NILINYOLEWA NYWELE ZOTE SEHEMU ZA SIRI NA WACHAWI USIKU NIKIWA NIMELALA


Naitwa Prisca mwenyeji wa mkoa wa Arusha napenda nishuhudie kitu ambacho kimetokea maishani mwangu hadi kupelekea kuokoka. mwaka 2010 kwa sababu ya kutafuta maisha nilikwenda zanzibar kuishi huko na nilipata chumba cha kupangwa maeneo ya airport na niliishi vizuri tu na majirani ambao tulikua tumepanga pamoja  na kama binadamu ukiwa bado unayapenda ya dunia na shetani ametawala maisha yako niliamua kuwa na mpenzi mwanajeshi na uhusiano wetu uliendelea kwa muda kidogo. Baada kama ya miezi 6 nilianza kupatwa na matatizo mara niugue ghafla na nikienda kupima naambiwa sina ugonjwa wowote na hadi nilienda kwa mganga wa kienyeji maeneo ya unguja ukuu lakini ndio kwanza matatizo yaliongezeka. Baada kama ya mwezi mmoja baadaye vituko viliongezeka maana siku moja nilikuta nywele upande mmoja wa kichwa zimenyolewa zote ukweli nililia sana na kusema MUNGU mbona haya yananipata mimi? siku mbili baadae nikiwa natoka kazini maana nilikua hotelia nilikuta watu wananiongea mimi na nilijificha ili nisikie kile wanasema niliwasikia wakisema ''HILI LI DADA NI LI KICHWA NGUMU SANA YAANI LICHA YA KULITUMIA MAJINI YAKALILALA NA LICHA YA KULINYOA NYWELE KICHWANI BADO TU HALITAKI KUMWACHIA HUYU MWANAUME AMBAYE AMETUKATAA SISI WENYEJI NA KULIKUBALI HILI JINGA SASA HUYU MWANAUME ATA-SHARE MAPENZI NA MAJINI YETU HADI ATAMCHUKIA '' nilishtuka sana na kuanza kulia na baada ya muda nilisikia mmoja akisema ''LEO NDIO FINAL NA BAADA YA LEO ATAMWACHA TU HUYU MWANAUME'' nilishindwa kujizuia na kutokea na kuwambia mbona kunitesa hivyo je kosa langu ni nini? walicheka sana  na dada mmoja kati yao akaniambia kama najipenda niachane na Sam ambaye ndiye mpenzi wangu na tulikua tumepanga kuoana kabisa niliingia ndani na kuanza kulia na jioni hiyo Sam alikuja na kunikuta nalia lakini nilimdanganya kuwa tumbo linauma ndio maana nalia na yeye kunisaidia na baadaye alienda kazini jioni hiyohiyo. siku hiyo nilisema silali ili nione kitakachoendelea na hata sijui nini kilitokea maana nilijikua nimeshalala na niliamka asubuhi na kukuta sehemu zangu za siri zimechafuka na pia kubwa kuliko yote na ambalo limesababisha kuandika haya ni kuwa nywele zote za sehemu yangu ya siri zilikua zimenyolewa na wembe nililia na kujiuliza maswali mengi sana yasiyo na majibu kwamba hivi inawezekana kweli mtu ukanyolewa nywele zote za sehemu ile bila kujijua? . Asubuhi waliendelea kunicheka na kusema walichobakiza ni kuniua. Nilikaa bila amani kwa zaidi ya wiki tangu siku hiyo huku kila siku nikisikia vitisho usiku kila siku mara kelele,miabga ya ajabu ajabu,na vitisho vingi mwisho nikakata tamaa ya kuishi na siku moja nikawaza kama ni kufa ngoja nikafie kanisani japokuwa mimi nilikua mpagani. Kesho yake baada ya siku hiyo nilienda kanisani la kilokole na kukuta vijana na watoto kama 7 wakiimba kwaya niliwauliza mchungaji yuko wapi wakaniambia mchungaji wao yuko safarini  Dar nilichukia sana na mkubwa wa wale vijana akanikaribisha kukaa na kusikiliza nyimbo nikamwambia nina shida na mchungaji na nataka aniombee kwani nina matatizo makubwa na nakalibia kufa yule kijana alinitazama na kuniuliza kwamba '' UNAAMINI KWAM,BA YESU KRISTO ANAWEZA KUKUPONYA?'' nilikubali akaniambia nipige magoti na wao wataniombea kiukweli nilikataa maana nilijua labda mchungaji pekee ndio anaweza kuniombea na si waoa ambao wote nawazidi umri hata kama yule kaka kiongozi ni kama namzidi miaka 3 naye ni mwanajeshi. Kaka yule alinisihi sana na kuniambia sio mchungaji anayeponya bali anayeponya ni MUNGU na wao watamwomba MUNGU na mimi nitapokea uponyaji. Nilikataa na kusema nitakuja siku mchungaji akirudi  lakini moyo unakataa na kusema naweza kufa kabla mchungaji kuja mikakubali lakini kwa masharti kwamba aniwekee mkono yule kiongozi wao tu na sio wale watoto yule kaka akaniambia ni mwamini MUNGU wanayemwabudu kwani hakuna linaloshindikana kwa JEHOVAH na akaniambia kwamba nitashuhudia kanisani kile ambacho MUNGU atatenda kupitia watoto hao kweli nilikubali kuombewa na wakaniombea nikapoteza fahamu na baada ya muda nikazinduka nikiwa nimepona yule kijana akaniambia kwamba nilikua na mapepo mengi sana  lakini YESU amenifungua na kweli nilijihisi mwepesi na niko tofauti sana na nilivyokuja na wakaniwekea mikono tena kuniombea ulinzi wa MUNGU na baada ya hapo wakaniambia sitachezewa tena na wachawi labda tu nimwache huyu YESU aliyeniponya . Niliwaahidi kwamba sitamwacha YESU na nitamshawishi mchumba wangu naye aokoke. Nilirudi nyumbani hakuna aliyeniongelesha na yule dada nilimkuta analia na kusema nimemkomesha kwani majini yake yote 51 yamekufa. sikusema kitu na nikaingia ndani na kumshukuru sana MUNGU hata kama nilikua sijajua kuomba lakini kwa maneno machache niliomba. Tangu muda huo sikupatwa na tatizo lolote na niliishi kwa furaha na niliamua kumweleza yote mchumba wangu akashangaa na akakubali kuokoka hivyo tangu feb 2011 akaokoka na baadae tukaoana na hadi sasa tuko ndani ya YESU. sina la kusema ila namshukuru sana BWANA YESU kwa kuniponya na kuniokoa na hadi sasa niko salala sifa na utukufu ni kwa MUNGU BABA wa mbinguni. AMEN.
picha hii haihusiani na Prisca lakini inaonyesha jinsi BWANA YESU anavyotenda miujiza  kwa kuponya mangoja na nkufungua kila kifungo cha adui kilichokuwa kimefunga watu

Comments

Unknown said…
IN THE NAME OF JESUS'''Yote yanawezekana
Peter Mabula said…
hakika kwa YESU yote yanawezekana