| MKUTANO WA INJLI HUKO MWAKAJE ZANZIBAR, MHUBIRI ALIKUWA NI REV. AMOS LUKANULA |
- 1.KUTUBU. 2.KUBATIZWA. 3.KUPOKEA NGUVU. Katika Biblia kitabu cha matendo 2:38-39 {Petro akawaambia,TUBUNI,MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi MTAPOKEA kipawa cha ROHO MTAKATIFU. kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na kwa watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na BWANA MUNGU wetu wamjie} Ndugu ukitaka kuishi maisha ya ushindi ya kiroho ni lazima kwanza utubu na kumwamini BWANA YESU na kutubu huku maana yake ni kugeuka kutoka dhambini na kumfuata BWANA.Matendo 3:19 Biblia inasema tubuni basi mrejee ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja siku za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA.Kubatizwa katika mwili wa KRISTO kwa maana Roho mmoja sote tulibatizwa wagalatia 3:26-27 {kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa MUNGU kwa njia ya imani katika KRISTO YESU, Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO}
ndugu tunapomvaa KRISTO na kuishi kama MUNGU apendavyo lazima tutadumu kuwa na nguvu za ROHO MTAKATIFU na kama tukimruhusu ROHO MTAKATIFU kutenda kazi ndani yetu hakika tutaishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi siku zote. katika Biblia 1 Yohana 4:13 {katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake naye ndani yetu kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. ndugu kama hujajazwa ROHO MTAKATIFU tamani sana kujazwa na tafuta kanisa la kiroho karibu na wewe na mpe BWANA YESU maisha yako na utajazwa na ROHO MTAKATIFU na kumbuka kuwa bila msaada wa ROHO MTAKATIFU hatuwezi kushinda dhambi. MUNGU BABA akubariki sana na naukutakia mafanikio ya kiroho na kimwili katika maisha yako ukimtegemea BWANA YESU aliye pekee wa kutupeleka uzima wa milele.
UBATIZO WA MAJI MENGI AMBAO UBATIZO WA KIBIBLIA 
UKIWA WA YESU LAZIMA YESU AWE NA WEWE HATA UZIMA WA MILELE
Comments