WACHUNGAJI WAMIMINIKA KATIKA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MTUME JOHN kOMANYA.

Marehemu Mtume John Komanya enzi za uhai wake na hapa akiwa na mke wake.
Jana jumatano ndiyo ilikuwa siku ya mazishi ya Mwanzilishi wa huduma ya Cathedral of Joy Mtume John Komanya. Mtumishi wa MUNGU John Komanya alifariki jumapili iliyopita,  alifariki asubuhi ya siku hiyo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikua akitibiwa matatizo ya kiafya yaliyokua yakimsumbua.
 Imekuwa ni simanzi kwa watu wengi na ni pigo kwa wana injili lakini kazi alyopewa na MUNGU ameimaliza na ndio maana MUNGU amemchukua.
Katika ibada ya kuuaga mwili wa apostle Komanya kanisani kwake watumishi wengi wa MUNGU walihudhuria na kuungana na familia ya marehemu pamoja na kanisa kwa ujumla. Baada ya kuagwa kwa Mwili Kanisani ilianza safari ya kwenda kuuweka mwili wa mtumishi huyo wa MUNGU katika Nyumba ya milele.
BWANA alitoa na BWANA  Alitwaa hivyo siku zote jina la BWANA lihimidiwe.
Zifuatazo ni baadhi tu ya habari picha katika tukio hilo. 
Mzee wa upako Mchungaji Anton Lusekelo akisema neno kanisani hapo..
Mtume Peter Rashid akiwasili kanisani hapo.
Wafiwa katika huzuni kubwa.
Mtume Peter Nyaga na Mtume Peter Rashid Abubakar pamoja na Apostle Mwingreza.
Mtume Peter Abubakar akisalimia na Pembeni ni Askofu Emmanuel Mwasota.

Mchungaji Mwansasu alikuwepo pia.
 
 
baadhi ya watumishi katika hali ya huzuni.

 

Askofu Dastan Maboya akihubiri wakati wa ibada ya  kuuaga mwili kanisani.

Mtumishi wa MUNGU Dastan Maboya akihubiri

Mchungaji Anton Lusekelo akiomba.

Mchungaji Lusekelo akifuatilia kinachoendelea.

 =Baada ya kuuaga mwili kanisani yalifuata mazishi.


BWANA alitoa na BWANA  ametwaa jina la BWANA libarikiwe milele. 

Comments