sababu mbili (2) kwanini usome kitabu cha "Dondoo Kuhusu Dhambi"

Bwana Yesu asifiwe
Nataka nikupe sababu mbili (2) kwanini usome kitabu cha "Dondoo Kuhusu Dhambi"
- Sababu hizi mbili ni matokeo baada ya kukisoma kitabu hiki


1). Baada ya kusoma kitabu hiki ni matumaini yangu kupitia dondoo hizi, utapata majibu ya swali hili “Kwanini yatupasa kutunza utakatifu?” Hivyo utaongeza bidii yako kumpendeza Mungu katika mwenendo wako wote. 

2). Kuokoka ni hatua ya kwanza kuliishi kusudi lako. Dhambi ni kikwazo cha kwanza kuharibu kusudi la Mungu katika maisha yako. Basi, kitabu hiki kiwe msaada kwako kuongeza chachu ya wewe kutunza kusudi la Mungu kwa kuepuka kuchafuliwa na dhambi,
KUMBUKA: Neno la Mungu lasema “Msishike, msionje, msiguse” [Wakolosai 2:21]
SAM_1691
Mtumishi Daud Lubeleje
Note: Kitabu hiki kinatolewa buree, cha kufanya Nitumie jina lako, email yako na mkoa ulipo kwenda 0764771298 au Inbox Whatsup kwa namba hiyo. Pia kwenye "comments" za post hii unaweza kuandika details zako
Daudi Lubeleje
VIJANA NA UTUMISHI

Comments