AGENDA YA UFALME

Na Askofu Dr Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

Neno ‘Ufalme’ limeandikwa ndani ya Biblia mara 321 na neno ‘Mfalme’ limeandikwa mara 1913. Kwenye Biblia.
Imeandikwa kwa vinywa vya mashaidi wawili au watatu neno linahesabika na ndiomaana Yesu alitengenezewa mashahidi wa uongo ili auwawe, Naboth pia alitengenezwa mashahidi wa uongo.
Warumi 1
Neno la Biblia linapotajwa mara nyingi linakuwa lina uzito uliofichika ndio maana farao aliota ndoto ya masuke na ngombe na hakuelewa maana yake ni nini lakini Mungu alimpa Yusufu uwezo wa kumtafsiria farao ile ndoto na kusema kwavile neno hili limekuja mara mbili maana yake limethibitika/ni halisi. Neno Ufalme na Mfalme limeandikwa mara nyingi kwenye biblia na limethibitika.
Yesu alipokuja duniani haja kuhubiri habari ya mafanikio na uponyaji bali alikuja kuhubiri ujumbe wa Ufalme wa Mbinguni.
Ukiwa ndani ya Ufalme wa mbinguni hauhitaji kuomba mafanikio yaje bali mafanikio yapo ndani ya Ufalme. Sheria ya Ufalme inasema “tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki zake na hayo mengine mtakuwa nayo. Neno Ufalme lililokuwa linatumika zamani ambalo sasa hivi linaitwa Nchi, kwa maana nyingine Yesu anasema tafuteni kwanza nchi na haki zake na hayo mengine mtaongezewa.
Watu wengi wameingia kwenye wokovu wakidhani watapata maisha mazuri lakini hawapati, wengine wanadahani wakiolewa ndani ya wokovu watapata raha kwenye ndoa lakini hawayapati tatizo ni ule mtazamo walio nao kuhusu wokovu bila kujua kuna Ufalme wa Mungu ambao una sheria zake na katiba yake na kanuni zake za kuishi ndani yake ukafurahia maisha.
Biblia ilikuwepo kabla ya madhehebu na makanisa hayajakuwepo, Biblia sio kitabu cha Dini, Tamaduni, Historia au Hadithi bali Biblia ni kitabu kinachohusu mambo haya:-
1. Biblia ni kitabu kinachohusu Ufalme.
2. Biblia ni kitabu kunachohusu Mfalme(Yesu) kwasababu huwezi kuwa na Ufalme bila ya kuwa na Mfalme anayetawala.

3. Biblia ni inahusu familia ya Mfalme au Raia wa Ufalme.
4. Ni kitabu kinacho husu serikali ya kifalme Isaya 9:6
5. Biblia ni katiba ya Ufalme Katiba ni sheria mama ya nchi na kwenye ufalme wa Mbinguni katiba yake ni Biblia.

6. Biblia inahusu uchumi wa ufalme. Kuna namna ya kupata pesa ndani ya Ufalme, kufanya Biashara, kufanikiwa ndani ya Ufalme, kuoa na kuolewa, kuongea na kuishi ndani ya ufalme.
7. Biblia ni kitabu kinacho husu funguo za Ufalme. Yesu alisema yeye ndiye mlango wa kuingia ndani ya Ufalme. Ukiingia ndani ya Ufalme utakutana na funguo nyingi sana za ufalme ambapo funguo hizo ni zile ahadi za Mungu zaidi ya 36,000 kwenye Biblia. Unatakiwa ujue ufunguo wa, uchumba, shule, mafanikio, uongozi utajiri ni upi, kuna funguo nyingi za ufalme lakini tatizo unakuta mtu anajaribisha ufunguo wa kusafiri lakini haufungui mlango, anajaribisha funguo wa kusoma haufungui, kwenda kanisani, kuolewa haifungui, kuwa mpole haifungui, kuwa mkali haifungui lakini kwenda mbinguni mtu huyo ataenda lakini akiwa bado yupo sebuleni hajafanikiwa kufungua hata mlango mmoja wa mafanikio ndani ya Ufalme. Mungu ameamua kuwafundisha watu kwamba anayetaka kufungua biashara funguo zipo, anayetaka kuolewa/kuoa funguo zipo ndani ya ufalme, anayetaka safari za kwenda nje ya nchi funguo zipo ndani ya Ufalme zimekaa pale ndio maana Yesu anasema tafuteni kwanza Ufalme wa Mbinguni na mengine yote mtazidishiwa.
8. Biblia ni kitabu kincho husu Agano yaani makubaliano ndiomaana imeagawanyika sehemu kuu mbili ambazo ni agano la kale na agano jipya.
9. Biblia ni mkataba.
10. Biblia inahusu sheria ya Ufalme ndiomaana Yesu alisema msifikiri amekuja kuiondoa sheria bali kuitimiza torati.

