MAMBO SABA(7) YANAYOWEZA KUSABABISHA BINTI ASIOLEWE.

Na Mtumishi Peter Mabula.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu ujifunze kitu cha msaada.
Ngoja nikufundishe mambo haya wewe ili yakusaidie na utawasaidia na mwengine ambaye BWANA atawaleta kwako.
Kuna vitu vingi vinaweza kusababisha binti asiolewe kabisa katika amaisha yake au hata akiolewa anaweza kuolewa kwa shida sana na kwa kuchelewa sana.
Wakati mwingine unakuta yeye hajui sababu hata moja kwanini haolewi. unakuta binti anaomba ila hajajua aombee nini maana ombi lake kila siku ni ''BWANA nipe mume mwema''
Tatizo sio BWANA kukupa mume mwema lakini wakati mwingine tatizo huwa kwako wewe ambaye unataka mume mwema lakini kuna kizuizi katika ulimwengu wa roho ambacho  ni lazima ukiondoe kwa maombi makali na kufunga, na wakati mwingine ukiondoe kwa sadaka nzuri kuitoa kwa MUNGU.

Yakobo 5:16C ''Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.''

Je ulishawahi kujiuliza kuomba kwake mtu asiye haki nakuaje?
Najua wewe una haki ya kuomba na kupokea maana umeokoka lakini je umeshawahi kujiuliza usipoomba kwa bidii kama agizo la Biblia itakuaje?
Najua kuna mtu anaenda kupona leo kupitia ujumbe huu.

=Vitu 7 Vinavyoweza kusababisha binti asiolewe.
 

        1.  Utisho wa kipepo.
Jambo hili linaweza kuwa geni kwa walio wengi na wakati mwingine jambo hili linaweza kuwa halieleweki kwa baadhi ya watu.
Lakini kwa ufahamu wangu na uzoefu wangu wa kuombea watu wengi wenye mahitaji ya wachumba niligundua kitu hicho. jambo hili lipo na linatesa baadhi ya watu sana.
Kama Mchungaji au mtumishi anaweza kuwa na utisho wa kiMUNGU kiasi kwamba hata kama wakubwa kabisa serikalini watataka kumfuata kwa ajili ya ushauri au maombezi lazima wajipange na waende kwa tahadhari na heshima kubwa hata kama kikawaida hawana heshima, unadhani ni kwanini? 
Huyo Mtumishi ana utisho wa KiMUNGU.
Kwa sababu kuna utisho wa kiMUNGU basi hata utisho wa kipepo upo na utisho wa kipepo upo kwa lengo la kukukosesha tu baraka zako. Utisho wa kipepo hutoka kwa shetani na mawakala wake.
Binti mmoja mrembo sana aliniambia afanyeje ili aolewe? maana vijana wote wa kanisani wanamuogopa na kusema yeye ni kipuri. nilichogundua kwake ni kwamba hakuwa malaya wala hakuwa na upungufu wowote ila alikuwa na utisho wa kipepo. Kila mtu anamuogopa bila sababu hata moja.
Mfano mtu mwenye mapepo ni rahisi sana kuwa na utisho wa kipepo.
Kuna wengine hata mapepo hawana ila wana utisho wa kipepo.
Kuna watu wanaogopwa sana hata kama ukichunguza kikawaida kabisa utaona hakuna sababu ya kuwaogopa maana hawana tatizo hata moja.
Binti, umewahi kujichunguza kwanini vijana wa kanisani kwenu wanakuogopa sana na siku zote wanakuheshimu tu kama dada yao na sio kuwa na mpango wa kukuchumbia?
Wakati mwingine utisho wa kipepo unakutesa hivyo omba ukiharibu utisho wa kipepo, BWANA YESU siku zote yuko tayari kukushindia kama ukiomba kwa imani na utkataifu ukiwa vazi lako.

Zaburi 55:17 ''Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.''
Omba ndugu 

.      2. Roho ya kukataliwa.
Kuna watu wana roho ya kukataliwa. hawa wako tofauti na wenye utisho wa kipepo. Hawa wao wakati mwingine wanaweza hata wasionekane hata kama wapo.
Kanisani wanaweza kuonekana mabinti wote na wakachumbiwa isipokuwa yeye tu maana ana roho ya kukataliwa.
Ukiona mtu kaolewa maana yake kwanza alikubalika.
sasa wewe mwenye roho ya kukataliwa inabidi utafute kukubalika kwa njia ya kuomba ukiharibu roho ya kukataliwa.
Dalili za roho ya kukataliwa ni 
=kupenda Kukaa peke yako tu katika hali ambayo sio ya kawaida.
=Mwenyewe kutokujikubali wala kujiamini
=Kutokukubalika kila sehemu anayoenda au alipo.
=Kuwa na huzuni isiyo na sababu na isiye ya kawaida huku wakati mwingine akitamani kujiua. na kujiua ni kujipeleka motoni kabisa.
Ni roho mbaya sana na hatari sana.
Ndugu ambaye ni binti au hata kijana au hata mama au baba kama una dalili hizo wewe una roho ya kukataliwa na nakuomba funga na kuomba na umwite BWANA YESU akushindie.
 ''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.-1 Yohana 5:14-15''


       3.Kutokujua kwamba kila jambo na wakati wake.
Mhubiri 3:1  ''Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.''
-Kumbe kila jambo lina wakati wake hivyo usipoujua vizuri wakati wako wa kuolewa inaweza kukusumbua baadae.
Ukiuchezea wakati wako sahihi wa kuolewa inaweza kuja kukusumbua sana baade.
Hapa sisemi mengi maana najua nimeeleweka vizuri.

