HERI ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MARAFIKI WA MAISHA YA USHINDI{3}



 BWANA YESU asifiwe. namshukuru MUNGU kwa uzima aliotupa hadi hii leo Dec 25 tunasherekea ukumbusho wa kuja kwa ukombozi duniani maana hakuna uzima popote ila ni kwa YESU KRISTO {Yohana 14:6}. Ndio maana dunia nzima ni shangwe na furaha kwa tukio ambalo limetokea miaka 2012 iliyopita ambapo siku YESU anazaliwa malaika ambao ni jeshi la mbinguni walishangilia na kumsifu sana MUNGU{Luka 2:8-14} na siku hiyo hiyo YESU mwanaume wa ajabu anazaliwa watu wenye heshima na watawala walimsujudia {Mathayo 2:11} hao walijua kuwa aliyezaliwa ni MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana. Pia YESU alizaliwa kwenye hori la ng'ombe ashilio la kwamba wanyama wapumzike maana hakuna tena sadaka ya kuteketezwa kama ilivyokuwa zamani  maana YESU ni dhabihu idumuyo milele ili watu wasamehe dhambi zao na kuurithi uzima wa milele bure kupitia yeye {Waebrania 9:12-15}.na tunasherekea christmas kwa kumwabudu MUNGU na kuonyesha upendo kwa wengine na kuhakisha kwamba  YESU anatenda jambo jipya mioyoni mwetu ili tuzidi kuishi katika neema yake maana kwa ajili yake na kwa neema yake alituhamisha kutoka kwa shetani na sasa tuko huru mbali na kuonewa na wachawi na hata nguvu zozote za giza. HIZI HAPA NI BAADHI TU YA SALAMA ZA KUTAKIANA HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU PAMOJA NA MARAFIKI NA WASOMAJI WA BLOG HII

 NAITWA VERO ROBERT WA NAIROBI KENYA kwanza Asante sana mtumishi wa MUNGU, Nawatakia heri za christmas na mwaka mpya  familia yetu yote baba na mama na mwanangu BRIGHT, marafiki zangu woote MUNGU awabariki sana na tusherekee kwa upendo na utu wema na matendo mazuri ya kumpendeza MUNGU .
VERO ROBERT
NAITWA EMMANUEL SUNGURA WA ARUSHA TANZANIA katika kuwatakia heri ya sikukuu ya christmas na mwaka mpya naanza na wewe  pia Emmanuel Mwakabana,Adamu Esau,George Sanga,Penuel paul Mtafya,Steven Mwikwabe,Wittness Godwin,Sophia Dikson Mhando,Frola Daud na marafiki wanaompenda YESU KRISTO popote walipo na MUNGU awabariki sana

Comments