BIBILIA KITABU CHA AJABU KULIKO VITABU VYOTE.


BIBLIA TAKATIFU



NENO LA KWELI LA MUNGU
Jina ''BIBLIA'' limeenea dunia nzima. Limetumiwa na karibu lugha zote zilizopata tafsiri za Biblia. 

Kwanza lilikua neno la kigriki cha kale au kiyunani. linaonekana katika mathayo 1:1  {kitabu cha YESU KRISTO.......} na Luka 4:17 {Akapewa chuo cha nabii isaya, akakifungua chuo akatafuta palipoandikwa} 

na penginenepo katika agano jipya la kiyunani. kwa lugha hiyo liliandikwa ''Biblos'', maana yake ''kitabu''au ''biblia'' maaana yake vitabu.   

''BIBLIA'' ni jina jema kwa kuwa BIBLIA ni ''kitabu cha vitabu'' kwa maana ni kitabu bora kuliko vyote na tena ni ''kitabu chenye vitabu'' yaani ni kusanyiko la vitabu vingi vilivyoungamana kuwa kitabu kimoja.       

 pengine BIBLIA  huitwa ''neno la MUNGU''[Marko 7:13, waebrania 4:12], na pengine hitwa ''maandiko matakatifu'' ua ''maandiko'' [2Timotheo 3:15-16; 2Petro 3:16} 

BWANA YESU akubariki sana.

Ni mimi ndugu yako Peter mMichael Mabula
Maisha ya ushindi Ministry

MKRISTO HARISI HUONGEA NA KUHUBIRI NENO LA MUNGU SIO LA KWAKE
BIBLIA NI NENO HAI

BIBLIA NI NENO LENYE UVUVIO WA MUNGU
MTU HATAISHI KWA MKATE TU BALI KWA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWA MUNGU

Comments