DHAMBI HUWATENGA WANADAMU NA MUNGU MUUMBA WAO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU la uzima.
Ni heri wewe kama utalitii Neno la MUNGU.
Leo tunaichambua dhambi na madhara yake.
jambo la kwanza kujua ni kwamba Dhambi Humtenga Mtu Na MUNGU.
Isaya 59:2'' lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. ''. 
Ndugu,Ukikubali Kujitenga Na MUNGU Muumbaji Wako Kwa Sababu Ya Dhambi, Chunga Maana Usipotubu Utatengwa Na MUNGU Milele Kwa Wewe Kuwa Jehanamu Huku Wateule Wa KRISTO Wako Mbinguni.
Lakini nafasi ya kutubu bado ipo hivyo itumie. Tunao muda mchache wa kusahihisha njia zetu na kubadilika kabisa kutoka kuitwa waovu na kuanza kuitwa watakatifu kama tu tukiamua kutubu na kuacha dhambi.
1 Yohana 1:9 ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. ''

Dhambi ndio kitu cha kwanza ambacho kinakufanya wewe uwe mbali na MUNGU.
dhambi ya Adamu imetuathiri wanadamu wote. 

Warumi 5:12 ''  Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; ''

Jambo Lingine la muhimu kujua kuhusu dhambi ni kwamba  Roho Itendayo Dhambi Ndio Itakayokufa Maana Yake Ndio Itakayokwenda Jehanamu.

Ezekieli 18:20 '' Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. ''

 Dhambi Haitakiwi Kuwatawala Wanadamu. 
Tatizo Kubwa La Wanadamu Ukiwahubiria Waache Dhambi Wanakuona Kama Umeleta Dini Mpya Kumbe Wewe Ndio Umelisimamia Kusudi La MUNGU. 
Ona mfano huu ambapo mfalme wa Israel alimwasi MUNGU. Neno la MUNGU lilimfuata likisema

 '' Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.-1 Samweli 15:23 ''  

-Dhambi inaweza hata ikasababisha ukaondolewa katika huduma yako.
-Dhambi inaweza ikakuondoa katika mpango wa MUNGU.

-Ukilikataa Neno La BWANA YESU Na Yeye Siku Ile Atakukataa. -Ukiukataa Uzima Usitarajie Kupelekwa Uzimani Kwa Nguvu Bali Utaenda Katika Njia Ya Jehanamu Uliyoichagua. 

Jambo jingine muhimu kujua kuhusu dhambi ni kwamba Dhambi Huzaa Mauti Yaani Dhambi Huzaa Jehanamu.

Yakobo 1:15-16 '' Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. '' 

Ndugu yangu,Kwa Unyenyekevu Mkubwa Nakuonya Uache Dhambi, Nakuomba Umpokee BWANA YESU Ili Upate Uzima. Kumbuka Afuataye Dhambi Hufuata Jehanamu .

Mithali 11:19 '' Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. '' 

 -Dhambi ni mbaya na dhambi huwapeleka watu jehanamu.
-Kama kuna kitu mwanadamu anatakiwa akiogope basi ni dhambi. na dhambi mbaya zaidi ni kumkataa YESU na kukataa kuongozwa na Biblia.
-Ndugu yangu, nakusihi kuanzia leo kataa dhambi zote na uanze kuishi maisha matakatifu.

Je Nimebakiza Nini Katika Kukuambia? 
Nimebakiza Moja, Ishi Maisha Ya Wokovu Matakatifu Siku Zote.
 Warumi 6:23 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.''  

-Ndugu,Naamini umejifunza na utachukua hatua
njema ya kumpokea BWANA YESU kama
hujaokoka ili awe BWANA na MWOKOZI wako
tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu.



KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO
HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO
UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA
MATAKATIFU.


''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele
zako mimi mwenye dhambi, lakini leo
nimetambua kosa langu na naomba unisamehe
dhambi zangu zote, nisamehe dhambi
ninazozikumbuka na pia zile ambazo
sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha
hukumu na uliandike jina langu katika kitabu
cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10
Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa
sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya
kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu
'' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na
hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na
hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga
ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa
matendo mema na matakatifu. BWANA nipe
ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda
dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo
mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU
mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila
roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa
jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU
linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza
mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana
kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea
na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU
kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO
nimeomba na kupokea .
Amen.''


Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe
kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa. Kwa sasa
naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza
tena siku nyingine. ulishindwa kumpokea
BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa
kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima
na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho
kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende
uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments