JE NITAJUAJE KUWA HUYU MCHUMBA WANGU NI CHAGUO LA MUNGU?

Swali: Nitajuaje kuwa anayenichumbia ni chaguo la Mungu? Make kuna wimbi la matapeli wa mapenzi?
Jibu:    Ukiwa mtoto wa Mungu, atakujulisha kuwa huyu ndiye, Mungu ana njia maelfu za kufunua yale Tusiyoyajua. Kinachotakiwa ni kukubali kuwa watoto wake ili tuisikie sauti yake, kama Baba anavyoongea na Mwanae ndivyo Mungu anavyojifunua kwa watoto wake.


Angalia mfano wa Mcha Mungu alivyompatia Isaka Mke aliyechaguliwa na Bwana, aliweka vigezo ambavyo Mungu alimuongoza Binti kuvitimiza, Isaka akajitwalia Mke wa kuchaguliwa na Bwana.
Mwanzo 24:13-14 [Kwa faida yako soma kisa kizima : Mwanzo 24:1-67]
“Tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji, basin a iwe hivi; Yule msichana nitakayemwambia, tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili Bwana wangu”. Nina mifano Mingi ya namna hii.

NB: Jambo la kusikitisha, ndoa nyingi leo ni ndoano zilizotegwa na yule Adui ambaye ndiye mwanzilishi, hebu jiulize ni Mungu yupi anayehamasisha NGONO kabla ya Ndoa? Na siku hizi vijana wengi wanadai ku “test” kwanza ndipo wafunge Ndoa. Kwa hiyo wengi leo wamekuwa Mboga za kuonjwa na mwishowe kuishia kuachwa, lakini hata wakioana kwa mtindo huo wasipotubu na Mungu kuwasamehe, Ndoa haiwezi kuwa Salama, kwani anayeisimamia ni ADUI bila kujali sala za wachungaji. Amri inasema USIZINI. Anayeendelea na Dhambi Maombi yake ni Dhihaka kwa Mungu. Waebrania 6:4-6.

Vijana Mungu anawapenda na wakati wote anawawazia MEMA kwa siku zijazo, mnayoyaona ni furaha sasa hivi ni mashimo marefu ya siku za usoni katika maisha ya familia. Kubali Yesu atawale maisha yenu ili mpate kuishi maisha ya furaha na AMANI.MUNGU akubariki sana na nakutakia maandalizi mema ya Christmas na mwaka mpya.








Comments

Unknown said…
Ubarikiwe sana kwa somo zuri.
Peter Mabula said…
amen mtumishi wa MUNGU