CHRISTMAS NI UKUMBUSHO WA KUJA KWA UKOMBOZI DUNIANI

RAPHAEL MBOGO WA KURASINI DAR ES SALAAM

Bwana Yesu asifiwe?
Mungu kwa nguvu zake ametupenda sana kwa kuwa tangu kuumbwa misingi ya ulimwengu aliwapenda wanadamu.Baada ya mshitaki wetu Ibilisi kumfanya mwanadamu amkosee Mungu kwa kutokutii{mwanzo 3:1-13}kwa kumkosea Mungu wanadamu tumehesabiwa kuwa tuko uchi,soma vizuri kitabu cha Mwanzo,Adam na Hawa hawakujua kama wako uchi..ndiyo matendo machafu ambayo yanatutenga mbali na Mungu.tulikufa kwa kuirithi dhambi hiyo{efeso 2},naye Mungu akafanya mapinduzi ambayo Shetani amelala chali,Mungu akanena kwa midomo ya nabii Isaya kwamba tutapokea ishara kuwa Bikira atachukua Mimba naye atamzaa mtoto nasi kwa KUMTII yeye tumekombolewa{isaya 7:14,yohana 3:16}..Tumekombolewa kwa yeye Yesu mwana wa Mungu..MUNGU awabariki sana na nawatakia sikukuu njema na tusherekee kwa amani na upendo. By Raphael mbogo

Comments