JITIE MOYO MWENYEWE KAMA HAKUNA WA KUKUTIA MOYO.



BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Majaribu  yapo na yatupasa tuyashinde.
Magumu wakati mwingine huja lakini kuwategemea wanadamu huleta mtego.
Wakati mwingine kama hakuna mtu wa kukutia moyo katika magumu unayopitia hakikisha unajitia moyo mwenyewe.

Kuna watu hata hulalamika kwanini humtii moyo katika jaribu lake.
Ni vizuri kutiwa moyo na wapendwa wako lakini wakati ukiona hakuna wa kukutia moyo hakikisha unajitia moyo mwenyewe maadamu unaishi maisha matakatifu na mngoje BWANA.

Ngoja nikupe mfano mmoja wa mtu aliyekuwa katika magumu ndani ya Biblia.

Ayubu alikuwa na marafiki, na alitarajia marafiki zake wakija basi watamtia moyo lakini ilikuwa tofauti. Kuna wakati Ayubu katika magumu yake alitarajia mkewe ndie angemtia moyo na kumfariji lakini hata mke naye aligeuka na kumwambia amkufuru tu MUNGU ili afe. jiulize hapo ''Yaana anayetakiwa kukutia moyo ndio huyo sasa anataka ufe?''

Ndugu, inawezekana kabisa unapitia magumu na unatarajia sana wapendwa wako wakutie moyo, kama ukiona kimya nakuomba jitie moyo mwenyewe maadamu tu uko katika kweli ya MUNGU.
Ayubu ni mfano mzuri na ninampenda sana maana jaribu lake linatufundisha kitu muhimu sana.
Ayubu alijitia moyo mwenyewe na kusema anauhakika MUNGU atamshindia tu.
Ayubu 19:25-27 ''Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona MUNGU; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu. ''
 Ayubu alibaki na BWANA  maana alijua wanadamu hawako upande wake.
Kazi ya wanadamu na marafiki kwenye jaribu la Ayubu ilikuwa ni kumsimanga, kumcheka, kumlaumu na kumtuhumu kwamba amefanya dhambi.
Ayubu 19:2-5 '' Je! Mtanichukiza nafsi yangu hata lini, Na kunivunja-vunja kwa maneno? Mara kumi hizi mmenishutumu; Hamwoni haya kunifanyia mambo magumu. Ingawaje nimekosa, Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe.Kwamba mtajitukuza juu yangu, Na kunena juu yangu shutumu langu;''
-Huu ni mfano wa watu wanaopitia katika magumu.
Kuna familia kila mwaka wanazika lakini ukiwauliza majirani watasema kwamba hiyo ni laana inawatafuna kumbe ni uongo.
Kuna binti kila akitaka kuchumbiwa anaachwa, ukiwauliza wapendwa wake utasikia mara hiki mara kile. mara nyingi ni uongo.
Yohana 16"33 '' Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. ''
Ndugu unayepitia magumu, nakuomba omba sana na vumilia.
Kesho yako haitakuwa kama leo yako kama tu hiyo kesho ukiikabidhi kwa BWANA YESU.
Dunia inakwenda kasi sana, kuna waliokuwa na kazi nzuri muda mfupi tu uliopita lakini sasa hawana. Ni vyema kukabidhi kwa YESU kazi yako, kipato chako na familia yako lakini pia yakija magumu nakuomba jifunze kuomba na kumshirikisha BWANA YESU ili akushindie.
 Mthayo 5:8 ''Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU''
Kama kuna leo basi na kesho ipo.
Kama leo imejaa miba inayochoma kwako, kesho yako inaweza kuwa na shangwe ya kudumu kama tu BWANA YESU utamshirikisha katika maombi yako.
Wakati wa dhoruba vumilia na omba sana.
BWANA YESU bado ana ushindi wako na ukivumilia ushindi huo utakuwa dhahiri kwako.
ona mfano huu.
Mathayo 9:2 '' Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye YESU, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.''
Jipe moyo mwenyewe kama hakuna wa kukutia moyo.
Dumisha utakatifu na hakikisha jaribu lako halikuondoi katika wokovu wa BWANA YESU.
Una heri wewe uliyeokoka na unamtegemea MUNGU.
Ubarikiwe  sana na hakikisha Vazi lako la Wokovu wa KRISTO halichafuliwi na chochote.
-Shika Wokovu Asije Mtu Akakunyang'anya.
-Hata Kama Utadharaulika Lakini Mtii BWANA
YESU Na Usimwache Hata Kidogo.
Kumb 6:5 '' Nawe mpende BWANA, MUNGU
wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa nguvu zako zote. ''

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana
. Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments