Kama
ulishawahi kuwa na mahusiano na mtu yeyote, na ukafanya naye tendo la
ndoa, alafu baadae ukavunja yale mahusiano hukumuoa au kuolewa naye,
ujue uliingia naye kwenye agano, unawezakuta mtu ana maagano ya ndoa na
watu kumi au zaidi anatembea nayo na Mungu anayafahamu. Haijalishi
uliingia kwenye maagano na watu wangapi, kama ni kumi, watano, mmoja
wataje mbele za Mungu na uvunje yale maagano uliyopatana
nao, mmoja baada ya mwingine. Sasa shida hapa inakuwa kwamba usipofanya
hivyo, lile agano na machozi ya uchungu ya yule uliyemuacha
yatakuandama popote, utajikuta hata sehemu nyingine mambo yako hayaendi
vizuri kumbe kilichokufunga ni maagano.Au kama ulishawahi
kutoa mimba, au kumshawishi mtu atoe mimba na akatoa, ujue pia uliingia
kwenye agano, unahitaji kuomba na kutubu mbele za Mungu, tena kwa
kumtajia Mungu, kama ni mimba kumi sema, kama ni tano sema, kama ni moja
sema, alafu vunja hilo agano na kutubu kwa damu ya Yesu. Upo hapo????





Comments