KUMRUDIA MUNGU HUPELEKEA KUOKOLEWA HATA NA WENGINE NJE NA WEWE





2 Nyakati 30:9 {kwa kuwa mkimrudia MUNGU ndugu zenu watahurumiwa machoni pa hao waliowachukua mateka nao watairudia nchi hii......}. ndugu zangu kutubu kwako au kugeuka kwako kutoka mienendo na matendo mabaya  kutasaidia sana kuponya hata familia yako au ndugu zako mfano kuna mama mmoja ambaye alikuwa mcha MUNGU lakini familia yake yote kuanzia na mmewe na watoto wake walikuwa wanatenda mabaya hata hayaelezeki na binti zake wawili walikua wanajiuza lakini huyu mama aliendelea na kudumu kutubu kwa ajili ya watoto wake na mme wako baada ya miezi kadhaa atubu kwa ajili yake na kwa ajili ya familia yote pia avunje maagano yote ya ukoo kwenye familia hiyo na mama huyo akafanya hivyo na katika kutubu binti yake mmoja aliyekuwa kahaba akaona aliyekua akijiandaa kwenda kujiuza akaona msalaba angani na akasikia sauti kwamba aende kanisani binti yule akakimbilia kanisani maana hofu ilimwingia na alipofika akaombewa na mapepo yakamtoka na kuanzia siku hiyo akaokoka na hadi sana anaendelea na wokovu tena mwaka jana kaolewa na maisha ni mazuri tena ya utakatifu hadi sana na baada ya muda familia yote ya yule mama waliokoka na hadi leo hii wanamtumikia MUNGU. hivyo kugeukwa kwako kunaweza kuiokoa familia yenu na hata nguvu za giza zinazowasumbua zitakoma pia Biblia inasema katika Matendo 12:5 [Basi petro akalindwa gerezani nalo kanisa likamwomba MUNGU kwa ajili yake} ukiangalia habari hii ya Petro tunaona  kuwa MUNGU alijibu maombi ya kanisa na Petro akaachiwa na kuwa huru tena. Tunaomba kwa ajili ya wengine kwa sababu ''BWANA yu karibu kwa wote wamwitao kwa uaminifu, Atawafanyia wamchao matakwa yao Nae atasikia kilio chao na kuwaokoa'' Zaburi 145:18-19.  pia Biblia inasema katika Zaburi 86:5 Kwamba ''Kwa maana wewe BWANA u mwema, umekuwa tayari kusamehe na mwingi wa fadhili kwa wote wakuitao'' pia yakobo 4:8 { Mkaribieni MUNGU naye atawakaribia ninyi, itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili} Hivyo ndugu omba sana kwa ajili ya ndugu zako na marafiki na MUNGU atakusikiliza wewe mwenye haki kwa ajili ya hao . MUNGU BABA wa mbinguni akubariki sana

Comments