MAANA TUMEPEWA MTOTO MWANAUME NA UWEZA WA KIFALME UTAKUWA BEGANI MWAKE


KESHO NI SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAKRISTO KOTE ULIMWENGUNI TUNASHEHERKEA KUZALIWA KWA MWOKOZI WA WANADUMU WOTE YESU KRISTO {Yohana 14:6}. Habari ya kuzaliwa kwa BWANA YESU inapatikana sehemu nyingi sana kwenye Biblia takatifu kuanzia agano la kale hadi agano jipya. katika agano la kale nabii isaya anatoa unabii wa kuzaliwa kwa YESU katika Isaya 9:6-7 {Maana tumepewa mtoto mwanaume na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake MSHAURI WA AJABU,MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE NA MFALME WA AMANI. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo}. NDUGU UKIWA KWA YESU UKO KATIKA MIKONO SALAMA  NA HAKUNA UZIMA WA MILELE KWINGINE NJE NA YESU. pia katika agano jipya Luka 2:6-14 {Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia,   
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.Malaika akawaambia, "Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kuu kwa watu wote.Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini."Mara kundi kubwa la jeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika, wakamsifu Mungu wakisema:    "Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu aliopendezwa nao!}. MUNGU akubariki sana wakati huu wa kushehrerkea ukombozi wa wanadumu. na burudika na nyimbo hizi  za Christmas. na furahia sikukuu hii kwa amani na upendo pamoja na matendo mema.
















Comments