Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
KATIKA MAGUMU KAMA HAYA MUNGU PEKEE NDIO MSAADA ULIO WA KARIBU KWANI YEYE HUJIBU MAOMBI |
Kuna
dada amenielezea mambo ambayo kweli anahitaji msaada lakini moyo wake
mgumu kuhusu kumpa YESU KRISTO maisha yake MUNGU ampe moyo wa nyama huyu dada aliolewa katika familia yenye mambo
ya giza kuna siku alishuhudia mama mkwe wake akichukua nguo za mwanae
na kumvisha kondoo na huyo kondoo alizikwa akiwa hai huyu binti baada ya
kuona hivyo akatoroka ukweni na watoto wake mapacha wakiwa na miezi
6 alipofika kwao baba yake akamfukuza arudi huko huko alitoka
atafute mahali pa kwenda alipokuwa njiani mdogo wake akamkimbilia
akamwambia baba amewaweka watoto kwenye kiroba anakwenda kuwatupa maana
anadai mtoto wake aliolewa bila watoto alirudi mbio nyumbani akakuta
kiroba kimetupwa kando ya barabara mdogo wake akikitambua kile
kiroba wakakifungua na kuwakuta watoto wake wakiwa wamechoka
sana baada ya hapo akapata mfadhili akaja dar kwa dada yake akijua sasa
atatulia dada yake alikuwa ameolewa na watoto 3 siku moja dada yake
alimfumania mumewe wakati anatoka katika fumanizi yule mama alipata ajali
na kufa hapo hapo hivi sasa analea watoto 5 yaani wake 2 wawili na wa dada yake marehemu watatu na ni mama lishe na hali ni mbaya sana napenda
aokoke ila anahitaji maombi hivyo tumwombee. BY HELLEN WANDE


- Get link
- X
- Other Apps
Comments