BWANA YESU asifiwe. namshukuru MUNGU kwa
uzima aliotupa hadi hii leo Dec 25 tunasherekea ukumbusho wa kuja kwa
ukombozi duniani maana hakuna uzima popote ila ni kwa YESU KRISTO
{Yohana 14:6}. Ndio maana dunia nzima ni shangwe na furaha kwa tukio
ambalo limetokea miaka 2012 iliyopita ambapo siku YESU anazaliwa malaika
ambao ni jeshi la mbinguni walishangilia na kumsifu sana MUNGU{Luka
2:8-14} na siku hiyo hiyo YESU mwanaume wa ajabu anazaliwa watu wenye
heshima na watawala walimsujudia {Mathayo 2:11} hao walijua kuwa
aliyezaliwa ni MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana. Pia YESU alizaliwa
kwenye hori la ng'ombe ashilio la kwamba wanyama wapumzike maana hakuna
tena sadaka ya kuteketezwa kama ilivyokuwa zamani maana YESU ni
dhabihu idumuyo milele ili watu wasamehe dhambi zao na kuurithi uzima wa
milele bure kupitia yeye {Waebrania 9:12-15}.na tunasherekea christmas
kwa kumwabudu MUNGU na kuonyesha upendo kwa wengine na kuhakisha kwamba
YESU anatenda jambo jipya mioyoni mwetu ili tuzidi kuishi katika neema
yake maana kwa ajili yake na kwa neema yake alituhamisha kutoka kwa
shetani na sasa tuko huru mbali na kuonewa na wachawi na hata nguvu
zozote za giza. HIZI HAPA NI BAADHI TU YA SALAMA ZA KUTAKIANA HERI YA
CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU PAMOJA NA MARAFIKI
NA WASOMAJI WA BLOG HII.
![]() |
DIANA NATASHA MUHANGO |
Comments