 |
WATU WAKIWA KATIKA SEMINA YA NENO LA MUNGU VIWANJA VYA JANGWANI |
Kundi
kubwa la watu lilikuwa linakusanyika, na watu walikuwa wanamjia Yesu
kutoka kila mji. Naye akawaambia mfano huu: "Mpanzi alikwenda kupanda
mbegu zake. Alipokuwa akipanda zile mbegu, nyingine zilianguka njiani,
na wapita njia wakazikanyaga, na ndege wakazila.
Nyingine zilianguka
penye mawe, na baada ya kuota zikanyauka kwa kukosa maji, Nyingine
zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota
ikazisonga.Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota na kuzaa
asilimia mia. Baada ya kusema hayo, akapaaza sauti, akasema, "Mwenye
masikio na asikie! {Luka 8:4-8} ndugu zangu mbegu zinazozungumzwa hapa
ni neno la MUNGU na linapandwa moyoni mwako ili liote na kuzaa mema
yanayompendeza MUNGU. hivyo ndugu hakikisha unakuwa udongo mzuri na
usikubali kupokea na neno harafu hulifanyi kazi bali unakuwa msikiaji tu wa neno la MUNGU lakini huwezi kuishi
sawasawa na neno linavyotaka na kitu hiki ni machukizo hapa BWANA YESU
alikuwa akiwafundisha watu wengi ambapo alitaka wawe watendaji wa neno
na sio wasikiaji tu na hata leo anatutaka mimi na wewe tuwe watendaji wa
neno hebu angalia ufafanuzi wa BWANA YESU kwako na kwangu kuhusu
tunavyolisikia neno ambalo MUNGU anapanga mioyoni mwetu kupitia
matumishi wake "Basi, maana ya mfano huu ni hii: mbegu ni neno la Mungu.
Zile zilizoanguka njiani zinaonyesha watu wale wanaosikia lile neno,
halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini na hivyo
wakaokoka.Zile zilizoanguka penye mawe zinaonyesha watu wale ambao
wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Hata hivyo, kama zile
mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na
wanapojaribiwa hukata tamaa.Zile zilizoanguka kwenye miti ya miiba ni
watu wale wanaosikia lile neno, lakini muda si muda, wanapokwenda zao,
husongwa na wasiwasi, mali na anasa za maisha, na hawazai matunda
yakakomaa.Na zile zilizoanguka kwenye udongo mzuri ndio watu wale
wanaolisikia lile neno, wakalizingatia kwa moyo mwema na wa utii. Hao
huvumilia mpaka wakazaa matunda.'' {Luka 8:11-15}. kumbe neno
tulilofundishwa na tunalofundishwa tuwe tunalifanyia kazi ila liwe ni
neno la kutoka Biblia sio mtu akufundishe neno lake huku akikuambia ni
neno la MUNGU ndio maana tunaambiwa zipimeni kila roho je zinatokana na
MUNGU au ni mwanadamu tu kwa matakwa yake au ni shetani? . ubarikiwe
sana na nakutakia siku njema ilia kumbuka kuwa mtendaji wa neno na sio
msikiaji wa neno.YESU KRISTO ANATUPENDA NA NDIO MAANA AMETUCHAGUA ILI TUURITHI UZIMA WA MILELE KUPITIA YEYE
 |
YESU KRISTO NI MUNGU PAMOJA NASI
 |
YESU KRISTO ANATUPENDA NA NDIO MAANA AMETUCHAGUA ILI TUURITHI UZIMA WA MILELE KUPITIA YEYE |
|
Comments