11. Biblia ni mila ya Ufalme. Kwa wanyakyusa wakiwa wanasalimiana au mbunge akienda kuomba jimbo lazima apige magoti na kunaa chini ndipo aongee na asipofanya hivyo mila hiyo haumo ndani ya Utamaduni wao, kwa wasukuma ukiwa unasalimia unapiga magoti maana yake ni mila ya ufalme na kwenye ufalme wa Mbinguni huwezi kufanikiwa au kutambulika kama raia wa Ufalme bila ya kufanya mila na tamaduni za ufalme wake.
12. Biblia inahusu raia wa Ufalme. Ufalme huu una raia wake
“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo” Wafilipi 3:20.
Biblia inahusu Ufalme na imekosewa sana kuitwa kitabu cha kikristo kwamaana ukristo hauna nguvu yeyote.

“Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.” Luka 16:16
Neno habari njema linaitwa injili. Neno torati maana yake ni sheria na kwenye Biblia torati ni vile vitabu vitano vya mwanzoni mwa Biblia na ndivyo vinaitwa sheria. Baada ya torati wanakuja akina Joshua na Ruth ambao ni waamuzi, baadaye wanakuja wafalme na Kutokea samweli mpaka malaki ni zimeandikwa habari za manabii, ndiomaana Yesu anasema torati na manabii zilikuwepo tangu enzi za manabii mpaka Yohana lakini kuanzia Yohana kwenda mbele ni habari nzuri zinazohusu Ufalme. Yesu anasema katika manabii wote hakuna manabii wakubwa kuliko nabii Yohana. Anaitwa mkuu kwasababu kuanzia kwenye torati kuja mpaka manabii yeye ndiye anayefunga habari za manabii. Yohana alikuwa anasema tengenezeni njia ya Ufalme na palipo pindapinda patanyooshwa tubuni kwamaana ufalme wa mbinguni umekuja.
“Neno tubuni kwa kigiriki maana yake ni badilisha mtazamo. Unapokuwa unasoma Biblia ya kiingereza na Kiswahili kuna baadhi ya maneno hayaeleweki yametafsiriwa ndivyosivyo na ukiamua kuangalia kwa lugha ya kigiriki unakuta maana yake ni badilisha nia au namna ya kufikiri au geuka”
Kwenye torati ujio wa ufalme ulitabiriwa kwa mfano wa nyoka wa shaba baadaye manabii wakawa wanasema kuna mfalme anakuja na kwa Yohana mbatizaji naye akasema kuna mfalme anakuja na akamwona na kumtambulisha kuwa yeye ndiye mfalme wa haki, Biblia inasema wafalme wengi na manabii walitamani kumwona Yesu mfalme atakaye Kuja katika dunia.
Ukiwa ndani ya Ufalme hauwezi kupatwa na shida na sisi ni gosheni katika nchi kwamaana hakuna mabaya yatakayotupata, wakati uchumi wa dunia unayumba sisi tunajenga nyumba, wakati magonjwa yanavamia nchi sisi hayatatupata kwamaana tupo ndani ya Ufalme.

Yesu alipoanza kazi alienda mlimani.
“Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana. Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope.” Mathayo17:3 – 7
Musa na Eliya walimtokea Yesu na kuzungumza naye kwasababu Musa alikuwa mwakilishi wa torati yote na Eliya alikuwa mwakilishi wa manabii wote na walikuja kukabidi kila kitu Yesu kwaajili ya Ufalme, wanafunzi wa Yesu waliamka na kuyaona hayo yote yakitendeka na kukimbilia pale maana walijua ndio wakubwa kwenye Israeli lakini Mungu Baba wa mbinguni aliamua kuongea kwa sauti na kuwathibitishia kuwa Yesu ndiye mwanaye mpendwa anayependezwa naye wamsikilize yeye.
Neno mwana wa Mungu maana yake ni wewe ni Mungu “aliyezaliwa anafanana na aliyemzaa” Yesu alikuja duniani ili ufalme uliopo mbinguni aulete duniani na sisi tuwe raia wa ufalme wa Mungu ndio maana tunaitwa wana wa Mungu na Yesu ni kaka yetu mkubwa.
Mathayo 6:1 - 13
Basin ninyi mkisali salini hivi:- Baba yetu uliye mbinguni Ufalme wako uje duniani na mapenzi yako yaje na utakalo lifanyike duniani kama mbinguni maana yake lolote litakalofanyika mbinguni lifanyike na hapa kwenye Ufalme wa duniani.
“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” Yohana 4:24

