ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA!.( 3)

Na Mwl Nickson Mabena

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri...
Natumia nafasi hii kukukaribisha kwenye muendelezo was Somo hili ambalo Roho Mtakatifu ameweka msukumo ndani yangu ili tujifunze pamoja...
Kutokana na utangulizi nilioutoa kwenye Sehemu ya kwanza ya Somo hili, Somo lina vipengele nane, na tayari vipengele vitano nimeshavimaliza na sasa tupo kipengele cha Sita..
6.SADAKA ZITOLEWAZO KWENYE UFALME WA GIZA!.
a)DAMU
Nilikwambia ya kwamba Damu inapomwagiga hua in a to a Sauti, tukaangalia Maandiko kadhaa kuhusu hili...
Pia nilikwambia kwamba IPO Damu inayonena Mema, pia IPO inayonena Mabaya!.
Biblia Katika kitabu cha Waebrania Sura ya Kumi na Mbili, mstari wa 24, inasema
"na Yesu mjumbe wa agano jipya, na Damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili".
Damu ya Yesu siku zote inanena Mema, inanena Uzima...
Usisahau tulipotoka, Siku zote Kaa ukijua kwamba Shetani Hana Damu, kwa hiyo hutumia Damu ya Viumbe vya Mungu kufanyia Mambo yake ya kiagano!.
Mtu unapoenda kwa mganga wa kienyeji, mganga anapokwambia kwamba Umpelekee kuku usidhani ya kwamba Mganga Ana shida ya Nyama, Shida yake kubwa ni Damu.. Maana Damu ndiyo inauwezo wa kunena badala yako...
Sasa Mganga ili kuongeza Mbwembwe, anaweza kukwambia Nyama tuchemshe kisha unywe Mchuzi wake, lakini haina matokeo yoyote Kiroho!!.
Damu inayomwagika kwenye madhabahu yake, ndiyo inayovuta nguvu za Giza zinazokuja kukusaidia.
Pia, sio Damu ya wanyama tu, hata Damu ya mtu inaweza kutumika, hapa ndipo linapokuja suala la utoaji wa kafara..

Inatengenezwa Ajali, kisha Damu inamwagika, nguvu za Giza zinakua nyingi sana ili kuingia agano na huyo mtu anayetaka msaada.
Kafara sio lazima ajali isababishwe, Bali hata wengine huwatoa Ndugu zao kafara!,
Soma hapa,
"Naye Mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia Saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; Basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe." 2Falme 3:26-27.

Mfalme aliamua kumtoa kafara Mtoto wake wa kwanza..
Katika Dunia ya Leo, inaweza ukayatamani mafanikio ya MTU flani, kumbe mwenzako ametoa kafara ndio amezipata hizo Mali. Wewe usione Magari mengi tu unapishana mayo alafu wewe unayatamani, na wala hujui siri ya mafanikio yao!, Hata maduka unayoyaona, wengine wameyapata kwa kumwaga Damu za wanyama, pia hata ndugu zao!!!.
Watu wanashauku kubwa ya kufanikiwa kwa haraka, ndiyo maana wengi hukimbilia kwa waganga kutafuta misaada!!.
Namshangaa Sana mtu amefungwa na nguvu za Giza, mapepo yanamsumbua alafu anaenda kwa Mganga wa kienyeji kutafuta Msaada!.
Kwa Mganga hakuna Msaada, Bali kuna Vifungo!!. Msaada upo kwa Yesu Kristo...
Kumbuka: Ukubwa wa msaada unaoupata kwenye ufalme wa Giza, unategemea na wingi na uthamani wa damu iliyomwagika kwayo!!.
👉Hata vifungo hutofautiana kwa sababu ya wingi na uthamani WA Damu iliyomwagika!.
👉Damu ya Yesu inanena Mema kuliko Damu zote!!.
....Somo litaendelea...
By Mwalm Nick
0712265856
WhatsApp#

Comments