Vita inakupa kutawala zaidi. Tunapovianza vita tuna vianza kama washidi, yaani ni washindi tayari, hivyo waambie wanaofanya vita nawe kuwa utafika pale unapotaka kufika, na saa yako ikifika utacheka. Vita ni mtihani wa kuingia ng’ambo ya pili na kuvaa sura mpya.
GALATIA 4:4-…[Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.]
Tuaona hata Yesu alikuja ilipotimia saa,Yesu akazaliwa. Hivyo nawe saa yako imetimia tena kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
ZABURI 126:1-6 …,[Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.4 Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.]
Ni kama unayeota ndoto, huelewi mchungaji anahubiri nini, lakini ni saa yako ya kuvaa vazi jipya. Sara aliitwa tasa kwa miaka mingi lakini siku moja ilibadisha na kuitwa mama wa mataifa. Ndani ya mzoga ilitoka asali, unoonekana kama usiyefaa lakini ndani yako kuna shangwe ya vigerere na ushindi unatoka ndani yako, ndani ya masaa machache, maana wapo watakaoenda kucheka na wewe wale walikuona haufai nao watamtukauza Mungu kwa ajili yako.

Comments