 

       4. Uchafu.
Kinyume cha usafi ni uchafu.
Kuna uchafu wa aina mbili; Uchafu wa rohoni na uchafu wa mwilini.
Katika suala la kuolewa au kuoa, uchafu usafi wa rohoni na mwilini huzingatiwa sana.
Ukiwa wewe ni mchafu wa mwilini itakusumbua sana kuolewa.
Ukiwa ni mchafu wa rohoni itakusumbua sana kuolewa na mara nyingi ukiolewa utaolewa na mchafu mwenzio wa rohoni. Ndiposa mimi nasema '' Kama wewe ni mzinzi na unahitaji mke/mume basi tarajia kumpokea mzinzi mwenzako''
Siamini kama wewe  wewe mwasherati harafu uombe na kupewa asiye mwasherati. utapata tu mwasherati mwenzio na huyo sio kwamba utapewa na MUNGU bali utajipa mwenyewe maana hata kumpata utampata kutokana na pilika zako za usasherati.
Waebrania 113:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.''


         5.   Tamaa mbaya,dharau na kiburi
Tamaa mbaya ni mbaya tu siku zote na haijawahi kuwa nzuri hata siku moja.
Kudharau na kiburi havifai.
Kiburi ndio mama wa dhambi zote, kiburi ndicho kilimshuka hata shetani.
Ni muhimu sana binti au mwanamke unayetaka kuolewa kuwa makini katika haya maana hakuna ambaye hapendi vitu vizuri. sasa kama wewe umejaa vitu vibaya tu kama tamaa mbaya, dharau na kiburi; ni nani atakutaka?
jibu ni hakuna.
Waefeso 5:3-5 '' Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa KRISTO na MUNGU.''
 

       6. Kuiishi historia ya nyuma.
Inawezekana kabisa kabla hujaokoka ulikuwa mtenda dhambi mkubwa sana hapa mjini.
Inawezekana kabisa dhambi zilikutawala kuanzia kifuani hadi kwenye nywele na magotini(nanena kiroho)
Kuna watu kwa sababu ya historia yao mbaya hukata tamaa na kujiona hawatafanikiwa tena, ndugu hayo ni mawazo yako na sio ya MUNGU juu yako.
Kuna watu wameokoka kweli lakini zamani walikuwa wavaa vimini maarufu lakini wameshindwa kuviacha livha ya kuokoka, ndugu, hiyo inakupunguzia tu CV yako ya kupata mchumba.
Isaya  43:18 '' Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.''
Kuna watu zamani kabla BWANA YESUU hajawaokoa walikuwa ni wadhambi sana lakini licha ya kuokoka ila kuacha kabisa dhambi wameshindwa ila wamepunguza tu dhambi, ndugu, hiyo ni kwa uangamivu wake mwenyewe na kwa habari ya kuolewa hiyo inakupunguzia tu maksi za kuampata mwenzi wa maisha maana ni ngumu kumpata.


      7. Kwa utukufu wa MUNGU.
Sababu ya 7 ambayo inaweza kusababisha binti asiolewe ni hii ya ''Kwa utukufu wa MUNGU''
Inawezekana kabisa katika mabinti 700 binti mmoja tu ndio akawa na sababu hii, hivyo ukiona hujaolewa usijilimbikizie sifa hii ukidhani ni yako.
Kwa utukufu wa MUNGU ina maana 2; maana ya kwamba MUNGU anaweza akamchelewesha mtu kuolewa kwa ajili ya MUNGU kuja kuchukua utukufu mwingi zaidi kupitia ndugu huyu, huyu ndugu kama ni wewe una neema sana. Kama unavyoona MUNGU akifunga tumbo la Hana ili asizae(1 Samweli 1:5) lakini baade sana MUNGU akalifungua tumbo hilo na wakatoka watoto 6 wa ukweli akiwemo nabii Samweli ndivyo vile MUNGU anaweza pia kumpitisha mtu katika mapito ya kukaa muda mrefu sana bila kuolewa maana MUNGU ni MUNGU tu na huwa hapangiwi jambo la kutenda katikati ya viumbe wake anaowapenda sana.
Kwa utukufu wa MUNGU maana yake ya pili ni kwamba kuna watu hata kama ni wachache sana MUNGU ameamua wasiolewe au kuoa katika maisha yao yote. Hiyo haina maoni maana MUUMBA kapanga hivyo MUNGU ni MUNGU tu na anawapenda sana wanadamu wote. Ndugu, Kama MUNGU naweza kuruhusu mtu akazaliwa kipofu na hadi uzee wake wa miaka 90 bado akawa kipofu sio kwamba amekosea kwa MUNGU na na sio kwamba ni adhabu kutoka kwa MUNGU bali ni kwa utukufu wa MUNGU tu , jambo kama hilo linawezekana pia kwa mtu kuishi maisha yake yote bila kuolewa wala kuoa, bila kupata mchumba wala kuchumbia.
Haimsumbuie MUNGU wewe kuwa hivyo maana muhimu sana MUNGU anataka wewe ukaisshi uzima wa milele kama tu utaupokea Wokovu wa BWANA YESU na kuishi maisha mataktifu.
Miaka 70 au 80- ya kukaa duniani sio muhimu sana ukilinganisha na milele ijayo, hivyo ni muhimu zaidi kuitafuta Milele ijayo ya uzima ambayo ipo pekee katika BWANA YESU.

Jitahidi sana jina lako lisiwe kwenye chupa za soda tu bali Liandikwe kwenye kitabu cha uzima wa Milele .
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments