WATU WA MUNGU WALIOMPA BWANA YESU MAISHA YAO WAKISALIMIANA BAADA YA IBADA KUISHA HUKO CHUKWANI ZANZIBAR |
![]() |
WATU WANAOTAKA KUMPA BWANA YESU MAISHA YAO WAKINYOOSHA MIKONO YAO ILI WAONGOZWE SALA YA TOBA TAYARI WAFANYIKE WATOTO WA MUNGU . |
Mtu kabla hajaokoka anaonekana katika mitazamo miwili isiofaa:
1.kama mfu yaani alikuwa amekufa WAEFESO 2:1-3[Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu, ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kumfuata mfalme wa uwezo wa anga , roho yule ataendaye kazi sasa katika wana wa kuasi, ambao zamani sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapendi ya mwili na ya nia tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine}
2.MPOTEVU yaani ulikuwa umepotea LUKA 15:4{Ni nani kwenu mwenye kondoo mia akipotewa na mmoja wapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?}
Hivyo mtu mwenye dhambi anafananishwa na:
1.kondoo aliyepotea LK:15:4-7
2.shilingi iliyopotea LK 15:8-10
Comments