MGANGA ALINILISHA KIDUDE AMBACHO KILISABABISHA NIFANYE MAPENZI NA MAJINI KILA SIKU

MORASI KACHILA

Naitwa Morasi Kachila ni mwenyeji wa kigoma wilaya ya kibondo. Nina miaka 16 nimezaliwa katika familia ya watoto 6 lakini ambao tupohai ni 2 tu mimi na kaka yangu. Napenda kuwaeleza jambo ambalo BWANA YESU amenitendea maishani mwangu baada ya kupita kwenye mikono ya shetani kwa muda mrefu sana katika maisha yangu na haya mabaya yote yalianzishwa na wifi yangu mke wa kaka na kaka huyo ni mtoto wa baba yangu mkubwa, Huyu wifi ni mchawi sana na ndiye aliyeuwa wadogo zangu wawili na dada yangu 1 na kaka yangu 1. kwa muda wa miaka mingi sikujua haya nilipopata neema ya wokovu tangu utotoni nilikua mgonjwa mgonjwa mwili mzima na watu wote kijijini kwetu walininijua mimi ni mwehu na wakati mwingine nilikua naanguka ovyoovyo na kuzimia na shuleni kila nikishika daftari kusoma kuna mtu ananijia na kuanza kuniongelesha lugha nisiyoifahamu na ilifika kipindi nikawa naongea nae lugha hiyo na wanafunzi wenzangu wakiwa hawajui kinachoendelea na hata akija mimi pekee ndiyo namuona,Wakati huohuo wifi mchawi aliniambia ni lazima tu aniue ila tu bado muda wangu lakini lazima anitoe sadaka kwa mkuu wao. Magonjwa yalipoendelea sana na kuzidi sana baba alimtafuta mganga wa kienyeji ili anitibu, mganga alipoletwa nilikataa kutibiwa na baba, kaka pamoja na huyo mganga walinishika kwa nguvu na mganga akaongea na mashetani yake na baadae akaniambia kuna kitu anataka kunirisha na kitu hicho kitakuwa ulinzi kwangu siku zote za maisha yangu na nilikataa ndipo wakanikamata kwa nguvu na yule mganga kushika mdomo wangu kwa nguvu na kuniwekea kidude kidogo kama kidonge cha panadol kile kidude kilipoingia tu kinywani mwangu kilikuwa cha baridi sana kama barafu na kilipogusa tu ulimi wangu kilienda chenyewe tumboni pila kupelekwa kanakwamba kina akili. Baada ya kumeza kidude hicho ndipo matatizo yalianza upyakwani tangu muda huo mwaka 2006 nilianza kuumwa tumbo chini ya kitovu na hali yangu ikawa mbaya mara mbili zaidi na tangu wakati huo nikilala tu hata sijasinzia alikuwa anakuja jini na kuniangalia tumboni na akiniangalia tumboni kile kidude kinatoka na kwenda kiganjani mwake na yeye kuniingilia  kimwili na akimaliza anakirudisha kwa kukielekezea tumboni mwangu, maaumivu niliyokuwa nayapata nayajua mwenyewe kwani ni hatari. Napenda kukuambia ndugu kuwa hakuna mganga wa kienyeji asiye mchawi na hakuna msaada wowote kwa waganga wa kienyeji ila wanachofanya ni kukuongezea jini ili kukupoza tu na baada ya miezi hali hurudi na kipindi hiki hali inakuwa mbaya zaidi ya mara ile ya kwanza hayo nimeyashuhudia mwenyewe kwa macho yangu Tangu hiyo 2006 niliendelea kuumwa na kulala na majini kila siku huku wifi akiniambia hadharani kuwa yeye ndiye aliyeyafanya haya mateso kwangu kwa sababu mimi nina kiburi na pia sababu wakuu wake wa uchawi wamemkataza kuniua maana nyota yangu inang'aa sana hivyo wataniua wakati wa mkutano wao mkuu na siku hiyo watanitafuna mzima mzima.. Mateso hayo yaliendelea hadi 2010 mwezi wa 7 alipokuja mjomba wangu aliyeokoka na anakaa zanzibar. Siku mjomba amekuja aliniambia nijiandae kwani akitaka kuondoka ataondoka na mimi ili nikaishi kwake huko zanzibar. ndugu zangu wachawi huwa wana mambo mengi sana kwani sikujua kwamba huyu wifi kajuaje kwamba naondoka wakati mkutano wao mkuu wa wachawi ulikuwa umekaribia ndipo siku moja kabla ya kuondoka kwenda zanzibar nikiwa shambani na mama ghafla nilianza kujisikia vibaya na ghafla akatokea nyoka mkubwa na kunizonga mwili wangu wote huku mama akishuhudia
MORASI KACHILA AKIWA ZANZIBAR
  { ndugu habari hii itaendelea kesho hapa maisha ya ushindi na ni tukio la kweli na mimi mkurugenzi wa maisha ya ushindi nilishiriki maombezi ya morasi kule zanzibar na haliyake kule zanzibar ilikuwa mbaya zaidi kwani majini yaliongezeka kutoka 1 hadi zaidi ya kumi hayo atayaeleza kesho pia atakueleza jinsi alivyofunguliwa kwa maombi na jinsi alivyopelekwa mbinguni na kuonyeshwa maisha yake yote yalivyokuwa tangu utoto wake pia jinsi baba yake alivyo na miguu bandia bila yeye kujijua pia jinsi alivyomwona BWANA YESU na kupewa jukumu la kufanya kwa ndugu zake na marafiki zake.MUNGU BABA akubariki sana na kama una habari ya kweli au habari ya kweli au ujumbe wa neno la MUNGU usisite kututumia kwa email hii mabula1986@gmail.com }

Comments