Mungu ni roho na ndiye ametuzaa na makazi yake ni mbinguni.
“Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.” Mathayo 6:29 -33
Yesu amesema ingieni ndani ya Ufalme kwamaana humo ndani ya ufalme kuna haki za ufalme zipo humo ndani mtazipata ndiomaana alisema tafuteni kwanza Ufalme wa mbinguni na hayo mengine mtazidishiwa yaani tusijisumbue tutakula nini au kuvaa nini bali tutafute kwanza ufalme wa mbinguni hayo mengine yapatikana.
“Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.” 1Wakorintho 4:20
Kwenye Ufalme wa Mungu si kwasababu ya neno bali kwaajili ya nguvu za Mungu, nguvu za Mungu hazijengwi kwenye hekima ya wanadamu bali ni kwa Uweza wa Mungu utokau juu mbinguni.
NAMNA YA KUINGIA KWENYE UFALME.
Kwenye Ufalme wa Mungu kuna wahamiaji haramu ambao sio wa kuzaliwa "Warumi 10:9" Kuokoka ni kuingia kwenye Ufalme wa mbinguni na kumkiri Yesu kwa kinywa chako mwenyewe. Kuna watu wanahamia kwenye Ufalme kwasababu zao wenyewe lakini huwa hawafiki mwisho.
Ukielewa siri ya Ufalme kila andiko utakalolisoma utaelewa maana yake.
Yohana 3
Kuzaliwa mara ya pili maana yake ni kuingia kwenye nchi iliyokuja hapa duniani ili uwe raia wa nchi hiyo na upate uraia wa kuishi humo kwa kumkiri Bwana Yesu kwa kinywa chako.
Ukiingia kwenye ufalme maana yake Yule mfalme anayemiliki ufalme huo unakubali akumiliki kwasababu yeye ni Mfalme, kuna mambo mengine huwezi kuyaomba kwasababu una mmiliki ndani ya Ufalme anayekupatia.
UKIRI
“Yesu ni Bwana wa maisha yangu, Yesu ni mmiliki wa maisha yangu”

Ukiingia kwenye Ufalme wa mbinguni unaanza kushika sheria za ufalme huu, unaanza kushika katiba ya ufalme huo, Ndani ya Ufalme huo kuna askari wake ambao wanawakamata wale wanaofanya mambo kinyume cha ufalme. Uweza ukamkuta mtu anapatwa na magonjwa, mikosi, balaa na yuko ndani ya Ufalme ukichunguza unakuta amekwenda kinyume cha sheria za Ufalme ndipo akakamatwa na askari wa Ufalme, kwenye Ufalme hairuhusiwi kuzini kabla ya ndoa na ukizini kuna askari wanakukamata, kwenye Ufalme huu ukishika sheria zake unaitwa mtakatifu, kwenye ufalme huu ukitoa kodi milango ya fedha inafunguka.
“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Mathayo24:1 - 14
Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ukiingia mahali unabadilisha sehemu hiyo na tamaduni zake zote na kupanda na kueneza utamaduni wake.
Kwenye neno hili la yatupasa kuingia mbinguni kwa dhiki nyingi watu wanalitafsiri kwamba unapotaka kuingia mbinguni lazima uhangaike mpaka siku ya mwisho ufe uingie mbinguni kitu ambacho sio ukweli bali ukweli ni kwamba unapotaka kuingia kwenye Ufalme utapatwa na matatizo na kupoteza baadhi ya vitu, marafiki na hata ukatengwa na familia kwasababu tu umeokoka na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni lakini Yesu alituhakikishia Yule atakayevumilia mpaka mwisho atazidishiwa zaidi ya vile alivyovipoteza.
Utambulisho wako kwamba wewe ni nani ndio utakaokupa utiisho. Mashetani hayawezi kukugusa kama ukijitambulisha kama mwana wa Ufalme wa mbinguni au mtu wa mbinguni lakini ukijitambulisha kama mkristo mashetani walishakuwepo mbinguni na wanajua mkristo hana tatizo mbele yao lakini mwana wa Ufalme maana yake ni mtu aliye ndani ya Ufalme ambaye anaishi chini ya Mfalme huyo lazima wamwogope kwasababu anafanana na Mfalme wake.
“Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.” 1Yohana3:10
Siri ya Nguvu za Ufalme.
Ufalme ni wake na nguvu ni zake na Utukufu ni wake leo na hata milele na sisi tumeingia ndani ya Ufalme huo. Yesu anaitwa Mzaliwa wa kwanza. Unaposema mzaliwa wa kwanza maana yake lazima awepo mzaliwa wa pili. Yesu alianza kuwa mwana wa Mungu na sisi tukafuata na Biblia inasema Yesu ni kaka yetu mkubwa anamwita Mungu Baba na sisi tunamwita Mungu Baba. Tunamilikiwa ndani ya ufalme na Yesu kristo.
Ukiri:
Yesu anafanana na mimi kwa vitu vyote Yesu ana kaa ndani yangu na mimi ndani yake, Mungu yu ndani ya Yesu na Yesu yu ndani yake na maana yake mimi ni mashine ya kutafuna maovu hapa duniani, wewe ni Mungu mdogo hapa duniani na nikisema kitu Mungu wa Mbinguni amesema mimi ni mmiliki halali juu ya nchi. Amen

Wakolosai 1:15, Mwanzo 1:16,
Ufunuo wa Yohana 5: 9 – 10
Wakolosai 2:12

Comments